Rukwa: Amuua mjamzito na watoto wawili kwa deni la Tsh. 100,000

Rukwa: Amuua mjamzito na watoto wawili kwa deni la Tsh. 100,000

Ni noma watu wamevurugwa sana tunapaswa kujitahidi kuishi clean.

Usidhulumu ,usitapeli,usiibe,usisaliti,usionee watu,usijivune kupita kiasi,usilingishie Mali,

Majanga yakiamua kukukuta yanakukuta tu ila angalau tuepuke vitu tajwa hapo juu tunaweza kusogeza siku!!

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Mimi naweza kusema Asalam aleikum au Bwana Yesu asifiwe na nikawa Shetani tuuuuu............
Hata shetani anatambua nguvu za Mungu. Mungu wetu ni wa upendo habagui, hata ukiwa umefanya baya ukamtaja basi atakusikiliza. Na ndipo amani ukuijia. Ni kwa nini dini zote umtaja yeye. Tafakari Maswala ya Mungu hayana ushabiki. Usilete siasa katika ukuu wa Mungu.
 
Hizi ni laana zinazolikumba Taifa baada ya kumuua mtu asiye na hatia.
Na bado tusibotubu na kusali ni mengi yanakuja, damu ya mwenye haki kamwe haiendi bure.
Na mbaya zaidi sijawah kumsikia Hangaya a.k.a Simba jike akimtaja Mungu hata kwa bahati mbaya.
Damu ya magufuli inamlilia hangaya.
 
Mimi naweza kusema Asalam aleikum au Bwana Yesu asifiwe na nikawa Shetani tuuuuu............
Hili ni swala la imani zaidi, kwa kusema hivyo shetani unuweka pending in heal kuliko kwenda oyaoya kama mama yako .
 
Hata shetani anatambua nguvu za Mungu. Mungu wetu ni wa upendo habagui, hata ukiwa umefanya baya ukamtaja basi atakusikiliza. Na ndipo amani ukuijia. Ni kwa nini dini zote umtaja yeye. Tafakari Maswala ya Mungu hayana ushabiki. Usilete siasa katika ukuu wa Mungu.
kuna unafiki wakulitaka bure jina Bwana Mungu..hilo kila mtu anafahamu, si SIASA.
 
JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata Philipo Vincent (22) kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata mapanga mjamzito na watoto wake wawili.

Jeshi hilo limesema wakati wa kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuwa anamdai mjamzito huyo gunia mbili za mahindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya, alisema kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kuwa alijaribu kujinyonga ndipo walimkamata, na walipomuhoji alisema kuwa anataka kujiua kwa kuwa hana amani baada ya kufanya mauaji hayo.

Mallya alisema walipomuhoji zaidi, alikiri kufanya mauaji hayo kwa kuwa alikuwa amemkopesha gunia mbili za mahindi na alipomdai alionekana kufanya ukaidi wa kumlipa.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipokuwa akienda kwa mwanamke huyo kudai fedha Sh. 100,000 alimjibu kuwa asimdai kwa nguvu kwa kuwa hakumlazimisha amkopeshe, kauli iliyomuudhi mtuhumiwa na kuamua kufanya mauaji hayo.

"Mtuhumiwa huyo alinunua panga jipya na kulinoa vizuri, na siku ya Januari 14 usiku alikwenda nyumbani kwa marehemu na kisha kufanya mauaji hayo na kutokomea," alisema Mallya.

Alisema polisi walipomuhoji sababu za kuwaua na watoto, alijibu kuwa aliamua kuwachinja kwa kuwa watoto hao walimuona wakati anamuua mama yao na pia wanamfahamu kwa kuwa mekuwa akienda katika nyumba hiyo mara kwa mara kudai fedha, hivyo wangemtaja.

Mapema wiki hii, jeshi hilo lilisema tukio hilo linadhaniwa kutokea usiku wakati mama huyo na watoto wake wakiwa ndani ya nyumba yao, kisha watu waliotekeleza mauaji hayo kuingia ndani.

