Tunapiga vita rushwa hadi tumeiundia taasisi. Na wengine wanasema nchi za Africa haziendelei sababu ya rushwa. Hili suala limefanyiwa utafiti na limeonekana halina ukweli. Imeonekana kuwa mtu anapokula rushwa na kuwekeza kwenye uchumi huo huo kunakuwa hakuna madhara yoyote ya maana kwenye uchumi.
Tatizo kubwa kwenye uchumi wa Africa ni utoroshwaji wa fedha. Viongozi wengi wa Africa wamekuwa wakiiba pesa na kwenda kuwekeza huko Ulaya au kuzitunza mabenki ya nje. Hapo wanaenda kukuza uchumi wa nchi hizo na kudhoofisha huku. Hili jambo linaathari kubwa sana kwa uchumi kuliko rushwa.
Matajiri wakubwa nao wamekuwa wakihamisha fedha nyingi kwenda nje ya nchi. Mambi haya yanaathari kubwa kiuchumi kuliko rushwa.
Pengine sasa PCCB waongezewe nguvu kubwa ili waweze kupambana na utoroshaji wa pesa, huo ndio moja ya adui wakubwa wa maendeleo yetu.
Hiyo ndio grand corruption,kama pesa halali kwanini uzikimbize nje?na wewe ni mtumishi wa umma?rejea ishu ya Mzee wa vijisenti,walinunua jengo la ubalozi kwa kuweka Cha juu,nchi ikalipa zaidi,hicho Cha zaidi kikachukuliwa na watu binafsi,wakazificha nje ya nchi,hazipo Nchini,kuendeleza uchumi,hiyo Rushwa ina madhara makubwa sana kwa maisha ya wananchi,badala ya nchi kufanya miradi kwa pesa ndogo,bei za vitu,tender zinaongezwa maradufu,miradi inafanyiwa kwa gharama kubwa,harafu kwa ubora hafifu,nchi inabidi ilipe zaidi,Cha ziada kinaliwa,mradi badala ya kukaa miaka 20,,ndani ya miaka 5,mradi unachakaa,nchi inabidi itumie pesa Tena kuukarabati,badala hizo pesa kufanya maendeleo,zinatumika kufanya matengenezo kwenye mradi mpya,
Grand corruption,missapropriarition of public funds,land grabbing,theft of public money through tendering,
Zina madhara makubwa kwenye uchumi wa nchi,Soko la Karume limechomwa kufukuzwa wamachinga,Ili eneo apewe mwekezaji!!hiyo ni Rushwa,kama huoni madhara hapo kwa uchumi wa wafanyabiashara wadogo watskaofukuzwa!!!!!!?basi