Ukichukua rushwa kubwa- watoto wakakosa elimu, wagonjwa wakakosa huduma za afya wakafa, ujenzi wa barabara ukafanyika below standard, hiyo haina madhara kiuchumi?
1, Tuchukue mfano mmoja wa rushwa kwenye miundombinu ya barabara- barabara mbovu zinasababisha:
- Pembejeo za kilimo sizifike kwa muda na zifike kwa gharama ya juu- hii husababisha gharama za uzalishaji kuongezeka au pia uzalishaji kushuka
- Usafirishaji wa mazao toka vijijini kwenda kwenye masoko huwa mgumu- hivyo bidhaa kupanda bei, kuongeza inflation n.k
- Kilimo kinakuwa hakivutii tena kama mwajiri wa vijana
- Uchumi wa nchi unadidimia
Mifano kama hii inaweza kutolewa kwa sekta nyinginezo muhimu kama elimu:
- Rushwa ya ngono kwenye elimu
- Rushwa ya mitihani
Yote hayani majanga makubwa kwa taifa.
Recipient wengi wa fedha za rushwa wanajenga majengo yao na familia zao, wananunua magari ya gharama kwa ajili ya familia zao na vimada wao. Rushwa haiwezi kamwe kuendeleza nchi