NIPASHE

Mallya alisema mume wa mwanamke huyo ambaye yuko Dar es Salaam alianza kumtafuta mkewe kwa kumpigia simu, lakini ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Alisema alipopiga kwa muda mrefu simu hiyo ilizima, hali inayoonyesha kuwa ilizima kwa kuishiwa chaji na kila alipojitahidi kupiga haikupatikana.

Baada ya hapo alimpigia rafiki yake, Paul Leonard, na kumwagiza aende akaione familia yake na alifika nyumbani hapo saa 2:30 usiku na alishangaa kukuta mlango umefungwa nje kwa kufuli, hivyo aliamua kuwaita viongozi wa kijiji na walipofika na kubomoa mlango na kuingia ndani walikuta mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane akiwa amechinjwa pamoja na watoto wake Milliam (8) na William (4).
walikuta mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane akiwa amechinjwa pamoja na watoto wake Milliam (8) na William (4).[emoji848][emoji848][emoji31][emoji31][emoji2827][emoji2827]
 
Hizi ni laana zinazolikumba Taifa baada ya kumuua mtu asiye na hatia.
Na bado tusibotubu na kusali ni mengi yanakuja, damu ya mwenye haki kamwe haiendi bure.
Na mbaya zaidi sijawah kumsikia Hangaya a.k.a Simba jike akimtaja Mungu hata kwa bahati mbaya.
Bora kutomtaja Mungu kabisa hasa unapojua umebeba kichwani dhambi ya kubambikia watu kesi kuliko kumtaja kinafiki huku unajua umebeba dhambi ya mauaji na kujeruhi watu kwa risasi zisizo na idadi.
 
Hata angekuja humu jf angesema anamdai mjamzito hiyo pesa tungemchangia na ingefika angepata pesa yake.. haya angalia anaenda jera bure kwa ajili ya pesa mbuzi laki moja.. JINGA TU
Mtu mwenyewe ana miaka 22 lakini akili za kuzimu.
 
Hata shetani anatambua nguvu za Mungu. Mungu wetu ni wa upendo habagui, hata ukiwa umefanya baya ukamtaja basi atakusikiliza. Na ndipo amani ukuijia. Ni kwa nini dini zote umtaja yeye. Tafakari Maswala ya Mungu hayana ushabiki. Usilete siasa katika ukuu wa Mungu.
Kuna kutaja jina la Mungu kuficha Uovu yani Mbwa mwitu kuvaa ngozi ya Kondoo na wengi wameshoneana hapa kama si kujazana hapa.
 
Bora kutomtaja Mungu kabisa hasa unapojua umebeba kichwani dhambi ya kubambikia watu kesi kuliko kumtaja kinafiki huku unajua umebeba dhambi ya mauaji na kujeruhi watu kwa risasi zisizo na idadi.
NAKAZIA tena ukitaka kujua mtu mwenye kujutia utamfahamu namna anavyoongea mara nyingi kupayuka payuka si mpango hata BIBLIA ILIKATAA Kupayuka payuka.
1)kuna watu hawawezi unafiki,na hawatafuti huruma ya wananchi
2)Kuna watu wamebobea ni wakufunzi wa Unafiki katika kutafuta huruma za wananchi
awamu ya sita na ya tano kila mmoja hapo ana kundi lake.
 
Mtu unamdai alafu anakujibu kwani nilikutuma unikopeshe? Wakati wa kuja kukopa alikuja ana shida na analia
 
Hakuna namna mtu ananoa panga Na kuua Mama innocent children Pasipo acceleration Fulani ya shetani
Alipomaliza akataka kujinyonga kama yuda baada ya roho ya kuua kumwacha, akarealize alichofanya akataka kujiua
 
Dah huyu pepo wa mauaji atuache kwa kweli
 
Back
Top Bottom