Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

Sidhani kama hiki kitu ni kweli. Kuna watu walizusha kwamba kwenye milima ya Usambara hao wajerumani walificha mali zao na waliwaua wale waswahili waliobeba zile mali ili kuficha siri ya uwepo wa hizo mali. Katika miaka ya themanini likazuka kundi la watu na kuna mtu alifadhili ufukuaji wa hizo mali.
Katika hilo kundi kuna Bwana mmoja alidai babu yake alikuwa ni mmoja wa wapagazi wa Wajerumani na alifanikiwa kuwachoropoka Wajerumani na kutokomea baada ya kufukia hizo amali. Eti pia babu yake aliwahi kumueleza kwamba hapo kwenye hilo eneo ndipo zilipofukiwa hizo mali na kuna alama maalum za kijerumani ambazo zinapatikana kwenye hayo mahandaki zinazotambulisha hayo maeneo. Na kwamba alama hizo ziliwekwa wakati wakifukia na pia huonyesha uelekeo wa sehemu zilikofichwa hizo mali.
Walifukua kipande cha mlima na baada ya tajiri kuona huo ni uongo alitokomea bila kuwaaga. Waliendelea kufukua na kukopa chakula, ila kila siku waliendelea kupungua (walitoroka kimyakimya). Hakuna walichopata zaidi ya kuambulia madeni!
 
Jamani hiii nikweli waliacha mali Tanzania..kuna maeneo mengi ukitembea milimani utakuta vyuma flani vya mviringo vimejazwa udongo wa cement kali.juu kuna maandishi yanaonesha vipimo flani vya umbali kutoka usawa wa alama hiyo ilipo.ninae changia maada hii ninauhakika. Ila cjawahi kuona wamefika na kuchukua mali ila hali hii ipo kabisa.. Nivigum kuamini kwasababu tumechelewa kupata elim lkn habari hii ni yakweli kabisa
 
hata hapa morogoro zipo mhizo stry huku juu miliman na mm hilo jengo nimewah kuingia na kuna alama fulan inasemekana waliojaribu walikufa kifo kibaya sana
 
N
Habari wanabodi!!

Kuna tetesi ambazo zilishavuma sana kwa kipindi kirefu sana hapa nchini huku baadhi ya wenzetu wakijitokeza sehemu mbalimbali kuthibitisha tetesi hizo.

Inadaiwa kabla ya wajerumani kukimbia Tanganyika wakati wa Vita ya kwanza ya Dunia baina yao na waingereza na kujikuta wakishindwa vibaya katika vita hiyo walikuwa wamemiliki hazina na Mali nyingi ndani ya eneo lao lililojulikana Germany East Africa Terrirory.

Haikuwa rahisi baada ya kushindwa vita hivi kuondoka na mali zao zote kwenda nazo Ujerumani. Hivyo basi, mali na hazina nyingi inasemekana zilifinywa maeneo mbalimbali hapa nchini. Kuna ambazo zilifichwa chini ya milima, kwenye mahandaki na kwingineko kama habari zilizotufikia zilivyokuwa zikienea.

Kuna watu ambao walijaribu Mara kwa Mara kuzifikia hazina hizi lakini hakuna aliyewahi kujitokeza na kutabainisha kuwa alifanikiwa kupata hata kipande kidogo cha hazina hizo. Kuna wengi ambao pia walikuja na madai kuwa kwenye maeneo hayo kuna ushirikina mkubwa ambao wajerumani waliufanya hivyo ni vigumu kuweza kufikia hazina hzo bila idhini yao.

Nakumbuka kipindi cha nyuma kuna jamaa mmoja alitoa ushuhuda huko sehemu za tabora kuwa wajerumani walifika na kwenda kuchukua baadhi ya Mali walizoziacha na walifanikiwa na haikuonekana kama ilikuwa ni kazi kubwa kwa upande wao. lakini wananchi wa maeneo hayo wamejaribu kuzifikia hizo hazina kwa miaka bila mafanikio.

Hii inanipeleka niwaze kuhusiana na nchi ya Misri. Kupitia filamu mbalimbali tumekuwa tukiaminishwa nchi ya misri hususani kwenye zile pyramid zake kuna hazina kubwa ikiwemo dhahabu ambayo huwezi kukisia utajiri wake.

