TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Msanii wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro maarufu kwa jina la 'Chid Benz’ amesema marehemu Ruge Mutahaba ameondoka na Password.


Chid Benzi ameyasema hayo leo Jumatano, Februari 27,2019 alipokuwa akizungumzia mchango wa Ruge katika muziki kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi .



Msanii huyo aliyewahi kutesa na wimbo wa Dar es Salaam Stand up, amesema Mkurugenzi huyo wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, ameondoka na password ya muziki na mpaka kuifungua itachukua takribani miaka saba.



“Kuna vitu Ruge alivitawala kwenye muziki na mpaka atokee mtu avijue sio leo wala kesho kwa kuwa vingi alikuwa akivifanya mwenyewe, kiukweli tumepoteza mtu wa muhimu,” amesema msanii huyo.



Kuhusu watu wanaomsema vibaya, Chid amewaita wapumbavu kwa kile alichodai hakuna msanii ambaye hajawahi kudhulumiwa kwenye maisha ya muziki na kutaka wanayemuongolea vibaya waulizwe vizuri wamedhulumiwa nini au wanawake?


“Watu kama sisi tushadhulumiwa, tushatapeliwa , tumepata mahela, tumevuta madawa tumeacha yaani tumefanya vitu vingi kwenye muziki lakini bado tunamuona Ruge mzuri, huyo anayesema katapeliwa amemchukulia mwanamke au muulizeni vizuri”.



Ameendelea kueleza kuwa Ruge amefanya vitu vingi katika muziki na anaamini watu walikuwa hawajui namna anavyofanya hadi leo kuacha alama na watu kumlilia.


Hata hivyo, Chid Benz amesema kwenye muziki kunahitaji watu tofauti na kuhoji kwamba hivi leo angekuwepo Shigongo tu ina maana watu wangekuwa wanapata taarifa tu na kubainisha kuwa kunahitajika watu kama kina Ruge kina Mengi, Diamond, Chid Benzi na wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa!Nimejikuta nakumbuka msiba wa Kabwe ambapo binti wa marehemu aligoma kumpa mkono RC Makonda!
Si vizuri kushirikiana watoto mambo ya kiofisi wakati wao hawako hiyo ofisi !! Na watoto wanatakiwa kukua baba akiwa mwizi akitumbuliwa usinune anachukia nini ulitaka baba yako aendelee kuwa mwizi akiibia serikali? Huko kununa kwaweza haribu future ya mtoto.Akaeleweka kuwa mtoto wa mwizi ni mwizi hivyo hata akipewa post atakuwa mwizi kama baba yake.Hata kama ana hasira angetungua tu Kilio na kutoa mkono au angekuwa neutral.Hicho kitoto kinaonyesha kipenda Ufisadi na kilillelewa na pesa za kifisadi Kasi kuwa zilipokata kikawa na hasira na watumbuaji waliotumbua baba yake.Mtoto usimshirikishe ya ofisini usipende kusimulia ya ofisini hasa mabaya kauka wajaze wenyewe.Usiseme ohh naonewa nk wakati wewe mwizi ofisini utaharibu future za watoto wata misbehave siku ya msiba kwa wasiojua kama huyo mtoto.Kajipa permanent damage ya future yake
 
Child mkomavu na yuko vizuri, hasa alipoacha na hata akiongea anaeleweka.
 
Back
Top Bottom