Rushwa imepeleka Kombe la Dunia Qatar, majuto yamebaki kwa mashabiki

Rushwa imepeleka Kombe la Dunia Qatar, majuto yamebaki kwa mashabiki

Kombe la dunia Qatar nalikataa kwasababu limenisimamishia ligi yangu pendwa, lakini hizo sababu nyingine wanazotoa wazungu sizielewi.
 
wazungu wenyewe ndio wamekataa kombe ilo kuchezwa mwezi wa 6 Qatar kwasababu ya joto ,Qatar walisema kama ishu ni Joto kutakuwa na AC viwanja vyote mitaani adi barabarani[emoji23][emoji23] jamaa wana jeuri ya pesa ndio nchi iliyovunja record kwa maandalizi ya kombe la dunia dola billioni 200 sawa na tirioni 456 na zaidi za kitanzania yani bajeti yetu ya miaka karibu 9 watu wanatumia kuandalia kombe tu, na nasikia wameweka record nyingine ya kuweza kuweka screen yani smart TV yenye ubora wa 8K siyo 4k kama za uku kwetu yenye urefu wa mita 62 kwa ajili ya watu watakaokuwa nje ya uwanja kuweza kuangalia..
 
Wakati Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yakiwa karibu kabisa kuanza, kupitia video fupi Mhariri wa uchambuzi kutoka shirika la habari la BBC Ros Atkin ameiongelea miaka ya tuhuma za rushwa ndani ya FIFA inayosadikiwa kupelekea Qatar kutunukiwa uwenyeji wa Kombe la Dunia 2022.

”Jumatatu iliyopita Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter alitamka kuwa ”kufanya mashindano haya nchini Qatar ni kosa”

Jumanne, Balozi wa Kombe la Dunia nchini Qatar Khalid Salman alisema kuwa ”mahusiano ya jinsia moja ni uharibifu katika akili”

Swali kubwa ni je ”iliwezekanaje kwa nchi yenye watu milioni 3 , joto kali sana, na ambapo mahusiano ya jinsia moja ni kinyume na sheria kuchaguliwa kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia?”

Kabla ya kupigwa kura, wanakamati wawili wa kamati kuu ya FIFA walitolewa baada ya uchunguzi uliofanywa na Sunday Times kubaini kuwa watu hao walikuwa wametoa ofa ya kuuza kura zao. Wanakamati wengine wote waliichagua Qatar na kuiacha Marekani ambayo ilionekana kupendwa zaidi.

Mwaka 2011 gazeti la Sunday Times liliripoti kuwa wanakamati wengine wawili walikuwa wamelipwa dola milioni moja na nusu kila mmoja ili kuipigia kura Qatar.

Siku chache baadae, barua pepe ilivuja iliyoonyesha Katibu wa FIFA wa kipindi kile Jerome Valcke akiwaongelea maafisa wa Qatar kwa kusema ”alidhani inawezekana kununua FIFA kama walivyonunua Kombe la Dunia.”

Kufikia mwaka 2012 uchunguzi mzito kuhusiana na mienendo ndani ya FIFA ulishaanza. Baadae ilijulikana kuwa FBI imekuwa ikiichunguza FIFA kwa miaka mingi na iligundua rushwa, utakatishaji fedha, malipo haramu yakiwa kama sehemu ya kufanya biashara ndani ya FIFA.

Hata hivyo mambo hayo hayakuhusiana moja kwa moja na jinsi Qatar iliyopata uwenyeji wa Kombe la Dunia.

Tunachofahamu ni kuwa hadi sasa wanakamati 11 kati ya 22 wa Kamati Kuu ya FiFA waliofikia uamuzi ule wamesimamishwa, kulipishwa faini, kufungiwa na wengine kushtakiwa kwa sababu mbalimbali.

Wiki hii Blatter amesema, "Ni hakika hii ilihusu pia pesa, kwa hili namaanisha nchi na siyo watu."

