Rukwa: Amuua mjamzito na watoto wawili kwa deni la Tsh. 100,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata Philipo Vincent (22) kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata mapanga mjamzito na watoto wake wawili.

Jeshi hilo limesema wakati wa kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuwa anamdai mjamzito huyo gunia mbili za mahindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya, alisema kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kuwa alijaribu kujinyonga ndipo walimkamata, na walipomuhoji alisema kuwa anataka kujiua kwa kuwa hana amani baada ya kufanya mauaji hayo.

Mallya alisema walipomuhoji zaidi, alikiri kufanya mauaji hayo kwa kuwa alikuwa amemkopesha gunia mbili za mahindi na alipomdai alionekana kufanya ukaidi wa kumlipa.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipokuwa akienda kwa mwanamke huyo kudai fedha Sh. 100,000 alimjibu kuwa asimdai kwa nguvu kwa kuwa hakumlazimisha amkopeshe, kauli iliyomuudhi mtuhumiwa na kuamua kufanya mauaji hayo.

"Mtuhumiwa huyo alinunua panga jipya na kulinoa vizuri, na siku ya Januari 14 usiku alikwenda nyumbani kwa marehemu na kisha kufanya mauaji hayo na kutokomea," alisema Mallya.

Alisema polisi walipomuhoji sababu za kuwaua na watoto, alijibu kuwa aliamua kuwachinja kwa kuwa watoto hao walimuona wakati anamuua mama yao na pia wanamfahamu kwa kuwa mekuwa akienda katika nyumba hiyo mara kwa mara kudai fedha, hivyo wangemtaja.

Mapema wiki hii, jeshi hilo lilisema tukio hilo linadhaniwa kutokea usiku wakati mama huyo na watoto wake wakiwa ndani ya nyumba yao, kisha watu waliotekeleza mauaji hayo kuingia ndani.

NIPASHE

Mallya alisema mume wa mwanamke huyo ambaye yuko Dar es Salaam alianza kumtafuta mkewe kwa kumpigia simu, lakini ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Alisema alipopiga kwa muda mrefu simu hiyo ilizima, hali inayoonyesha kuwa ilizima kwa kuishiwa chaji na kila alipojitahidi kupiga haikupatikana.

Baada ya hapo alimpigia rafiki yake, Paul Leonard, na kumwagiza aende akaione familia yake na alifika nyumbani hapo saa 2:30 usiku na alishangaa kukuta mlango umefungwa nje kwa kufuli, hivyo aliamua kuwaita viongozi wa kijiji na walipofika na kubomoa mlango na kuingia ndani walikuta mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane akiwa amechinjwa pamoja na watoto wake Milliam (8) na William (4).
 
Kila siku mauaji, mnaendekeza sana habari za mauaji, kwani hamna habari nyingine? au mnachafua tuu serikali ya awam ya 6 kisa haiteki watu kama ya mwenda zake.
 
Hii ndiyo Afrika na wa2 wake, kuna maji2 haya imani hata wakina chui na simba wanaafazali. Unyama huu uwezi kukuta kwa white
 
JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata Philipo Vincent (22) kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata mapanga mjamzito na watoto wake wawili.

Jeshi hilo limesema wakati wa kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuwa anamdai mjamzito huyo gunia mbili za mahindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya, alisema kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kuwa alijaribu kujinyonga ndipo walimkamata, na walipomuhoji alisema kuwa anataka kujiua kwa kuwa hana amani baada ya kufanya mauaji hayo.

Mallya alisema walipomuhoji zaidi, alikiri kufanya mauaji hayo kwa kuwa alikuwa amemkopesha gunia mbili za mahindi na alipomdai alionekana kufanya ukaidi wa kumlipa.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipokuwa akienda kwa mwanamke huyo kudai fedha Sh. 100,000 alimjibu kuwa asimdai kwa nguvu kwa kuwa hakumlazimisha amkopeshe, kauli iliyomuudhi mtuhumiwa na kuamua kufanya mauaji hayo.

"Mtuhumiwa huyo alinunua panga jipya na kulinoa vizuri, na siku ya Januari 14 usiku alikwenda nyumbani kwa marehemu na kisha kufanya mauaji hayo na kutokomea," alisema Mallya.

Alisema polisi walipomuhoji sababu za kuwaua na watoto, alijibu kuwa aliamua kuwachinja kwa kuwa watoto hao walimuona wakati anamuua mama yao na pia wanamfahamu kwa kuwa mekuwa akienda katika nyumba hiyo mara kwa mara kudai fedha, hivyo wangemtaja.

Mapema wiki hii, jeshi hilo lilisema tukio hilo linadhaniwa kutokea usiku wakati mama huyo na watoto wake wakiwa ndani ya nyumba yao, kisha watu waliotekeleza mauaji hayo kuingia ndani.

NIPASHE

Mallya alisema mume wa mwanamke huyo ambaye yuko Dar es Salaam alianza kumtafuta mkewe kwa kumpigia simu, lakini ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Alisema alipopiga kwa muda mrefu simu hiyo ilizima, hali inayoonyesha kuwa ilizima kwa kuishiwa chaji na kila alipojitahidi kupiga haikupatikana.

Baada ya hapo alimpigia rafiki yake, Paul Leonard, na kumwagiza aende akaione familia yake na alifika nyumbani hapo saa 2:30 usiku na alishangaa kukuta mlango umefungwa nje kwa kufuli, hivyo aliamua kuwaita viongozi wa kijiji na walipofika na kubomoa mlango na kuingia ndani walikuta mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane akiwa amechinjwa pamoja na watoto wake Milliam (8) na William (4).
Shetani ametamalaki,tumrudie Mungu hali sio nzuri,...
 
Back
Top Bottom