Rwakatare Hawezi Kushitakiwa Kwa Ushahidi wa "You Tube!"

Rwakatare Hawezi Kushitakiwa Kwa Ushahidi wa "You Tube!"

Yes kuna mtu hauziki kwa vile ama ni too low au bei yake ni too hivyo hivyo kuwa una affordable!.
Ikulu sio mahali pa majaribio!, sikuzote tumekuwa tukiwapangisha watu pale mahali kwa mazoea tuu, sasa tufike mahali yoyote anayetaka kwenda ikulu, tumuulize kwa kinaganaga, anataka kwenda ikulu kufanya nini?. Hivyo najiandaa kurudi on air soon ili kama kuna watu ambao ni wababaishaji wanataka kwenda ikulu, my role will be just to expose ubabaishaji wao na kuwaachia Watanzania waamue!. Kama kusema nitakuwa "mwiba mkali" umekutafsiri kuwa hizo ni tambo, then ni tambo nzuri tuu kwa kuanzia kwa sababu hata wakati nikiendesha "kiti moto", kuna watu walikuwa wakikaribishwa tuu, wanagwaya!, hii itasaidia sana kutikuwa na utitiri wa wagombea urais huku wengine wakiingia kujaribisha tuu na ku boost cv zao!. Tunataka 2015, ngoma iwe ama zao, ama zetu!, washindani wakuu wabaki wawili!. Hili la kutaka changes, please take time kupitia threads zangu za nyuma, utanielewa!. Choice ya mgombea wangu kwa CCM, alikuwa ni EL, ni kila nikimtaja, pia huwa naweka msisitizo, "ili tuupate ule ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!" na pia ili litimie lile neno la "rais wa 2015 lazima atoke Kaskazini!".
Pasco.
haya tutafika tu!
 
Mkuu Pasco acha kuruka sarakasi!!
Mkuu Blacktiger, pole!, majukwaa mengine ni too technical kiasi wenzetu kuona ni sarakasi!, tena afadhali yako, sarakasi ni mchezo wa kweli, wenzako waliozoea "kidali poo", wao wameona ni mazingaombwe!. Kuna hoja nyingine, kama hauzami kabisa, lazima utoke kapa!, ila usijali tuna majukwaa mengi tuu unaweza kufit kutafutia usingizi ila sio humu!, labda jaribu MMU au hata Chit Chat! unaweza ukapata usingizi.
G9T!.
Pasco.
 
Wewe pia umeishia kumsifia Pasco eti kaleta thread nzuri, ukasahau kuonyesha ni eneo gani kisheria ambalo ni Zuri ktk hiyo thread. Btw hivi unaelewa Sheria vzr au unakurupuka tu ili mradi tuone hiyo post yako.....
ukitaka kujua sheria vizuri soma sheria, mimi si mwanasheria na wala sina interest ya kusoma sheria; wenye kunielewa walinielewa, wewe hujanielewa na haunipunguzii kitu... sanasana naona unakurupuka tu kutaka kutoka nje ya mada

Ubora wa hii thread kwangu mimi ni namna Pasco alivyoweza kuvuta watu wenye uwezo wa kuijadili mada (sio wewe maana huna uwezo huo, ungekua nao ungeachana na mimi na kukomalia hoja)

I have gained from this thread, kwahiyo kwa upande wangu ni thread nzuri na wachangiaji wengi wamekua na manufaa sana kwa sie tusiojua sheria na tusio wanasheria

haya komalia hoja, kama huna hoja achana na mimi
 
Kimsingi mkuu Pasco pale kwenye "hununuliki" nilidhamiria kusema "huuziki".

Mtu mwenye tambo mimi huwa simfurahii, unapotamba kuwa utakuwa "mwiba" tena Ukadai kwa wanaotaka ikulu ili

kuijaribisha unaeleweka unachomaanisha. You dont want changes, why?. Huwezi kuwa mtetezi wa wanyonge na

unadhamiria kutumia kalamu yako vibaya, unajaribu kutoa taarifa kwa wale jamaa kwamba unaweza kusaidia kuzuia

mabadiliko.

Ndio maana nikakushauri kuwa endelea kujiuza huenda wakakuona hatimae. KILA LA KHERI.

Duh! Mkuu Mjuni Lwambo, nimekuvulia kofia.. Kelele zote za Pasco umezimaliza kwa lugha ya busara lakini iliyomchoma mpaka misho. He is what he is, anatumia usomi wake kuendeleza siasa za kihafidhina huku akijitahidi kujificha kama muumini wa mabadiliko. Bahati mbaya watu tunasahau kwamba tunachofanya kwa faida zetu leo, ni majuto kwa wanetu kesho. Nina uhakika watu kama Kingunge sasa hivi wanatamani wafe ili kukwepa aibu waliyoitengeneza kwa kuwa sehemu ya siasa za mtandao ambazo zinaitesa nchi huku wakishuhudia kwa macho yao!
 
