Rwakatare Hawezi Kushitakiwa Kwa Ushahidi wa "You Tube!"


Pasco, mkuu kuna marekebisho ya TEA, yaliyofanyika mwaka 2007, kifungu cha 40A, umeishapata wasaa wa kukisoma kifungu hiki, na je mawazo yako unayapimaje kwenye kifungu hicho??
 
Wataalam wa I.T na wengine wa uzoefu kazin, wanasema Feki na kuyataja mapungufu kadhaa ya video. Aliyesoma sheria miaka 4 ful T, anasema ni "bonafide genuine". bila kufafanua usahih wa mapungufu yaliyotajwa na wataalam.

Kama sio ushabik ni nin?.
Mkuu Chiya Chibi, ulitaka ufafanuzi gani zaidi ya huu, au nikuwekee usome tena!.
Kama hao wataalamu wa IT unaowaamini, wengine ni kutokana na uzoefu, nami tangu mwaka 1995 (sijui wewe ulikuwa na umri gani wakati huo), ndio nimerusha program yangu ya kwanza ikiitwa "Mada Moto" then 1997 ndipo nikaja na "Kiti Moto", na mpaka sasa hapa niliko, behind the camera ndipo ilipoafisi yangu!, hivyo kama ni mauzoefu na mimi nimo!, clip ile ni "bonafide genuine!".
Pasco.
 
Pasco, mkuu kuna marekebisho ya TEA, yaliyofanyika mwaka 2007, kifungu cha 40A, umeishapata wasaa wa kukisoma kifungu hiki, na je mawazo yako unayapimaje kwenye kifungu hicho??
Mkuu Denoo49, sisi wengine sio wazuri kwenye vifungu ndio maana mahakamani hatukanyagi, ukikiweka hapa nitakushukuru vinginevyo naomba reference!.
Pasco.
 
Pasco Pasco mwanangu mboni umekuwa mchungu hivoooo!?
 
Mkuu Mzalendo80, mimi nimeipenda sana hiyo "we will never vote for ..." umeyatamka ukiwa determinant as if umefanya "mass mobilization" mkakubaliana wote kuwa "we" katika umoja wetu sisi Watanzania!. Kabla ya uchaguzi wa 2015, vyama vyote vitasaini makubaliano ya "rules of the game" na chama chochote kitakachoshinda, ndio itakuwa "we!", sasa kama hii "we" yako haitokani na mass mobilization, then, "we" ya atakayeshinda jumla ndio itakuwa ni "we" ya watanzania Wote!, kwa mambo yalivyo mpaka sasa, i very seriously doubt hiyo "we" yako!.
Pasco.
 
Mkuu Denoo49, sisi wengine sio wazuri kwenye vifungu ndio maana mahakamani hatukanyagi, ukikiweka hapa nitakushukuru vinginevyo naomba reference!.Pasco.
binafsi pia, si mzuri kwenye sheria zaidi ya kujitoa tongotongo kwa kuijua sheria ngazi ya cheti miaka kadhaa iliyopita. Sema huwa ninapopata muda hupenda kudurufu vitabu vya sheria kwa manufaa yangu binafsi.Kifungu 40A, of TEA, "Evidence obtained under cover operations"In any cr.proceedings...(a) an information retrieved from computer systems, networks or servers; or(b)the records obtained through surveillance of means of preservation of information including facsimile machines, electronic transimission and communication facilities;(c)the audio or video recording of acts or behaviours or conversation of persons charged,shall be admissible in evidence.
 
hapa ninapata wasiwasi na 'capacity' ya jeshi la polisi. kuna na kutatokea challenge nyingi sana kwasababu jinsi ukizingatia jeshi linavyopatikana . inabidi zifanyike jitihada za dhati kuwa na jeshi dogo ambalo ni softiscated. ile habari ya kusema "umekosa nafasi, hata .....!! basi tukutafutie nafasi ya polisi" nadhani basi. Ukienda ulaya ukigusa tu kitu tayari informations ziko recorded na IT polices. inashindikana vipi kusema kila chuo chenye IT students tunachukua hawa kwenda jeshini, polisi au usalama wa Taifa. kesi nyingi serikali inashindwa na pesa zinapotea bure. Serikali itusaidie kufanya building capacity kwa jeshi letu. kuweza kufanya uchunguzi kitaalamu zaidi kuliko kukalia YUOTUBE masaa zaidi ya 100 ni aibu sana zingekuwa tano ingekuwaje? na hii inawatia wananchi mashaka na nyie.
 

Kazi nzuri wataalam!
 
Mkuu Denno, asante kwa hii, for the sake of this, hiyo audio na video, inamaanisha the original recoding and not duplicate ya kwenye you tube. Wakifanikiwa kuipata computer iliyopandandisha kule youtube, wataichukua as an evidence, ushahidi wa storage devices kama DVD, Hard Disc na flash pia unakubalika kwa mujibu wa sheria ya Electronic Evidence Amendment Act 2007 yaliyopelekea kuongezwa kwa kifungu 40A kwenye sheria yetu ya Tanzania Evidence Act 1967 ambayo inaruhusu Information retrieved from computer systems, networks or servers; or records obtained through surveillance of means of preservation of information including facsimile machines, electronic transmission and communication facilities, the audio or video recording of acts or behaviours or conversation of persons charged utakubaliwa kama ushahidi, lakini video ile haiwezi kukubaliwa kwa sababu haujapatikana kwenye storage devices!.

