Rushwa haina madhara yoyote ya maana kwa maendeleo ya nchi

Kuna mahali niliona anataja neno ufisadi na rushwa separately nikapata wasiwasi juu ya uelewa wake katika maswala ya rushwa
 
Ukichukua rushwa kubwa- watoto wakakosa elimu, wagonjwa wakakosa huduma za afya wakafa, ujenzi wa barabara ukafanyika below standard, hiyo haina madhara kiuchumi?
1, Tuchukue mfano mmoja wa rushwa kwenye miundombinu ya barabara- barabara mbovu zinasababisha:
  • Pembejeo za kilimo sizifike kwa muda na zifike kwa gharama ya juu- hii husababisha gharama za uzalishaji kuongezeka au pia uzalishaji kushuka
  • Usafirishaji wa mazao toka vijijini kwenda kwenye masoko huwa mgumu- hivyo bidhaa kupanda bei, kuongeza inflation n.k
  • Kilimo kinakuwa hakivutii tena kama mwajiri wa vijana
  • Uchumi wa nchi unadidimia
Mifano kama hii inaweza kutolewa kwa sekta nyinginezo muhimu kama elimu:
  • Rushwa ya ngono kwenye elimu
  • Rushwa ya mitihani
Yote hayani majanga makubwa kwa taifa.

Recipient wengi wa fedha za rushwa wanajenga majengo yao na familia zao, wananunua magari ya gharama kwa ajili ya familia zao na vimada wao. Rushwa haiwezi kamwe kuendeleza nchi
 
Kwani Waziri wa Fedha Mwigulu si alisema hatutakuja kufuatwa nyumbani kulipa deni, sasa hiyo hofu yako inatoka wapi hata ikiwa Trilioni 10!!! Mbona logic zetu zinagubikwa na uchama!
 
Pia watu wasiona sifa wanapata tenda mbalimbali kupitia rushwa hii inafanya miradi kufanywa Chini ya viwango.hapa umeshaathiri maendeleo ya nchi.
 
Kwani Waziri wa Fedha Mwigulu si alisema hatutakuja kufuatwa nyumbani kulipa deni, sasa hiyo hofu yako inatoka wapi hata ikiwa Trilioni 10!!! Mbona logic zetu zinagubikwa na uchama!
Tumia akili.hayo madeni yanalipwa Kwa kutumia Kodi ya watanzania.
 
Kwani Waziri wa Fedha Mwigulu si alisema hatutakuja kufuatwa nyumbani kulipa deni, sasa hiyo hofu yako inatoka wapi hata ikiwa Trilioni 10!!! Mbona logic zetu zinagubikwa na uchama!
Uelewa wenu unatia mashaka!Watu wafanye ufisadi,kwasababu ni pesa za serikali basi mnasema Haina madhara kwasababu mtu hatafuatwa nyumbani kudaiwa!Hizi ni akili timamu kweli?Pesa ambayo ilipaswa ikajenge Barabara,ikanunue madawa na wananchi tupate maji,eti ndio inakwenda kugharamia matumbo ya watu kujineemesha!
Hivi kweli unaweza kusema Kodi unayolipa watu wajinufaishe na haina tatizo kwasababu haikugusi Moja Kwa Moja?Huu ni Ujinga!
Basi tukafute hizo Sheria tulizoweka juu ya rushwa na ufisadi!
Na hiyo Takukuru ifutwe,goli liwe wazi kila mtu kujipimia anapoweza kula!
 
[ Hiyo ni shida nyingine. Mtu anaweza toa rushwa ili apate tenda sababu competition ni kubwa, lakini akatoa huduma nzuri. Mtu anaweza kuwa na sifa zote za kuajiriwa lakini akatoa rushwa ili aajiriwe.

Hiyo ya kutoa huduma kihuni hata ambaye hajatoa rushwa anaweza kufanya. Rushwa ina madhara, haitakiwi kushabikiwa, lakini haina madhara ya maana kwenye uchumi wa nchi. Shida kubwa ni pale mla rushwa au fisadi anapotorosha hiyo pesa
 
Hizo fedha zinazo toroshwa hadi zifanyiwe udhibiti wanazitoa wapi?
Unajua nini maana ya rushwa?
Kokote kule. Kisheria huwezi kutokap nchini na 10k usd bila kibali.
 
Nilimsikia M7 akiliongelea hilo, walipokuwa wanalalamika watumishi wa umma kuishi maisha nje ya uwezo wao, alisema kama wangekuwa wanapeleka na kufungua miradi nje tungeshugulika nao,lakini kwa kuwa wanatumia humu humu na ndugu zao hakuna shida
 
Siku ndugu yako atakapokosa huduma hospitali na kufariki, uje utupe update kwenye huu uzi.
Ndiyo matatizo ya kuamisha theories za uchumi kwenda kwenye practice katika mazingira yasiyo. Theory ni muhitasari wa tena kiduchu kabisa wa hali halisi. Mleta mada kabeba theory kama ilivyo na kuibwaga hapa. Wachumi achananeni na mambo yenu ya kubishana....Leteni suluhu zinazoeleweka na zina manufaa kwa jamii nzima.

Vinginevyo, useme unachokusudia katika awamu hii.
 
Ingefaa kama ungetupa kwanza maana ya neno "rushwa" kutokana na ufahamu wako, ndipo tuweze kuelewa undani wa hoja yako juu ya athari zake za kiuchumi na kijamii.
 
aki yake. Hicho ni kitu kibaya, lakini kilichopo ni hizo hela zilizoliwa wanaenda kutumia kujenga majumba, kufungua biashara, kujenga viwanda, mashamba nk, nk. Mwisho wa siku unakuta athari kwenye uchumi zipo, lakini siyo za maana.

So rushwa si kitu kizuri lakini haina athari zozote za maana kwenye uchumi wa nchi. Uliona utawala wa JK ulivyojaa rushwa, lakini uliona jinsi biashara na mambo mengine ya kichumi yalivyoshamiri?

Tulitakiwa kuweka nguvu kubwa sana kuzuia utoroshaji wa pesa kuliko kupambana na rushwa.
 
Since tunaongelea Uchumi na sio matatizo mengine ya Haki n.k. ngoja tuongelee Uchumi
How Corruption affects emerging economies
Inefficiently Allocated Resources
Uneven Distribution of Wealth
High Prices for Low Quality
Low Stimulus for Innovation
A Shadow Economy Exists
Low Foreign Investment and Trade
Poor Education and Healthcare
 
Takukuru ipo chini ya hawahawa watoroshaji pesa na madini , so itafutwenjia nyingine ya kuwabana Ila ya takukuru meno hayana makali.

Jambo lingine linalo changia umasikini 50% ni Waafrika Kuamini kwamba wazungu wanaweza kila Jambo kuliko sisi ,hivyo tenda za miradi mikubwa hupewa wazungu kwasababu ku tatu.

(1) Kwamba eti wanamitaji ya kuendesha miradi hivyo hawasumbui.
(2) Utaalamu wa wazungu ni waju kuliko waafrika hivyo ubora wamiradi huzingatiwa.
(3) Ubinafsi na ufisadi , Viongozi huchukua 10% kwa hao wazungu na wakati mwingine husaini mikataba hiyo hukohuko Ulaya, Uchina,na Marekani.

Viongozi na wananchi wa Afrika tuache ushamba wa kuthamini rangi za watu badala yake tujikubali na kuheshimu Kama waafrika.

Tuwatumie watu wetu wa ndani kujengamiundombinu hata kwa kuwawezesha mitaji ,ujuzi,na utaalamu inapo bidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…