Basi wewe una akili nyingi kuliko CAG aloyetoa hati safi. Huko kwenu ruzuku ina kazi moja tu eti?
Najaribu kupiga hesabu za kufikirika hapa. Ebu fikiria Chadema wanapokea ruzuku milioni mia nne(TZS.400 million) kwa mwezi. Pia fikiria kuwa mpaka sasa wamepewa ruzuku kwa miezi yote ndani ya miaka minne. Hivyo, mpaka sasa watakuwa wamekusanya karibu bilioni kumi na tisa (TZS 19 bilioni). Pia inasemwa wabunge wake walikuw wanakatwa mishahara/ posho kila mwezi kwa ajili ya kuendesha chama na mambo mengine.
Sasa turudi kwenye ununuzi wa magari. Ebu fikiria kwa wastani kila gari limenunuliwa kwa shillingi 60 milioni( pamoja na kodi na ushuru). Hivyo, Chadema watakuwa wametumia shilingi 1.5 bilioni kwenye ununuzi wa magari.
Bilioni 19 kutoa bilioni 1.5 zinabaki 17.5 bilioni. Sema bilioni 7.5 zimetumika kwenye shughuli za uendeshaji chama. Je. bilioni 10 za ela za kitanzania ambayo ni sehemu ya ruzuku imetumika kufanya nini!? Nimetoa maelezo haya nikijua yupo CAG anaye kagua mahesabu. Mimi si mkaguzi bali najaribu kufikiria namna Chadema wanavyotumia ruzuku.