....Hatuwezi kuwa na taifa bovu lisilokuwa na staha kwa excuses ndogo kama vijana kukosa ajira eti bado wachanga kwenye industry basi waachwe tu wavuruge maadili...
Sijasema awajakosea au hawastahili sanctions ila miezi sita ni mingi sana.
Fines tu zingetosha kuliko kuwafungia kila kosa.
Ni hivi Wasafi TV ni kituo kipya serikali inayo encourage vijana kujiajiri anapotokea mmoja anatoa ajira kwa wenzake lazima impe heshima anazostahili, pili ni interest ya serikali kuona tasnia ya habari inakuwa na kuna variety of shows zinazogusa watu wenye interest mbali mbali zaidi ya serious news na siasa tu kama ilivyo zoeleka.
Wasafi ni wachanga common sense ni kuwapa margin of error katika operation zao. Kwa sababu lazima watakosea tu hapa na pale.
Producer mwenye experience na aliebobea anapoona kuna images tata palepale anachange camera na kuonyesha sehemu nyingine.
Hawa vijana ndio kwanza wanaingia hiyo industry serikali lazima ielewe kutakuwa na mistakes za hapa na pale hawa sio Azam, TBC au ITV zinazoendeshwa na watu nguli.
Kwa ivyo common sense has to prevail sometimes they need nurturing at this stage sio kuwapa adhabu kubwa, lazima wafundishwe vitu kama live shows zingine kuwe na delays za dakika mbili katika kupokea picha na kurusha hewani zinazoingia ili kujipa muda wa ku react haraka itasaidia pale ambapo kuna jambo wasilo tarajia linapotojea, litasaidia kujua jinsi ya kubadili camera on time, etc with other live production challenges.
Bado ni amateurs halafu wengi ni vijana watakosea tu kipindi hiki cha mwanzo wa safari yao wanahitaji guidance sio kuwaumiza kila wanapokosea.