Mkuu Ngambo Ngali, hii sio civil ya kumtafuta complainant hii ni criminal hivyo mshtaki angekuwa state!. The witness ni aliyekuwa anaelekezwa, wengi wanadhani muelekezwaji ndie lazima aliyepiga ile video!, its not necesarily inawezekana mpiga video ni mwingine nae pia ni shahidi namba 2. Aliyeipandisha youtube ni shahidi number 3!.

Ikithibitishwa Rwakatare was not acting alone, washirika wake pia watakamatwa na kuwa joined together wengine wakiwa ni accsesories before the fact na wengine after the facts wakithibitisha kuwa tayari jinai nyingine ya mipango hiyo dhalimu ilikwisha tekelezwa.

The offence ni " felony to plot to commit the criminal offence agains humanity!". Kwangu sina umeme nitakuwekea mpaka vifungu!.

Ila haya yote ni kama!.
Pasco.

Unajitahidi sana kuandika kama independent thinker lakini hapa ''Japo ile clip ya Rwakatare kwenye Utube ni "bonafide genuine", nikimaanisha ni video ya ukweli na sio ya kupikwa au kufanyiwa maujanja yoyote, bali kwa mujibu wa sheria zetu za ushahidi, "law of Evidence", Lwakatare hawezi kushitakiwa kwa sababu ushahidi wa video ya utube hauwezi kutumika mahakamani kwa vile Tanzania bado hatuna e-legistlation on e-evidence'' unajiingiza mkenge na kuonekana uko biased.
hutofautiani na mtu msomaji sana wa magezeti akaibuka na kusema mnajua wanabodi '' Wanasiasa ni malaya sana kuliko Madakatari'' nasema hivi kwa kuwa mimi ni msambazaji wa magazeti hapa mjini kila gazeti naona habari za ufuska wa wanasiasa sijawahi ona ufuska wa madaktari''
na wewe ndicho unacho maanisha unapohitimisha ubonafide geniune wa clip kwa kuwa wewe ni mtu
Audio Visual day & night, this is too low my friend.
Labda ungesema wewe unafanya kazi kwenye kampuni inayotengeneza software ya utambuzi na umetumia the latest siftware umegundua hiyo clip haijaongezwa wala kupunguzwa kitu toka kwenye original recording.

Mkuu pasco hitimisho la aina hiyo linatokana na kitu inaitwa Cognitive biases...
 
Mkuu Mzalendo kiukweli video ile si ya kupika hivyo hakuna upishi mwingine wowote on the making labda kama ndio uanze sasa!.

Pili Mzee wetu ni salama na mambo yake yote yanakwenda vizuri!. Si unajua lakini kuwa yeye ni "Yohana Mbatizaji tuu!" akinyoosha mapito ya "yule" ajaye!.

Wengi hawajui the motive behind ule mpango!, japo mlengwa wa mpango mzima ni yule mwandishi ila the motive behind sio yule mwandishi bali ni kumdhoofisha "the one and only" threat kwa "uimla" wa Chadema!. Mimi siko behind any threat to any party or anybody hivyo I'm very safe at least for the time being mpaka wakati nitakapo simama kuhesabiwa which is very soon from now, nitakuwa a very bad threat kwa "wababaishaji" wanaoitafuta ikulu ili kuijaribisha!.
Nitasimamia kuhakikisha wanaokwenda Ikulu 2015 ni wale tuu wanaostahili!. Hivyo soon nitakuwa "mwiba" wenye "ncha kali!" na kwa lessons za Kubebea na Kibanda, I'll be well equiped with A.38, A.45, kwenye gari nitatembea na Sub na hand gre, na nyumbani naweka full kit kuanzia LPG hadi AK 47!.
Pasco.
Hiyo Misilaa yote ya nini? Unamjuwa utakayepigana naye? Maana kuna wakati unaweza ukawa na AK47 kumbe adui ni mbu. Having that kind of preparations, ina maana unajuwa nini kilikosekana kwa Kibanda na Kubenena hadi yakawatokea yaliyowatokea.....
 
Wanabodi,
Japo ile clip ya Rwakatare kwenye Utube ni "bonafide genuine", nikimaanisha ni video ya ukweli na sio ya kupikwa au kufanyiwa maujanja yoyote, bali kwa mujibu wa sheria zetu za ushahidi, "law of Evidence", Lwakatare hawezi kushitakiwa kwa sababu ushahidi wa video ya utube hauwezi kutumika mahakamani kwa vile Tanzania bado hatuna e-legistlation on e-evidence.

Kwa mujibu wa sheria zetu, evidence must be original!. Hata wale vijana wa Ze Utamu wangekamatwa, wasingeweza kushitakiwa na hata ukimtukana mtu kwa kutumia e-mail au website, huwezi kushitakiwa!.

Kwenye E-laws kuna sheria mbili tulizipitisha ikiwemo Sosper, Anti Money Loundering na Sheria ya Anti Terorrist ambazo zote zina vipengele vya kukubali e-evidence lakini sina uhakika kama sheria zote hizi zilitengenezewa regulations za namna ya kutumika.

Mwaka 2006, nakumbuka wanasheria madada wawili, Dr. Hawa Senare na mdogo wake Mwanaidi Maajar, waliandika makala ndefu kuhusu madhara ambayo Tanzania itayapata kwa ukosefu wa E-law!.

