Huu ni mchezo umechezwa. Akili kubwa sana imetumika. Raila kauzwa.
Hili igizo la ugomvi ilikuwa ni muhimu kwa sababu zifuatazo;
1. Serikali inayomaliza muda wake huwa haipendwi hivyo Ruto angegombea toka serikali inayomaliza muda wake asingeuzika. Hivyo ilibidi wajifanye wanagombana ili chuki dhidi ya serikali inayomaliza muda wake isimuhusu Ruto.
2. Rais kumaliza muda wake na kumuachia makamu wake ingeleta dhana ya Ufalme na wananchi wangemkataa Ruto.
3. Hata angeuzika na akashinda kiuhalali au kwa kuiba kura, kutangazwa kwake Ruto kungeleta fujo kubwa hivyo ilibidi serikali ijifanye inamuunga mkono Odinga ili akitangazwa kushindwa ionekane hapakuwa na namna.
4. Serikali inayoondoka madarakani mara nyingi inachukiwa, hivyo Kenyata kumuunga mkono Raila ni kumuhamishia lawama zake hivyo wasiompenda Kenyata na serikali yake lazima wamchukie na mgombea wake / anayemuunga mkono. A friend of my enemy is my enemy.
5. Kujifanya Uhuru na Ruto wanagombana ni kumtafutia kura za huruma kwa Ruto kwamba kasalitiwa na ananyanyaswa.
6. Uhuru kumuunga mkono Raila ni kumvuta karibu ili kumshauri vibaya na kuchota siri za kambi yake wakati wa uchaguzi.
7. Uhuru kumuunga mkono Raila ni kuonesha kuwa watoto wa viongozi wanataka kupeana madaraka so Ruto anajitokeza kama Hustler, son of no body ili kuwavuta watu wengi wa hali ya chini.
Hapa Uhuru kafaulu kumuachia jamaa yake kama walivyoahidiana.