Swali ni je, habari kuhusu hizi Mali za wajerumani zilizofichwa ni za kweli? Zimefichwa maeneo gani? Kwanini wazawa hatuwezi kuzifikia hizi Mali? Je, hii nadharia ya ushirikina kwenye maeneo haya ni ya kweli? Ni kweli pia kuwa wajerumani huwa wanafika kuchukua hizi Mali zao walizoficha.

Lets contribute na tujifunze
Nimeshawahi sikia stori ya aina hii sikuamini. ila moja ya sehemu inayosemwa ni Mwambao wa Mto Ruvuma wilaya ya Namtumbo Maeneo yanaitwa kama sikosei Milepa, kuna hazina kubwa na wajerumani na inasemekana ukienda bila wao hupati kitu. na maeneo yenye hazina hizo nasikia wameyaweka alama ya vimiti fulani hivi inasemekana havikui coz vilipakwa dawa fulani. (Angalizo; Inasemekana sijathibitisha)
 
Nakuja na hii kitu na ntawatafuta wanaojua hizo sehemu tukasake mali hizo
105cfbe0e5661a0e7e7396fb6b620a37.jpg
Ndugu tunazo tena hiyo cha mtto hiyo haifiki kwa sensa yake kama hii na hii ni chamtto ipo
FB_IMG_14939795041837878.jpeg
 
Mnazo wapi hizo?
Hebu nielekeze duka hilo na bei yake maana hiyo niliyoweka ni 3m
Hiyo unachoka mkono na inachosha kuivaa kiunoni,ssa zipo kama ipad vile ngoja iingie alafu nikutupie uione.hiyo nilinunua mwaka 2009 ilikuwa 7mill kwa hela yetu ssa cjui kwani kuna matoleo mengi yamepita hapo katikati ndo nimeona niipiganie hii yenye mfumo kama ipad unaweka tu kwenye bag,unazunguka pori to pori
 
Hiyo unachoka mkono na inachosha kuivaa kiunoni,ssa zipo kama ipad vile ngoja iingie alafu nikutupie uione.hiyo nilinunua mwaka 2009 ilikuwa 7mill kwa hela yetu ssa cjui kwani kuna matoleo mengi yamepita hapo katikati ndo nimeona niipiganie hii yenye mfumo kama ipad unaweka tu kwenye bag,unazunguka pori to pori
Inaonekana umeokota za kutosha (gold) kama hizo mashine zinachambua
Hongera sana
Naona utajiri unao
Najua kuna companies zina toa hivyo vifaa na kazi ni kuokota vito vya thamani beach
 
Moja kwa moja utawaza kuhusu rupia(rupee ya mjerumani) na pesa nyingine za kale na yale yanayosemwa kuzihusu hasa kwenye habari nzima za kichawi
Watu wamezinguka na kuzinguliwa hasa watu wametapeliwa na wengine kufa wakitafuta hivi vitu vinavyotajwa kuwa na thamani kubwa

Ukweli huu hapa na si pesa tu bali na vitu vingine vya kale
1. Aina ya malighafi iliyotumika
Wakati huo vilitengenezwa vitu imara sana kutokana na upatikanaji wa malighafi ya kutosha ...vitu kama vyombo vya bati na chuma urembo kama bangili mikufu pete nk leo hii ukivipata na kuviyeyusha kila kimoja unaweza kutengeneza kumi kupitia hicho kimoja

2. Uhifadhi
Wajerumani kwa hapa kwetu walikuta malighafi vito na madini ya kutosha sana! Kutokana na uhifadhi hafifu wakati huo vingi ya hivi vitu viliwekwa tu majumbani mwao wakiviandaa kuvidafirisha kwao
Vita ya pili ya 1939-45 iliwachanganya mno na walipoelekea kushindwa waliamua kuficha mali yote kwenye mashimo makubwa mashambani misituni kwenye mahandaki na milimani kusikofikika kwa urahisi kisha wakawaua watu karibia wote walioshiriki na wanaojua yale maficho wakasepa
Huku kote mali hizo zilihifadhiwa kwenye vyumba imara vilivyojengwa kwa zege gumu hasa ili iwe ngumu kuchimbua ama kuvunja na kama ni mapangoni yalikuwa mapango ya mbali hasa milimani na misituni

