TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Ruge Mutahaba ataendelea kutajwa kila kipindi siku zote Kama yeye mwenyewe alivyoacha ujumbe kuwa akifa watu wasilie bali washerekee mafanikio ya kuenzi na kuendeleza yote aliyochangia.
Overdo
 
Naota kivipi....ile ni mali yao ni chombo chao cha biashara wanaweza kuamua kufanya chochote kuhusiana na msiba wa Ruge
 
Katekista ni muumini wa kawaida kabisa kwa maneno mengine ni kwamba kazikwa na muumini mwenzake
naomba nijibu haya!
Ibada huwa kwaajili ya marehemu au waliopo pale kwenye mazishi?

2:Kuzikwa na padre au katekista ina athari yoyote kwa marehemu katika safari yake ya milele?
 
Chritiana Mutahaba ambaye ni mama mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba amesema familia yake itafarijika iwapo mazuri aliyoanzisha mwanaye yataendelezwa kwa kuwa inaonekana aligusa maisha ya wengi.
Akizungumza leo Machi 6, 2019 katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, amesema amesikia mengi kuhusu mwanaye ambayo hakuyafahamu lakini itakuwa faraja yake yakiendelezwa.
“Mpaka sasa najiuliza huyu Ruge ni nani, amewafanya nini Watanzania, mbona amepata heshima kubwa, mbona mdogo sana lakini amezikwa kwa heshima hivi. Lakini nitafutahi kuona ndoto zake zinaelezwa,” amesema.
Amesema ukiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwanaye amekuwa Mtanzania wa pili kupata heshima kubwa katika mazishi yake.
“Wakati Mwalimu Nyerere anafariki hatukuwepo nchini lakini tulifuatilia mazishi yake yalikuwa makubwa sana, tangu hapo sijaona tena, kwa kweli amepewa heshima kubwa ninashukuru,” amesema katika mahojiano yaliyofanyika katika Kijiji cha Kiziru, Bukoba.
Pia, amemshukuru Rais John Magufuli na viongozi wengine walioshiriki kufanikisha maziko ya mwanaye kwa hali na mali.
“Namshukuru Mungu aliyetuwezesha kuleta mwili wa Ruge mpaka Bukoba, nawashukuru viongozi wa Serikali kuanzia Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na wote waliotusaidia. Pia, nawashukuru Watanzania kwa maombi yao.”
Akinukuu vitabu vya dini amesema mkono wa mwanadamu ni mfupi kwamba kuna mahali unaishia na ndivyo ilivyokuwa kwa Watanzania walioshiriki kwa hali na mali kuokoa uhai wa Ruge wakati akiugua.
 
Mimi naomba kuuliza...
hivi ni sawa kwa mtu kupewa sakramenti zote kwa siku moja??
Nilishuhudia harusi flani mwaka jana ..bwana na bibi harusi wamebatizwa..kipaimara...na sacrament ya ndoa siku moja..tena kati kati ya ndoa.
Hii ilifanyika kanisa kuu katoliki Znz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni bosi wao wanaweza wakaamua kumtangaza ama kufanya maombolezo kila siku and nobody no institution can do anything about it...you get my drift
Media ni kwaajili ya umma , inabidi waonyeshe kwa kiwango , na maisha yaendelee, kazikwa imetosha , lakini kama wanamlilia nyumbani kwao haina shida hata walie miaka kumi . Hiyo ni dalili tosha kuwa Ruge kaondoka na clouds , na ya kwamba hamna kiongozi hapo., unapofanya kitu in public weledi ni muhimu , huwezi fanya utakavyo , hapo ndipo mnatuonyesha mapungufu yaliopo.kwenye hiyo media.
 
naomba nijibu haya!
Ibada huwa kwaajili ya marehemu au waliopo pale kwenye mazishi?

2:Kuzikwa na padre au katekista ina athari yoyote kwa marehemu katika safari yake ya milele?
Mimi nimejibu tu kuhusu katekista, ila sio mkatoliki
 
Back
Top Bottom