Wakuu hivi ni mimi sina taarifa au vipi? Mbona kila sehemu ukienda watu wanadai rushwa bila kificho? Immigration, TANESCO hata TRA. Nini kimetokea ghafla?
1. Immigration - ili upate passport lazima ujipange sawasawa, zile siku zilizoainishwa ni geresha?
2. Kuwekewa umeme - unaambiwa hamna nguzo, hadi uwape chochote, nguzo zinapatikana siku hiyo hiyo.
3. Tunduma na Kasumulu Border posts - kila ukigusa Ni mwendo wa rushwa kuanzia (polis, TRA),
4. Hospitali - Mwananyamala pamoja na makamera kukaa kila corridor hiyo nyomi Lazima ulazimishwe kutoa Chochote. Dawa akanunue kwenye pharmacy za staff nje ya geti
5. POLISI @trafiki - highway
bagamoyo @msata
kabuku SAME mwanga.