denoo49
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 6,113
- 6,950
Wanabodi,
Japo ile clip ya Rwakatare kwenye Utube ni "bonafide genuine", nikimaanisha ni video ya ukweli na sio ya kupikwa au kufanyiwa maujanja yoyote, bali kwa mujibu wa sheria zetu za ushahidi, "law of Evidence", Lwakatare hawezi kushitakiwa kwa sababu ushahidi wa video ya utube hauwezi kutumika mahakamani kwa vile Tanzania bado hatuna e-legistlation on e-evidence.
Kwa mujibu wa sheria zetu, evidence must be original!. Hata wale vijana wa Ze Utamu wangekamatwa, wasingeweza kushitakiwa na hata ukimtukana mtu kwa kutumia e-mail au website, huwezi kushitakiwa!.
Kwenye E-laws kuna sheria mbili tulizipitisha ikiwemo Sosper, Anti Money Loundering na Sheria ya Anti Terorrist ambazo zote zina vipengele vya kukubali e-evidence lakini sina uhakika kama sheria zote hizi zilitengenezewa regulations za namna ya kutumika.
Mwaka 2006, nakumbuka wanasheria madada wawili, Dr. Hawa Senare na mdogo wake Mwanaidi Maajar, waliandika makala ndefu kuhusu madhara ambayo Tanzania itayapata kwa ukosefu wa E-law!.
Naendelea kulifanyia mapitio hili jambo na ikitokea nikajikuta mimi ndio nimepitwa na wakati, nitaiondoa hii thread!.
Najua nyingi ya hoja zitahusu "bonafide genuine", ile kwa sisi tunaofanya kazi za Audio Visual day&night, utatambua kwa naked ayes tuu kama picha imefanyiwa maujanja kwa kutazama flow na frames na utatambua kama imefanyiwa maujanja ya sauti kwa kusikiliza flow ya sauti na kuilinganisha na syncronization ya sound na lip movements!, hata waje wataalamu kutoka mbinguni, huwezi ku sinc 100% perfect!.
Nawatayarishia vipengele mahsusi vya kisheria ambavyo wangeweza kuvitumia na kwa kwanini hawawezi.
Angalizo: Hapa ninazungumzia ile clip ya utube tuu!, ikitokea original video ikapatikana!, hapa tutakuwa tunazungunza mengine!.
Pasco.
NB. Pasco wa jf sio mwanasheria bali alipitia pale UDSM Kitivo cha Sheria na kutoa tongotongo za sheria kwa kipindi cha miaka 4 full time!. Kwa sasa anaendeleza kazi ya Uandishi wa Habari wa Kujitegemea kwa Kujitolea!.
Pasco, mkuu kuna marekebisho ya TEA, yaliyofanyika mwaka 2007, kifungu cha 40A, umeishapata wasaa wa kukisoma kifungu hiki, na je mawazo yako unayapimaje kwenye kifungu hicho??