Rwanda kujengwa bandari kavu kwa ajili ya mzigo wa DP World, Kagame nae anaiuza nchi Rwanda kwa Mwarabu?

Rwanda kujengwa bandari kavu kwa ajili ya mzigo wa DP World, Kagame nae anaiuza nchi Rwanda kwa Mwarabu?

Kwani hio bandari kavu inamilikiwa na DP world?, au ni mwezi mchanga. Tunaongelea waarabu kumiliki nchi yetu
Mwezi mchanga ni nyinyi mnaolishwa matango pori. Hakuna mwarabu anayekuja kumiliki nchi yako wakati wewe ukiwa hai na unazo akili zenye kuchanganyika na elimu ya darasani.
 
Hii mijitu haielewi aisee,tumesema mkataba kati ya Tanzania na DP ni wa kipumbavu,hatujasema kuwa dp ni mbaya ila mkataba ni wa hovyo,kuna mtu juzi hapa kaleta story ya dp world na england,kuna mzalendo wa kweli akamwekea hapa hapa mkataba kati ya dp england na dp Tanzania,ni mbingu na ardhi,tapeli anamtapeli mjinga asiyejua,ila when its due to pay bills he pays respectively,mkataba wa dp england unakazia zaidi majukumu ya dp na mipaka yao,mkataba wa dp na tz unakazia kabisa haki za dp ambazo serikali ni lazima ihakikishe dp inazipata,tena bila kikomo,sasa huu mkataba?au utekaji?
Hayo yameandikwa kwenye ule mkataba wa jumla, hii mikataba yenyewe ya kiutendaji haijasainiwa bado na ni mpaka yafanyike majadiliano ya kina kati ya pande hizi mbili.
 
..Dp ana bandari kavu Kigali.

..Tanganyika tuna bandari kavu ya kuhudumia mizigo ya Rwanda Isaka.

..Je, Dp akianza kuendesha bandari zote za Tanganyika bandari kavu ya Isaka itasalimika?
Anapewa sehemu tu ya bandari kuendesha, kama ilivyokuwa kwa TICTS. Hakuna anayeweza kuinunua nchi hii, hizo ni siasa za kunywea kahawa vijiweni.
 
Ni rasmi sasa Rwanda inamiliki bandari kupitia DPW. Kweli wajinga ndio waliwao
 
Ni rasmi sasa Rwanda inamiliki bandari kupitia DPW. Kweli wajinga ndio waliwao
Kwenye masuala ya kutengeneza pesa Kagame hataki kabisa siasa za majitaka kama za hapa bongo. Ameshaweka mazingira mazuri tatizo ni vichwa maji wengi waliopo hapa bongo.

Tatizo ni matutusa sisi watanzania tunaoshikiwa akili na hatujui ni kwa namna gani tunaweza kuzichukua tena akili zetu.
 
Unalinganisha mafua na Marburg ndugu yake ebola.

Hao wawekezaji huja na terms za mikataba kulingana na jinsi nchi yenyewe na viongozi wake walivyo!

Historia yenu na Rwanda kwenye mikataba ni mbingu na ardhi.
 
Hakuna mtu yyt mwenye akili timamu anayeweza kupinga uwekezaji wenye tija, tatizo ni pale terms za uwekezaji zinapokuwa hazina tija kwa taifa. Hata mpangaji wa chumba ana clear terms na mwenye nyumba, inakuwaje ishu kubwa km ya bandari isiwe na clear terms?
 
Mradi umeanza kupiganiwa tangu 2015 hivyo ni mjadala hata kuzipata hizi terms zinazoonekana sio nzuri.
 
Unalinganisha mafua na Marburg ndugu yake ebola.

Hao wawekezaji huja na terms za mikataba kulingana na jinsi nchi yenyewe na viongozi wake walivyo!

Historia yenu na Rwanda kwenye mikataba ni mbingu na ardhi.
Kinachojengwa DRC na Rwanda ni mwendelezo tu wa kinachotaka kufanyika TZ. Ni suala letu sisi kuwa na muitikio chanya kwenye suala lenye kulenga kuifikisha nchi katika uchumi wa kati wa juu.
 
Mpuuzi mmoja anadhani rwanda ni kama tanzania,watu aina ya mleta mada ndo wanaoutrudisha nyuma nchi kama nchi kimaendeleo.
 
