Kila ilipokuja suala la kulaumiwa aliyetangulia kulaumiwa ni Ruge Mutahaba,
kwa logic ya kawaida nauliza tu
kwani wasaniii walikuwa wanalazimishwa kufanya kazi na clouds? mbona vituo vilikuwa vingi sana kama vile magic, Radio one, Ea radio, na Times Fm, bila kusahau RFA ya mwanza?
Kwa akili ya haraka ni mjinga pekee atakaye lalamika kwenye open market ambayo hulazimishwi na yeyote kuchagua nani wa kufanya naye kazi,
Nilichogundua kwa haraka haraka ni kwamba ubunifu wa Mr Ruge ulifanya kila mtu aisikilize clouds fm na kila msanii atamani kufanya kazi na Clouds fm, lakin ikifika suala la mapato ndo panaleta matata, Kwa dunia hii huria huwezi kukubaliana vibaya wee alafu ukalaumu uliyekubaliana naye,
Kuna watu wameibuka na kusema kwamba kama ni kuibua vipaji mbona hawajawaibua mama zao na dada zao wanasubiri vipaji vilivyoibuka tiyari ili wavinyonye? nikashangaa nami nauliza kama kweli wewe ulikuwa ni kipaji ambacho kimeibuka tiyari kwanini hukwenda radio nyingine mpaka clouds?
Kwaheri Ruge umebeba mengi mpaka lawama usizostahili hata za wazembe, hata za waliochezea wakati hata za waliokuwa wanataka vya free, lakin Tambua kwamba hakuna freee,