Wangeweza kutumia kifungu namba 78 cha Tanzania Evidence Act ambacho kimeongezewa kipengele cha 78A ili kuruhusu printed out records kept or information system including but not limited to computers and storage devices , magnetic tapes, microfilm, video or computer display screen or any other form of mechanical or electronic data retrieval mechanism or other process which in itself ensures the accuracy of such print out, shall be received as evidence, kwa kuhalalisha download ya youtube, lakini hili litagonga mwamba in absence ya aliye upload ile video.
 
hii ni tamthilia kushinda ya Isidindo!! mnakumbuka isue ya Osama! chuo kilipokea waomabji wa nafasi za urubani more than two year before action. mara Kigogo, Morogoro, Iringa, kitaeleka tu.
 
Mkuu Jack, si nimejieleza mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea?!, hizo bahasha atoe nani na kwa malengo yepi?.
kwahiyo yakitokea mauaji nami nikawa namkanda wa mauaji ukionyesha muuaji anavyoua,nikauweka utube watu wakaona muuaji hawezi kushitakiwa?kwa sababu tu iko online
 

Ungekuwa mbunge wa chadema, wafuasi wa chadema wangekupigania kukutea kuwa wewe ni mwanasheria. Si unaona Mnyika anavyotetewa kuwa hajaishia form six kwa sababu alipita pita kwenye corridors za UDSM...
 
Ndugu, mimi nadhani sheria ya ushahidi haina utata katika hii. Kumbe hakuna sababu ya kuuma maneno. kinacho wakwaza polisi kumfikisha mahakamani ni watashtaki na kosa gani. Maana hakuna sehemu hata moja katika video alitaja mlengwa.

Lakini ngoma ni watadhibitishaje kwamba hii si-video ya kugushiwa. Kumbuka kazi yake kama mshitakiwa ni kujenga shaka tu kwamba kunauzekano wa kuipika.

lakini sasa police wamisha kwaa kisiki kingine cha 24 hrs rule. maana ni dhaili pia kwamba 'fair trial' inaanzia hapo.
 

Je, iwapo Ludovick atakiri kuwa yeye ndiye aliyepiga ile picha na kusema kuwa original imeibiwa siku ile alivyotekwa na kuporwa kompyuta yake, itakuwaje?
 
Unaweza fafanua hiyo 'original video'?
nimeona Manyerere anasema ile video ilikuwepo mitaani siku nyiingi
unaweza sema chochote?
Mkuu The Boss, kwenye mada yangu, nimejikita tuu kwa hiki tulichonancho mkononi, ila nikatoa angalizo, kama original video itapatikana, hata kama ni duplicate of the original, hapa tutazungumza mengine!.

Saometimes vyama vina tend kuwaamini sana wanasheria wake kuwa ndio mabingwa, lakini wanajisahau kuwa hata hao wanasheria nao pia ni binadamu, kwenye sensetive issues kama hii, Chadema walipaswa to seek expert opinion kabla ya kukimbilia kukanusha kuwa the video is fake!. "better be sure than sorry!". Hakuna ubishi kuwa Lissu na Kicheere ni wanasheria wazuri, ila I'm not sure kama opinion yao ndio expert opinion kwenye mambo ya electronic evidence!.

Siku ile serikali inawasilisha ile rasimu ya kuundwa kwa tume ya kukusanya maoni, Chadema kwa kumtegemea Lissu pekee, iliamini ametoa pingamizi muswada ule usisomwe kwa mara ya pili, nikawaambia kitendo cha Lissu kuisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani, ni uthibitisho kuwa wameikubali hoja ya serikali, katika sentesi ya mwisho ya hotuba ya Lissu ndipo akaweka pingamizi!, Spika akalitupilia mbali pingamizi lile na kuendelea na hoja iliyo mezani, Chadema wakasusa wakatoka nje!. Nilibahatika kukutana na Lissu nikamuu kwa nini hakutanguliza pingamizi?, na badala yake kuendelea na hotuba!, hakuwa na jibu!.

Mimi nimewashauri Chadema, hii ni "political liability", they are left with only two options, kumfanya "Rwakatare ni mbuzi wa kafara" kwa kum disown kuwa was acting alone!, au kuendelea kumkumbatia kwa kung'ang'ania "the video is fake", na hivyo chama to suffer the consequences!.
Pasco.
 
kwahiyo yakitokea mauaji nami nikawa namkanda wa mauaji ukionyesha muuaji anavyoua,nikauweka utube watu wakaona muuaji hawezi kushitakiwa?kwa sababu tu iko online
Mkuu Elungfata, huo mkanda wako utasaidia tuu kwenye identification ya kuwawezesha polisi kumtia nguvuni mtuhumiwa, ila haiwezi kutumika as an evidence before the court of law mpaka ama origina ipatikane, ama uchukuliwe kama secondary evidence tuu hadi ipate collaborative primary evidence!.

Hata nikukutukana kwa e-mail, wewe kaiprint na uende popote ikashitaki, ni kazi bure!.
Pasco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…