Russia World Cup 2018: France crowned World Champions after defeating Croatia 4-2

Russia World Cup 2018: France crowned World Champions after defeating Croatia 4-2

Leo Sweden na England zilibadili mchezo wao na hivyo kuvuruga utabiri wangu. England ilibadili mchezo na kucheza mchezo wa kushambulia ukiwa balanced sana kuliko siku za nyuma, wakati Sweden nayo ilibadili mchezo wake na kucheza mchezo wa kujihami kuliko sio za nyuma. Matokeo yake Engand imeshinda kinyume na matarajio yangu. Kwa upande wa Croatia na Urusi, ilikuwa ni wazi kuwa Urusi ilikuwa imefungwa isingekuwa yule jamaa aliyenawa mpira kwa makusudi katika eneo la hatari; hata hivyo utabiri wangu kwenye mchezo huo umetimia kwa njia ya penalty, sikutegemea ifikie hapo. Kwa mabadiliko hayo, sasa hivi msimamo utakuwa kama ifuatavyo:

(1) France, (2) Croatia, (3) Equal chances Belgium/England..
upload_2018-7-7_16-37-30.png
 
we jamaa bhana, ok me nnachojua kila mechi ina mipango yake kazi kubwa ya kocha kuangalia nguvu na udhaifu wa mpinzani wake kwahiyo kila mechi inakuwa na approach yake, mfano mzuri game ya Brazil Na Belgium, Wabelgiji Jana walienda kuzuia na kufanya mashambuliz ya kushtukiza yan counter attacks na kweli ikawalipa

let's wait and see
Mfumo waliyocheza jana ubelgiji kama sikosei ni 5-3-2 mbele alikuwa hazard na lukaku. Nyuma na kati walikuwa wengi plus Brazil hakuwa na kiungo wakaitumia hiyo advantage. Angalia kipindi cha kwanza game ilivyokuwa na kipindi cha pili, mchezo ulibadilika kabisa baada ya Brazil kufanya substitution ya Costa, Augasto na Ferminho. Costa winger mzuri sana anayejua kuuficha mpira na mwenye kasi, hiyo ikamlazimu courtinho kuwa namba 8 neymar kuwa 10, Costa 7. Sasa nini kilichofuata, mpira ulibadilika.

Kusema Belgium mashambulizi yao yalikuwa ya kushtukiza hapana, mchezo wao ulikuwa unaanzia nyuma kabisa hazard anazunguka na mpiraa kuanzia kati kabisa. Lukaku naye vilevile anaanzia kati kabisa liangalie goli la assist ya Lukaku. Kwa kifupi Belgium Mpira wao ni wa kasi. Na kufungwa Brazil kwa Jana inatokana na ubovu wa kocha kushindwa kuwatumia vizuri wachezaji.

Na match ya Croatia vs England, hii match naangalia huku nimevaa suti nyeusi yaani England tunamzika mapemaaaaa.
 
Atakachokifanya England jumatano watu watakimbiana humu, zitabaki stori England kaingia fainali kwa kucheza na timu nyepesi nyepesi (Wakati leo watu wanasema England hachomoki kwa Croatia, England atagota kwa Croatia)
Modric na lactic hahahaha England mtapata tabu sana tena sana. Andaa sala ya mazishi kabisa.
 
France vs Belgium apo France out, ukija England vs Croatia apo England baba jeni bai bai, final Belgium vs Croatia na apo ndo Belgium anachukua ndoo mwaka uhuu.Sitaki ubishi time will tell
Croatia mafundi sana, sema wamechoshwa na dakika 120 za leo! England watakuwa na nguvu za ziada maana hawakuchoka sana. Hata hivyo nawapa heko Croatia. Nitafurahi wakishinda.
 
Zagreb se pripremi. Bruxelles se prépare. [emoji111] [emoji111] [emoji111]
 
La
France vs Belgium apo France out, ukija England vs Croatia apo England baba jeni bai bai, final Belgium vs Croatia na apo ndo Belgium anachukua ndoo mwaka uhuu.Sitaki ubishi time will tell
Labda kante asicheze siku hiyo mnajua shughuli yake huyu jamaa huyu ndio anaeichezesha timu beki,kiungo,mshambuliaji pia
 
Nimegundua humu watu wengi wana chuki na England na wala hawashughulishi vichwa vyao kuangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa England na uzoefu walionao.
Wachezaji wa England wengi ni wachanga kwenye mechi za kimataifa na wapo pale kutengeneza jina na wala sio kuwabeba Fans. Timu toka imechaguliwa mpk inaondoka ilikuwa haipewi nafasi ya kufika hata nusu fainali, waingereza wenyewe waliipa mpk robo fainali lkn vijana wameonesha uwezo na kujituma kwa hali ya juu.
Pressure ambayo wanayo timu ya France na Belgium ni tofauti kabisa na pressure waliyonayo waingereza sababu Belgium alishapewa nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri. Wafaransa hawakupewa nafasi kubwa lkn wameandikwa sana kama timu yenye wachezaji vijana wenye vipaji ambao wanahitaji kuunganishwa tu ili wafike mbali.
Mechi ya Croatia na England, wengi mnaipa Croatia nafasi ya kushinda sababu ina Modric pale kati, mnasahau kuwa waingereza ni mabingwa wa mipira mirefu na cross. Hivyo kuipa Croatia nafasi ya kushinda dhidi ya England 'eti' kwa sababu tu kuna majina matatu makubwa mnakuwa hamjitendei haki, matokeo yake England akishinda mnakuja hapa na kusema inacheza na timu rahisi......kwenye kombe la dunia hakuna timu rahisi, kungekua na timu rahisi basi Spain na German wangekuwepo mpk leo
 
Back
Top Bottom