Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lazima kombe litembee mabara yoteSikubaliani na Ushoga ila kombe la dunia kufanyika Qatar ni makosa makubwa ni rushwa tu ndio imefanya haya
Ushoga sio concerned kwa mtu ambaye sio shoga, tatizo ni kukataza mpaka bia yaan unywe mafichoniWakati Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yakiwa karibu kabisa kuanza, kupitia video fupi Mhariri wa uchambuzi kutoka shirika la habari la BBC Ros Atkin ameiongelea miaka ya tuhuma za rushwa ndani ya FIFA inayosadikiwa kupelekea Qatar kutunukiwa uwenyeji wa Kombe la Dunia 2022.
”Jumatatu iliyopita Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter alitamka kuwa ”kufanya mashindano haya nchini Qatar ni kosa”
Jumanne, Balozi wa Kombe la Dunia nchini Qatar Khalid Salman alisema kuwa ”mahusiano ya jinsia moja ni uharibifu katika akili”
Swali kubwa ni je ”iliwezekanaje kwa nchi yenye watu milioni 3 , joto kali sana, na ambapo mahusiano ya jinsia moja ni kinyume na sheria kuchaguliwa kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia?”
Kabla ya kupigwa kura, wanakamati wawili wa kamati kuu ya FIFA walitolewa baada ya uchunguzi uliofanywa na Sunday Times kubaini kuwa watu hao walikuwa wametoa ofa ya kuuza kura zao. Wanakamati wengine wote waliichagua Qatar na kuiacha Marekani ambayo ilionekana kupendwa zaidi.
Mwaka 2011 gazeti la Sunday Times liliripoti kuwa wanakamati wengine wawili walikuwa wamelipwa dola milioni moja na nusu kila mmoja ili kuipigia kura Qatar.
Siku chache baadae, barua pepe ilivuja iliyoonyesha Katibu wa FIFA wa kipindi kile Jerome Valcke akiwaongelea maafisa wa Qatar kwa kusema ”alidhani inawezekana kununua FIFA kama walivyonunua Kombe la Dunia.”
Kufikia mwaka 2012 uchunguzi mzito kuhusiana na mienendo ndani ya FIFA ulishaanza. Baadae ilijulikana kuwa FBI imekuwa ikiichunguza FIFA kwa miaka mingi na iligundua rushwa, utakatishaji fedha, malipo haramu yakiwa kama sehemu ya kufanya biashara ndani ya FIFA.
Hata hivyo mambo hayo hayakuhusiana moja kwa moja na jinsi Qatar iliyopata uwenyeji wa Kombe la Dunia.
Tunachofahamu ni kuwa hadi sasa wanakamati 11 kati ya 22 wa Kamati Kuu ya FiFA waliofikia uamuzi ule wamesimamishwa, kulipishwa faini, kufungiwa na wengine kushtakiwa kwa sababu mbalimbali.
Wiki hii Blatter amesema, "Ni hakika hii ilihusu pia pesa, kwa hili namaanisha nchi na siyo watu."
Miaka 12 baadae Qatar bado inakanusha kuhusika na lolote ambalo ni kinyume na sheria au maadili. Swali linabakia, kwanini mashindano haya yanafanyikia Qatar?
uarabuni ni mfalme akiamua tu imepita hakuna bunge wala kitu gani kujadili vyenginevyo, mabajeti ya ajabu ni rahisi kupitaKwamba Qatar Wana Pesa Chafu kuizidi Marekani?
Udini upo wapi? Au una allergy na waislamu?Qatar hamna amsha amsha udini mwingi.
Na ndio vizuri hivyo, akisema hatutaki mashoga basi mashoga wanakaa mbaliuarabuni ni mfalme akiamua tu imepita hakuna bunge wala kitu gani kujadili vyenginevyo, mabajeti ya ajabu ni rahisi kupita
Kwenye Iman ya kiislamu pombe ni halal? au waislamu wanaruhusiwa kuchagua dhambi?Kwahiyo wewe umekasirika kwa mashoga kukataliwa?
Na wanasema kombe la Dunia likiisha wanaya dismantled viwanja na viti vyote kugawa nchi masikiniwazungu wenyewe ndio wamekataa kombe ilo kuchezwa mwezi wa 6 Qatar kwasababu ya joto ,Qatar walisema kama ishu ni Joto kutakuwa na AC viwanja vyote mitaani adi barabarani[emoji23][emoji23] jamaa wana jeuri ya pesa ndio nchi iliyovunja record kwa maandalizi ya kombe la dunia dola billioni 200 sawa na tirioni 456 na zaidi za kitanzania yani bajeti yetu ya miaka karibu 9 watu wanatumia kuandalia kombe tu, na nasikia wameweka record nyingine ya kuweza kuweka screen yani smart TV yenye ubora wa 8K siyo 4k kama za uku kwetu yenye urefu wa mita 62 kwa ajili ya watu watakaokuwa nje ya uwanja kuweza kuangalia..
David Beckham kapewa £10m na Qatar awe Ambassador wa World CupOkay nimekusoma, nilihis ni mambo ya LGBT tu pekee......Ila hata hivo Qatar imewekaa bayana kuwa hawatabadili iman yao ya dini ndani hizo siku 28. Kwaio hao jamaa acha waongee tuu
Hizo sheria umewahi kuziona wapi zaidi ya nchi za kiislam.Udini upo wapi? Au una allergy na waislamu?
Si ungereply hiyo thread yenyewe ndgu yang, mbona umeifata comment yangu??Ona haka nako,kanakurupuka tu kucomment ili nakenyewe kasisahaulike kua kamo humu JF,
Hivi umeisoma Thd na kuielewa kua inahusu nini?
Wewe si ndio uliyeanza kuniquote, au ulikua usingizini jomba?Si ungereply hiyo thread yenyewe ndgu yang, mbona umeifata comment yangu??
Punguza mikurupuko mzee.
Wazungu ni washenzi sana, mbona Urusi hatukuwaona hawa mashoga na hawakuongea lolote?Kwahiyo kwakuwa Qatar inapinga mahusiano ya jinsia moja wazungu wanaona haikutakiwa kuwa mwenyeji wa World Cup?
Laana kabisa.
Basi wapo vizuri haloo hawa jamaa ni hatari bwanaNa wanasema kombe la Dunia likiisha wanaya dismantled viwanja na viti vyote kugawa nchi masikini
Hapo naona kuna mataifa wameisha weka order
Nenda reply #9 na #28 utajua nani alieanza kumquote mwenzie.Wewe si ndio uliyeanza kuniquote, au ulikua usingizini jomba?
Wajomba wana jeuri mnoo.wazungu wenyewe ndio wamekataa kombe ilo kuchezwa mwezi wa 6 Qatar kwasababu ya joto ,Qatar walisema kama ishu ni Joto kutakuwa na AC viwanja vyote mitaani adi barabarani[emoji23][emoji23] jamaa wana jeuri ya pesa ndio nchi iliyovunja record kwa maandalizi ya kombe la dunia dola billioni 200 sawa na tirioni 456 na zaidi za kitanzania yani bajeti yetu ya miaka karibu 9 watu wanatumia kuandalia kombe tu, na nasikia wameweka record nyingine ya kuweza kuweka screen yani smart TV yenye ubora wa 8K siyo 4k kama za uku kwetu yenye urefu wa mita 62 kwa ajili ya watu watakaokuwa nje ya uwanja kuweza kuangalia..