Miaka 12 baadae Qatar bado inakanusha kuhusika na lolote ambalo ni kinyume na sheria au maadili. Swali linabakia, kwanini mashindano haya yanafanyikia Qatar?
Ushoga sio concerned kwa mtu ambaye sio shoga, tatizo ni kukataza mpaka bia yaan unywe mafichoni
 
Wakristo wengi ndo wanapinga na kulaumu Qatar kuwa mwenyeji wa world cup sema hapo kwenye ushoga umezingua kwa hyo unataka mruhusiwe mupigane pipe shenzi kabisa
IMG-20221113-WA0002.jpg
 
Platini na wenzie walikula rushwa ndefu sana
Ila Qatar walitaka sifa tu kushindana na Saudia na UAE kwa kila kitu
Hawakuwaza haya kuwa jamaa kwenye mpira ni utalii tosha na wanakuja kila aina ya watu

Pombe lazima, mashoga hawawezi kuwazuia kwani wamekubali wenyewe
Naona hawakuwazia haya wao waliona ni mpira tu na ijulikane duniani
 
wazungu wenyewe ndio wamekataa kombe ilo kuchezwa mwezi wa 6 Qatar kwasababu ya joto ,Qatar walisema kama ishu ni Joto kutakuwa na AC viwanja vyote mitaani adi barabarani[emoji23][emoji23] jamaa wana jeuri ya pesa ndio nchi iliyovunja record kwa maandalizi ya kombe la dunia dola billioni 200 sawa na tirioni 456 na zaidi za kitanzania yani bajeti yetu ya miaka karibu 9 watu wanatumia kuandalia kombe tu, na nasikia wameweka record nyingine ya kuweza kuweka screen yani smart TV yenye ubora wa 8K siyo 4k kama za uku kwetu yenye urefu wa mita 62 kwa ajili ya watu watakaokuwa nje ya uwanja kuweza kuangalia..
Na wanasema kombe la Dunia likiisha wanaya dismantled viwanja na viti vyote kugawa nchi masikini

Hapo naona kuna mataifa wameisha weka order
 
Okay nimekusoma, nilihis ni mambo ya LGBT tu pekee......Ila hata hivo Qatar imewekaa bayana kuwa hawatabadili iman yao ya dini ndani hizo siku 28. Kwaio hao jamaa acha waongee tuu
David Beckham kapewa £10m na Qatar awe Ambassador wa World Cup
Sasa njoo usikie mashoga wanavyomponda leo
Eti David ainamishe kichwa chini kwa aibu
 
Ona haka nako,kanakurupuka tu kucomment ili nakenyewe kasisahaulike kua kamo humu JF,

Hivi umeisoma Thd na kuielewa kua inahusu nini?
Si ungereply hiyo thread yenyewe ndgu yang, mbona umeifata comment yangu??

Punguza mikurupuko mzee.
 
Kwahiyo kwakuwa Qatar inapinga mahusiano ya jinsia moja wazungu wanaona haikutakiwa kuwa mwenyeji wa World Cup?

Laana kabisa.
Wazungu ni washenzi sana, mbona Urusi hatukuwaona hawa mashoga na hawakuongea lolote?
 
wazungu wenyewe ndio wamekataa kombe ilo kuchezwa mwezi wa 6 Qatar kwasababu ya joto ,Qatar walisema kama ishu ni Joto kutakuwa na AC viwanja vyote mitaani adi barabarani[emoji23][emoji23] jamaa wana jeuri ya pesa ndio nchi iliyovunja record kwa maandalizi ya kombe la dunia dola billioni 200 sawa na tirioni 456 na zaidi za kitanzania yani bajeti yetu ya miaka karibu 9 watu wanatumia kuandalia kombe tu, na nasikia wameweka record nyingine ya kuweza kuweka screen yani smart TV yenye ubora wa 8K siyo 4k kama za uku kwetu yenye urefu wa mita 62 kwa ajili ya watu watakaokuwa nje ya uwanja kuweza kuangalia..
Wajomba wana jeuri mnoo.

Sasa wao wananufaika nini mkuu, maana kusema pesa yao itarudi, sidhani kabisa maana naskia hadi pesa ya maandalizi toka fifa wameikataa.

Nikajua labda ni ushawaishi wa nchi za magharibi ili kupenyeza ajenda zao ila kwa hapo naanza kuamini ni ujeuri yao tu.
 
Haya yote yamekuja baada ya wajomba zake mama kukataa ushoga nchini mwao.
 
Back
Top Bottom