Rusumo: Mpaka pekee unaoweza kupitisha magendo yoyote hasa usiku

Rusumo: Mpaka pekee unaoweza kupitisha magendo yoyote hasa usiku

Kwa uongo uko vzr eti silaha na risasi unavusha tu Rwanda,juzi naona umeandika eti ulikua unawauzia M23 mabuti nikacheka Saana.

Yaani hao M23 wanaokua supported na serikali ya Rwanda/ jeshi Lao(RDF) liache kuwapa buti uje kua wewe mwananzengo ndio uwauzie mabuti [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Naona uko busy na spinning.Au ni mtumishi wa hapo mpakani?
Unaitakatisha story mleta mada aonekane hana point
 
Mpaka wa Tanzania na Rwanda upande wetu Tanzania ndio mpaka pekee unaoweza kupitisha magendo ya aina yoyote iwe kutokea Rwanda ama Congo DR.

Ndio mpaka unaolindwa kizembe kuliko huenda kuliko mipaka yote ya Tanzania!

Suma JKT eti ndio walinzi wakuu wa Exit gate letu pale Rusumo huku nyakati za usiku maafisa wa forodha na usalama wa taifa wakiwa ama baa wakilewa ama makwao wakikoroma.

Aibu zaidi ni pale exit gate letu kuelekea Rwanda ifikapo saa 5 usiku huwezi kukuta afisa wa forodha pale na ukiuliza unaambiwa ndiyo kawaida yao huwa wanaenda kulala hadi saa 10 alfajiri kesho yake jambo ambalo huwa linasababisha foleni ya maroli usiku.

Ajabu ukivuka upande wa Rwanda maafisa wao wote huwepo kwa saa 24 tena kamwe hukuti amesinzia hata kwa bahati mbaya!

Hii ni aibu kubwa kwa mamlaka za Tanzania.
😇😇😇😇😇
 
Itasikitisha sana, endapo hizi taarifa zitakua na ukweli...
 
Wafuatiliwe,wachukuliwe hatua stahki.
 
Back
Top Bottom