Nimefanya mapitio ya baadhi ya sheria zetu kuhusu hili, ili audio na video, ikubalike kuwa ni ushahidi, inapaswa iwe ni the original recoding and not duplicate ya kwenye you tube. Wakifanikiwa kuipata computer iliyopandandisha kule youtube, wataichukua as an evidence, ushahidi wa storage devices kama DVD, Hard Disc na flash pia unakubalika kwa mujibu wa sheria ya Electronic Evidence Amendment Act 2007 yaliyopelekea kuongezwa kwa kifungu 40A kwenye sheria yetu ya Tanzania Evidence Act 1967 ambayo inaruhusu Information retrieved from computer systems, networks or servers; or records obtained through surveillance of means of preservation of information including facsimile machines, electronic transmission and communication facilities, the audio or video recording of acts or behaviours or conversation of persons charged utakubaliwa kama ushahidi, lakini video ile haiwezi kukubaliwa kwa sababu haujapatikana kwenye storage devices!.

Wangeweza kutumia kifungu namba 78 cha Tanzania Evidence Act ambacho kimeongezewa kipengele cha 78A ili kuruhusu printed out records kept or information system including but not limited to computers and storage devices , magnetic tapes, microfilm, video or computer display screen or any other form of mechanical or electronic data retrieval mechanism or other process which in itself ensures the accuracy of such print out, shall be received as evidence, kwa kuhalalisha download ya youtube, lakini hili litagonga mwamba in absence ya aliye upload ile video.
Najua nyingi ya hoja zitahusu "bonafide genuine", ile kwa sisi tunaofanya kazi za Audio Visual day&night, utatambua kwa naked ayes tuu kama picha imefanyiwa maujanja kwa kutazama flow na frames na utatambua kama imefanyiwa maujanja ya sauti kwa kusikiliza flow ya sauti na kuilinganisha na synchronization ya sound na lip movements!, hata waje wataalamu kutoka mbinguni, huwezi ku sinc 100% perfect!.

Nawatayarishia vipengele mahsusi vya kisheria ambavyo wangeweza kuvitumia na kwa kwanini hawawezi.
Angalizo: Hapa ninazungumzia ile clip ya utube tuu!, ikitokea original video ikapatikana!, hapa tutakuwa tunazungumza mengine!.

Paskali.
NB. Paskali sio mwanasheria bali alipitia pale UDSM Kitivo cha Sheria na kutoa tongotongo za sheria kwa kipindi cha miaka 4 full time!. Kwa sasa anaendeleza kazi ya Uandishi wa Habari wa Kujitegemea kwa Kujitolea!.
Kwa wale wenye interest zaidi kisheria, mnaweza kupitia hii link
ADMISSIBILITY OF ELECTRONIC EVIDENCE IN TANZANIA
Sasa Polisi kama wamepewa hints juu ya wahusika ambao ni Chadema kwa nini hawachukui hatua?
Kuna public crimes na private crimes.

  1. Public crimes ni uhalifu dhidi ya public, hapa polisi wakipokea hint "taarifa za kiinteligencia" ndio wanachukua hatua kama kuzuia maandamano.
  2. Private Crimes ni uhalifu dhidi ya private individuals, polisi haipokei tip wala hai act on this, bali mwenye tip kuhusu private crimes anapaswa aende polisi kuripoti.
  3. Private crime si kama vile kumchinja mtoto wako na kumfanya kitoweo, Kuua ni kosa la jinai, regardless umemuua nani, kitendo cha mauaji kikisha fanyika ni public crime, hatua zinachukuliwa bila yoyote kuhitajika kuripoti, ila kutishiwa maisha ni private crime lazima ukaripoti polisi ndipo hatua zichukuliwe!.
  4. Hata polisi wakipita nyumbani kwako, wakuesikia unampiga mkeo au mwanao, hawata ingilia kwasababu it's a private affairs, Ila mkeo akishitaki ndio inakuwa a public crime.
  5. Hata polisi wakipita kwako wakaona mlango umevunjwa na futuma, hawaji kuuliza kulikoni, lazima ukaripoti!.
  6. Lissu alipofuatiliwa na like gari, Nissan nyeupe, alitoa taarifa kwenye Press Conference only, ili polisi wa act alipaswa akaripoti polisi.
  7. Hivyo Dr.Slaa or Dr. Mollel kama , ana ushahidi wa uhalifu wa Chadema akaripoti polisi na sio kuzungumzia mitaani au Bungeni.
  8. Natoa wito, mtu yoyote mwenye ushahidi wowote usiotia shaka kuwa Chadema inahusika na uhalifu wowote, akaripoti polisi na Jeshi makini la polisi likipokea taarifa hiyo, litafanya uchaguzi, likijiridhisha, hatua za uchaguzi wa kijinai zitafanyika na ikithibitishwa, then ndicho kitu hiki nilicho kisema hapa Ikithibitika CHADEMA ilihusika na uvunjifu wa amani, then inapaswa kufutwa kwa mujibu wa katiba! kinatakiwa kufanyika.
P.
 
Back
Top Bottom