TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

R.I.P Ruge Mutahaba
Nisauti ya millard katika kipindi cha amplifier saa mbili na dk42 anathibitisha kutokea kwa kifo cha manager huyo wa CMG.
 
Wakati mwingine huwa najiuliza Mwenyezi Mungu anatumia criteria gani kuchagua nani afe na nani abaki hai.

Inatia simanzi pale Mwenyezi Mungu anapoamua kumchukua kiumbe mwema ambaye ana mchango mkubwa na msaada kwa jamii na kuwaacha hai watu ambao hawana msaada wowote kwa binadamu wenzao zaidi ya kupanga nani atekwe, nani awekwe kwenye kiroba akatupwe baharini, nani apigwe risasi zaidi ya 30, nani abambikiwe kesi ya mauaji ya Akwilina na nani afunguliwe mashataka ya kesi ya uchochezi na anyimwe dhamana!

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya mdogo wangu Ruge Mutahaba mahali pema peponi. Tutamkumbuka kwa mambo mengi mema na mazuri aliyoyafanya hapa dunia. Amen.
 
SO SAD KWA KWELI
 
Mungu amuweke panapostahili, ameondoka angali bado Taifa linamhitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…