RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

Ni jambo la kupongezwa kwa mamlaka kwa hatua hiyo maana upuuzi wa namna hiyo ndiyo unaharibu maadili ya jamii, watoto na vijana huiga kwa hao wasanii ambao wameshachanganyikiwa. Hongereni TCRA sasa baada ya hiyo TV kushughulikiwa na TCRA, Basata nao wadeal na huyo muonyesha tupu kwa kumfungia naye ili huo utupu awaonyeshe nduguze
Kabisa....ndomana sahv watoto wa kiume wakuwa legelege...nywele kupakaa dawa,mdomoni lipstick,wanavaa nguo za kubana
Upuz mtupu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha kurusha matangazo kwa miezi sita kuanzia leo kutokana kwa kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui ya utupu.

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akicheza ‘utupu’ kinyume na Kanuni katika tamasha la “Tumewasha Live Concert” lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

Aidha Wasafi Tv wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.

Pia soma > Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?
Nasikia kwanza hawakuwa na kibali cha kuperfom hawa vijana
 
Wataenda popote, kwahiyo wasionywe kisa watakuwa hawana ajira? Hakna hiyo.
Sheria ni msumeno, hukata huku na huku. Safi kwa TCRA kufanya kazi yao kwa weledi
Huo msumeno nani kauunda?? Inaonekana umeundwa na watu wasiokuwa na akili.

Kuna wakati Floyd Mayweather alipatikana na hatia ya kumpiga girl friend wake (Battery charges) na akahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja. Kabla hajafanya tukio hilo la shambulio tayari alikuwa na commitment ya pambano na pambano hilo lilikuwa bado kama wiki moja lifanyike, kwa kuona umuhimu wa pambano katika uchumi wa jiji la Lasvegas yule Jaji akaahirisha kifungo hadi atapomaliza lile pambano na ikawa hivyo, hiyo ndiyo akili na sheria zenye akili zinatakiwa ziwe hivyo, unatakiwa kuungalia maslahi mapana ya umma kukiko kuangalia maslahi finyu.

Inatakiwa hao waliorusha huo uchafu katika Tv ndio wachukuliwe hatua na sio Kituo kizima cha TV chenye maslahi ya jamii kubwa.
 
Habari ni kwa mujibu wa tweet ya Swahili Times:

HIVI PUNDE: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kituo cha televisheni, Wasafi TV, kwa muda wa miezi sita. TCRA imesema kituo hicho kimekiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui yaliyomuonesha mwanamuziki Gigy Money akionesha utupu wake akiwa jukwaani.
 
Huo msumeno nani kauunda?? Inaonekana umeundwa na watu wasiokuwa na akili.

Kuna wakati Floyd Mayweather alipatikana na hatia ya kumpiga girl friend wake (Battery charges) na akahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja. Kabla hajafanya tukio hilo la shambulio tayari alikuwa na commitment ya pambano na pambano hilo lilikuwa bado kama wiki moja lifanyike, kwa kuona umuhimu wa pambano katika uchumi wa jiji la Lasvegas yule Jaji akaahirisha kifungo hadi atapomaliza lile pambano na ikawa hivyo, hiyo ndiyo akili na sheria zenye akili zinatakiwa ziwe hivyo, unatakiwa kuungalia maslahi mapana ya umma kukiko kuangalia maslahi finyu.

Inatakiwa hao waliorusha huo uchafu katika Tv ndio wachukuliwe hatua na sio Kituo kizima cha TV chenye maslahi ya jamii kubwa.
Points zako nazielewa hapa[emoji1666][emoji123]. Sjiui tuna serikal ya Aina gan jaman
 
TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha kurusha matangazo kwa miezi sita kuanzia leo kutokana kwa kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui ya utupu...
BASATA wangekuwa wanatekeleza wajibu wao nyimbo nyingi za bongo Flava zingefungiwa. Vijana wamekosa ubunifu wa kisanii wamegeukia kuimba matusi ya nguoni. Karibu nyimbo zote ni matusi tu. Huwezi kusikiliza au kuangalia nyimbo hizi na mtu unayemheshimu. Wameachwa sababu no wapiga debe wa chama ila madhara yake ni makubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla
 
Wakiumia ndiyo watakuwa makini kurusha maudhui yanayokubalika sawa na miongozo ya TCRA na utamaduni wa kitanzania. Huwezi kuacha kuadhibu kisa kuna watu wataumia, maana hata wafungwa wapo waliokuwa wanategemewa na familia zao ila kwa kuwa walitenda makosa hakuna namna
Kwa sababu sio wewe. You're not affected directly. Imagine ni wewe
 
Back
Top Bottom