3. Dhana ya majoka na viumbe wa ajabu
Huko kwenye hayo maficho kuna baadhi ya watu walisalimika hivyo wakasimulia vizazi vilivyofuata
Kizazi cha kusaka utajiri wa haraka kikaona fursa na kuamua kuchangamkia dili. ..Wajerumani hawakuweka ulinzi wowote wa majoka! Hao ni viumbe tu walijitwalia makazi huko ambako ndio maisha yao yaliko
Watu walioenda bila tahadhari waliumwa na hayo madubwana na kupoteza maisha! Waliosalimika walitimua mbio na kuunda stories za kufikirika

4. Dhana ya uchawi na majini
Kwa wale waliosaka kwenye mahandaki na mashimo marefu yenye vyumba vilivyojengwa kwa zege , baada ya kufanikiwa kuvunja hayo mazege na kutaka kuingia ndani nao walikutana na mauzauza ya kila aina
Unajua ni kwa nini? Sehemu yoyote yenye mfumo wa nyumba ama chumba isiyokaliwa na binadamu roho zinazotangatanga na mapepo hufanya makazi yao kumbuka ile mada ya kutakasa makazi! Hivyo ukiingia huko lazima ukutane na vitu vya ajabu...Mjerumani hahusiki kabisa!

5. Uamuzi wa kufanya kafara ama tambiko kabla ya kuchimba ama kuingia pangoni
Wengi walitafuta waganga wa kienyeji kwenye hili na hawakufanikiwa. ..waliofanikiwa walifanikiwa kwa ujanja tuu....ukienda kwenye pango misituni ukachinja mnyama ukapiga manyanga automatically mkiondoka ile nyama italiwa na kuna wakati manyanga huleta kelele na kufukuza mnyama yoyote aliyeko pangoni...ndio maana baada ya kafara hamuingii siku hiyo hiyo bali kesho yake nk
Wale wa kwenye mashimo NA mahandaki ni ibada tu ya kuziomba roho ziondoke ama kuzifukuza kwa kutumia mitishamba na harufu wasizozipenda....mkikutana na roho korofi mtachezea kichapo mpaka muache kila kitu na kutimua mbio kali sana

6. Ukweli hasa ni UPI?
Baada ya vita ya pili kukoma na baadae Uhuru wajerumani walishindwa kurudi kwa ubabe hivyo wakatumia njia za kijanja kurudi
Unajua waliondoka na ramani zote kule mali zilikofichwa hivyo walirudi kuzichukua kwa njia ya kununua yale maeneo na kuyaendeleza kwa kujenga shule vyuo hospital nk ama miradi ya barabara ufugaji na kilimo
Kwa njia hii walichukua vyao kiulaini mno

7. Thamani na umaarufu wake ni UPI!?
Vitu vya kale kwa wenzetu vina thamani kubwa sana....wenzetu wana utaratibu wa kuweka vituo vya antiques na kuchaji watalii pesa ndefu kuviangalia . kila kimoja kinakuwa kimeandikiwa historia yake. Kwa hiyo wakija huku kuvitafuta wengi huenda kuviuza kwenye hayo maduka kwa bei kali mno

8. Nguvu ya utajiri
Biashara imevamiwa , vitu vya kale haviwezi kukupa utajiri wa miujiza ..havina huo uwezo bali kuna baadhi kutokana na malighafi iliyotumika kuvitengeneza vina mvuto kwenye ulimwengu wa giza kama mabangili ya shaba

9. Usumbufu
Kuna watu wanawachezea wenzao shere na kuwasumbua bila sababu.. Miaka hiyo pesa ilitengenezwa kwa mpango maalum(nadhani hata sasa) na zilitengenezwa kwa miaka... Kuna miaka pesa hazikutengenezwa. Sasa mtu anakupa dili na kukuahidi kukupa pesa ndefu ukimletea rupee ya mwaka fulaniView attachment 526110

10. Hitimisho
Kuna baadhi ya sehemu kulikofichwa hizo mali wafichaji walinuizia ama kufanya mambo ya giza ili atakayejaribu kuchukua ama apate madhara au asizione kabisa...lakini kwa sehemu kubwa ni habari zilizotiwa chumvi nyingi


JUMAPILI NJEMA
Jr[emoji779] [emoji781]
Aisee Mshana uko vizuri kwenye mambo haya,mi mwenyewe nilikuwa napata masimulizi sasa leo umenipa ufahamu
 
Back
Top Bottom