benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC), jana ilimtangaza Ndugu, William Samoei Arap Ruto kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Kenya. Ruto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, na amehudumu chini ya Rais Uhuru Kenyatta kwa takribani miaka 10 sasa.
Pamoja na urafiki wa muda mrefu wa wawili hawa lakini mara kadhaa walikuwa wakipishana kauli na mwaka jana walikwaruzana kiasi cha Rais Kenyatta, kuamua kumuunga mkono mgombea urais kupitia Azimio la Umoja, Raila Odinga "Baba" akimtosa makamu wake Ruto aliyesimama kwa tiketi ya Kenya Kwanza.
Baada ya kutangazwa ushindi wa Ruto kuwa Rais Mteule wa Rais ya Kenya, maswali yamekuwa mengi vichwani mwa watu wengi.
Je Rais Uhuru Kenyatta ni kweli ameshindwa? Ni kweli kabisa Rais Kenyatta alichagua upande ambao hakua na uhakika wa kushinda?
Mwanafalsafa Muitaliano, Niccolò di Bernardo dei Machiavelli aliwahi kusema ni mpumbavu pekee anayeweza kupoteza uchaguzi akiwa madarakani, je tumuweke Uhuru katika hili kundi la Machiavelli au tuanze kuwa kwamba kuna namna Baba amechezewa mchezo?
Huyuhuyu Uhuru aliwahi kuwaambia Wakenya yeyey akitoka madarakani ataiacha nchi kwa kijana zaidi yake na sio kwa mzee, Je ndio tuseme amelihakikisha hilo?
Je, kugombana kwake na Ruto ilikuwa ni sehemu ya kumsafishia njia na kumuondoa kwenye kivuli cha madhila ya Serikali aliyohudumu kwa miaka 10?
Wakati bado unatafakari nakuacha na mfano huu:
"UHUU na RUU walikuwa marafiki. RUU akamwomba UHUU amuamchie kibanda chake cha mihogo kwa kuwa juma amemaliza muda wake…..........UHUU akamwambia RUU kuwa akimwachia kibanda ghafla atatengeneza uadui na wengine kwani kila mtu anataka kibanda hicho, lakini pia itaonekana kama wanapokezana kijiti …....... UHUU na RUU wakapanga kuwa wagombane kwa muda mrefu …..ugomvi wao ulidumu kwa mwaka mmoja hivi na watu wote mtaani waliamini hivyo........uchaguzi ukaja, HADHARANI, UHUU akamuunga mkono BABA, ila kwa kifupi ni kwamba jana UHUU kampa RUU kibanda."
Tafakari, Tujadili.