Leo katika msiba wa Ruge Mutahaba nyumbani kwa mama yake Mikocheni jijini Dar es salaam, kumeibuka taaruki baada ya kuonekana mkurugenzi wa Efm na Etv Francis Antony Ciza Majey (Majizo) akiwa katika msiba huo na kuonesha ushilikiano mkubwa sana katika siku hii ya msiba wa ndugu yetu Ruge Mutahaba.
[
https://2]
Alipo ulizwa ni kwanini anashiriki kwa moyo mmoja katika msiba wa mtu aliyekuwa katika media nyingine alijibu ya kwamba
"Mimi ninafanya media kama hobby na sijali kama nitaweza kushuka kibiashara ama sitoshuka kibiashara kwasababu hata nikishuka itakua ni basi kwasababu sina bifu na mtu yoyote wala media yoyote na sifanyi kushindana ninafanya media kama kitu ambacho ninakipenda, na kuhusiana ma Ruge yeyepia alikuwa anamchango wake mpaka mimi kufikia hapa nilipo na ndio maana unaona ninakuwa na mchango mkubwa hapa katika msiba wake kwasababu ninakumbuka Msaada wake"
Maneno hayo alifunguka Majizo aliipoojiwa na waandishi wa habari pale nyumbani kwa mama yake na Ruge Mikocheni.
Mwili wa Ruge unatarajiwa kufika siku ya Ijumaa ukitokea Afrika Kusini na kuagwa Jumamosi na kisha utasafilishwa mpaka kwao Bukoba Kwa shughuli za mazishi kama ilivyo amuliwa na Familia ya Ruge Mutahaba.
[
https://4]
CHANZO
www.msakaji.com
Sent using
Jamii Forums mobile app