Kipindi Cha Magufuli rushwa ilipotea ila tu atayajua haya kama wewe ni mtu wa mishemishe hapa mjini kama upo upo tu hauwezi kuyajua hayaJibu swali, nani amesema rushwa ilipotea? Hata kuelewa swali nako ni shida!
Kama huwezi kujibu swali langu, basi jibu la mleta mada. Ameuliza kama rushwa imehalalishwa.
Wewe ndiye mropokaji sasa. Kwani ni nani aliyesema rushwa iliisha? Rushwa ilikuwepo, lakini haikuwa nje nje kama ilivyo sasa hivi. Sasa hivi mtu unaombwa rushwa mchana kweupe, tena mbele ya kadamnasi, ndiyo sababu mleta mada akauliza kama imehalalishwa!Miaka yote rushwa ipo haijawahi kuisha whether JK au JPM rushwa ipogo. kasome ripoti za TAKUKURU kila mwaka ni mabilion wanaripoti yalitolewa kama rushwa haijalishi Rais alikua nani? Msiwe mnaropoka tu.
Mimi nikuzuie kuwaza utakalo?Kwa nini?Wewe waza,penda,chukia au vyovyote utakavyo kama id yako.Niache nami niwe na mawazo na mitizamo yangu.Umerogwa SI Bure. Muda na wakati wote unafikiria na kitengeneza ubaya Kwa magufuli. Mpaka umekuwa zuzu
Acha uongo hivi si ndio JPM alihalalisha kuwapa rushwa traffic akisema ni ya kubrush viatu?lakini haikuwa nje nje kama ilivyo sasa hivi.
Bora! Kuliko mambo ya kutekana na kupigana risasi mchana kweupe rushwa haiuwi.Wakuu hivi ni mimi sina taarifa au vipi? Mbona kila sehemu ukienda watu wanadai rushwa bila kificho? Immigration, TANESCO hata TRA. Nini kimetokea ghafla?
1. Immigration - ili upate passport lazima ujipange sawasawa, zile siku zilizoainishwa ni geresha?
2. Kuwekewa umeme - unaambiwa hamna nguzo, hadi uwape chochote, nguzo zinapatikana siku hiyo hiyo.
3. Tunduma na Kasumulu Border posts - kila ukigusa Ni mwendo wa rushwa kuanzia (polis, TRA),
4. Hospitali - Mwananyamala pamoja na makamera kukaa kila corridor hiyo nyomi Lazima ulazimishwe kutoa Chochote. Dawa akanunue kwenye pharmacy za staff nje ya geti
5. POLISI @trafiki - highway bagamoyo @msata kabuku SAME mwanga.
EehNenda Ardhi.
Utafurahi.
Wakuu hivi ni mimi sina taarifa au vipi? Mbona kila sehemu ukienda watu wanadai rushwa bila kificho? Immigration, TANESCO hata TRA. Nini kimetokea ghafla?
1. Immigration - ili upate passport lazima ujipange sawasawa, zile siku zilizoainishwa ni geresha?
2. Kuwekewa umeme - unaambiwa hamna nguzo, hadi uwape chochote, nguzo zinapatikana siku hiyo hiyo.
3. Tunduma na Kasumulu Border posts - kila ukigusa Ni mwendo wa rushwa kuanzia (polis, TRA),
4. Hospitali - Mwananyamala pamoja na makamera kukaa kila corridor hiyo nyomi Lazima ulazimishwe kutoa Chochote. Dawa akanunue kwenye pharmacy za staff nje ya geti
5. POLISI @trafiki - highway bagamoyo @msata kabuku SAME mwanga.
Wala usitaje, ni nchi nzima! Walisharuhusiwa wale Kwa urefu wa kamba zao! Kudadeki!pole sana