Naona waraabu wanazidi kutetewa kwa nguvu, na wanavyo penda tgo 😅 mtaliwa sana vijana
 
Mpuuzi mmoja anadhani rwanda ni kama tanzania,watu aina ya mleta mada ndo wanaoutrudisha nyuma nchi kama nchi kimaendeleo.
Wanaoturudisha nyuma ni wale wanaokabidhi akili zao kwa wafanyabiashara wakubwa wenye malengo yao binafsi wanaodanganya umaa kwamba bandari inataka kuuzwa.

Wanaoturudisha nyuma ni wale wanaokuja na hoja za kuichonganisha serikali ya awamu ya sita na umma wa walipa kodi.
 
Kumuhusisha kagame kama mfano na ujio wake siku za mwisho kabla ya IGA kwenda kwenye kikao Cha Wana ccm waliolewa madaraka na wenye chuki ya wazi dhidi ya hii nchi ni sababu tosha kabisa kukataa huu uwekezaji
 
Ipo video inatembea Youtube inayoonyesha namna serikali ya Rwanda ilivyofungua bandari kavu tayari kwa ajili ya mzigo wa DP World. Tayari kwa ajili ya biashara ya kuweka mzigo unaokuja bandari ya Dar na kwenda Dubai.

Mwarabu alijipanga siku nyingi sana. Hii ni biashara iliyoanza tangu miaka 2010 katikati. Ujenzi wa Reli yetu kwa kiwango cha SGR ni sehemu ya serikali ya JPM kujiweka tayari kwa ajili ya kupitisha mzigo unaotoka DRC na Rwanda na unaoelekea katika nchi hizo ukitokea katika bandari ya Dar.

Zipo tuhuma nyingi sana zinazopandikizwa na wanasiasa wenye kuvizia urais wa 2025 na 2030, wao wanachukulia giza ya ubaguzi dhidi ya wazanzibari kuwa ni nyepesi tu hawajiulizi juu ya madhara ya kudumu ya ubaguzi huo!.

Hawajiulizi juu ya chuki wanayoitengeneza dhidi ya watanzania wenzao kwa kigezo tu cha biashara hii ya DP World.

Iwapo wanasema kuwa Samia ameuza nchi kwa waarabu, vipi kuhusu Paul Kagame wa Rwanda aliyemaliza kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wao, na yeye kauiza Rwanda kwa waarabu?.

Kagame aliyeipigania Rwanda huko msituni akipoteza maelfu ya wanajeshi vitani, anaweza kweli kuja kuiuza nchi yake kwa pesa ya mwarabu?.

Watanzania wenzangu tusikubali kushikiwa akili, na kuchezewa vichwani kama watoto wa miaka mitano. Hakuna mwenye nia wala lengo la kuiuza nchi. Na hao waarabu waache kununua nchi kama Somalia, Sudan na Eritrea zenye utajiri mwingi wa mafuta na madini eti aje kuinunua Tanzania!.

Tupunguze uoga huu ni muda wa kukubali kupokea changamoto mpya za utendaji kazi pale bandarini. Ni muda wa kuondokana na matumizi mengi ya kazi za karatasi zinazochanika na kupotea na kukubaliana na utendaji wa kidigitali wenye tija nyingi ndani ya muda mfupi wa kazi.

Ikiwa Samia anatuuza kwa waarabu ambao ni wajomba zake, vipi kuhusu Kagame na yeye anaiuza Rwanda kwa mwarabu huyo huyo?.

Ni huyu huyu Kagame aliyeisaini mkataba na Arsenal wa mapesa mengi na leo hii dunia nzima inakaribishwa Rwanda kwa maneno tu yanayokuwa mgongoni mwa jezi ya Lionel Messi na Neymar. Kila wanapovaa jezi ya PSG, dunia nzima inakaribishwa Rwanda kupitia matangazo ya umeme yanayokatiza kwenye kioo cha runinga kila mechi ya Arsenal inapochezwa pale Emirates.

Tunahitaji sana marais wenye maono na wanaosimamia kile wanachokiamini mfano wa Paul Kagame, ambaye hatakuwa na muda wa kusikiliza kelele za wajuaji na wajinga wenye kushikiwa akili zao na wanasiasa wenye malengo yao ya kibinafsi.
Weka mezani mkataba wa Kagame ndo tuingie kwenye mjadala. Vinginevyo usitupotezee muda hapa
 
Back
Top Bottom