Russia sio nchi ya kuitegemea kwenye muungano wa kijeshi na ulinzi

Russia sio nchi ya kuitegemea kwenye muungano wa kijeshi na ulinzi

Iran alitega sehemu mbili,kuna makubaliano alikuwa anayafanya na nchi za Magharibi wkt huohuo anafanya na Urusi.Alipendelea zaidi ya nchi za Magharibi kwakuwa yangempunguzia ama kumuondolea baadhi ya vikwazo vya kiuchumi.
Kwote hakufanikiwa kusaini na Israel akafanya mashambulizi ya kivita.
 
Hivi kwanini waisrael hawaifanyi nchi yao iwe kama Marekani kwa kiuchumi na kijeshi kuliko hivi ilivyo kwamba tunaambiwa kuwa wao ndio kila kitu mara wapo kila sehemu?
Wewe unataka iweje, nchi ya watu milioni 10 lkn angalia GDP yake kisha ilinganishe na ya nchi yako yenye walalahoi milioni 70+
 
Hivi kwanini waisrael hawaifanyi nchi yao iwe kama Marekani kwa kiuchumi na kijeshi kuliko hivi ilivyo kwamba tunaambiwa kuwa wao ndio kila kitu mara wapo kila sehemu?
Israel ni kambi kubwa la jeshi la marekani na Britain pale middle east
 
Wewe unataka iweje, nchi ya watu milioni 10 lkn angalia GDP yake kisha ilinganishe na ya nchi yako yenye walalahoi milioni 70+
Mbona south korea, Qatar na japan zina watu kibao lakini na viinchi vingine kibao vinauchumi na technologia inayoonekana kwa macho na sio ya kubumba ya israel kila mwaka wamekalia technologia ya kulima matunda tu
 
Russia majuzi hapa alikuwa anapewa silaha na Iran, pamoja na North Korea, na China walikuwa wana smuggle wakaonekana wakaonywa wakaacha.
China ilisema kama ingekuwa imeisadia Urusi leo vita isingekuwa kama tunavyoona mambo yangekuwa mabaya zaidi kwa Ukraine

Na hakuna taifa la kuizuia China sio Ufaransa, Ujerumani, Uingereza au Poland hawana ubavu huo hata Marekani kama China wakiamua kutoa msaada wa kijeshi kwa Urusi.

Wataishia vitisho tu
​
 
Iran alitega sehemu mbili,kuna makubaliano alikuwa anayafanya na nchi za Magharibi wkt huohuo anafanya na Urusi.Alipendelea zaidi ya nchi za Magharibi kwakuwa yangempunguzia ama kumuondolea baadhi ya vikwazo vya kiuchumi.
Kwote hakufanikiwa kusaini na Israel akafanya mashambulizi ya kivita.
Alilenga zaidi biashara yake ya mafuta na gas,sasa Russia vyote hivyo anavyo.
 
Imechukua siku tatu tu Marekani kuingia kwenye vita kumsaidia Israel ila mpaka sasa Russia anaangakia mshirika wake anapigwa na watu kibao.

Jeshi la Marekani lina jisifu kuthibit anga ya Iran, na kusema wako vizuri. Russia uko wapi?
View attachment 3373731
Kwa nini ujiingize kwenye vita vya wengine? Vita ni gharama vina cost uchumi, maisha
 
China ilisema kama ingekuwa imeisadia Urusi leo vita isingekuwa kama tunavyoona mambo yangekuwa mabaya zaidi kwa Ukraine

Na hakuna taifa la kuizuia China Ufaransa, Ujerumani, Uingereza au Poland hawana ubavu huo hata Marekani kama China wakiamua kutoa msaada wa kijeshi kwa Urusi.

Wataishia vitisho t
​
Wanatishwa na vikwazo vya marekani tu.
 
Du wewe kweli umeota pembe za kichina china.

Wachukue Taiwani leo basi tuone mbabe nani?
Kipaumbele cha China ni peaceful reunification na Taiwan

Marekani imekuwa kwenye vita vya kiuchumi na kiteknolojia na China na hata kuzuia bidhaa za China tangu Trump akiwa raisi mwaka 2018

Je, so far Marekani imefanikiwa kuishusha China?

Trump alianzisha vita vya ushuru dhidi ya China April 2025, mwezi mmoja baadaye yeye ndiyo kapiga goti kwa China tena

Wiki mbili zilizopita Trump alimpigia simu Xi wawatume wawakikishi wa mataifa yao wakutane London

Kwa hiyo Trump alianzisha vita ambavyo vilikuwa nje ya uwezo wake
​
 
Back
Top Bottom