Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Tokea ramadhani ianze ni mwendo wa kutushambulia hawa jamaa 😁

Qur'an👇🏽

وَلَنْ تَرْضَىٰ عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.
Kwanini Allah mda wote ni ku deal na mayahudi na wakristo, alikuwa hajui duniani Kuna dini nyingine nyingi tu?
 
Ugonjwa wako ni pale uliponiita "shwain", mimi sina ugonjwa kwasababu tangu tuanze mjadala huu naamini sijakutusi au kukuudhi kama nimefanya hivyo nisamehe.

Neno langu la mwisho; let's agree in our disagreement.--- na huo ndio ubinadamu kwani ubinadamu ni zaidi ya utu.
Imeisha hiyo!
 
Kwa hili Rwanda nawapongeza sana, zile kelele za alfajiri zinakera sana.

Hii ni Taharifa ya BBC...

Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo.

Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.

Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu.
===

Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo

"Uamuzi huo ulikiuka haki zetu za kutekeleza imani yetu," anasema Zaina Mukamabano mwenye umri wa miaka 55 ambaye anaishi katika mji mkuu, Kigali.

Anasema ni mara ya kwanza katika maisha yake kuwa hakuna wito wa maombi, au "adhan", asubuhi wakati wa Ramadhani.

Zoezi la kupachika vipaza sauti kwenye minara kwenye misikiti lilianza huko Asia katika miaka ya 1930 na kuenea kote ulimwenguni. Wito tano hutolewa kwa siku, kuwaita waumini kwa sala zao tano za kila siku.

Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu.

"Hatuna furaha ... wakati wa Ramadhani ni adhana ambayo inatuambia kuwa ni wakati wa kuanza kufunga, na sio Waislamu wote nchini Rwanda wana saa za kengele," anasema mkazi mwingine, Nuhu Bihibindi.

Bi Mukamabano anasema serikali ingeweza kuiambia misikiti kupunguza tu sauti, "kama wanavyowaambia mabaa kupunguza sauti ya muziki wao".

“Adhana ni utamaduni wetu, ni imani yetu, kuipiga marufuku ni kuwakera Waislamu, kutokuwa nayo wakati wa Ramadhani kunatia uchungu zaidi,” anasema.

Mkazi mwingine wa Kigali, Issa Karim Mugabo, anasema yeye na wengine sasa wanafikiria kupeleka serikali mahakamani.

Lakini Sheikh Souleiman Mbarushimana, mshauri wa mufti wa Rwanda, na mwanazuoni wa Kiislamu, anasema viongozi wa Kiislamu tayari wamelijadili suala hilo na serikali na kukubaliana juu ya uamuzi huo.

"Waislamu wanasema haki yao ya imani ilikiukwa ... lakini mamlaka imetuambia (Adhana)] imepigwa marufuku kwa manufaa ya wote," Bw Mbarushimana anasema.

"Tulisema kwamba lazima tukubaliane na kuendelea, kwa sababu imani yetu pia inatutaka kuheshimu uamuzi wa mamlaka."

Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
Kule uswizi jamaa mmoja kachoma msaafu,waamiaji kutoka Arabia wamefanya fujo balaa,sasa huku Afrika Kuna kidume kimepiga marufuku adhana,sasa wale ndugu zetu wenye vielele vya hasira kali,tunawakaribisha Rwanda,mfanye fujo,kitakachowapata nyie na ndugu zenu,basi tu,
 
sasa huku Afrika Kuna kidume kimepiga marufuku adhana,sasa wale ndugu zetu wenye vielele vya hasira kali,tunawakaribisha Rwanda,mfanye fujo,kitakachowapata nyie na ndugu zenu,basi tu,

Kwahiyo sifa sio!! Allah hachezelewi bwana,, atapata anachositahili.
 
Ukataze adhana uruhusu wenye mabaa wapige mziki watakavyo,laana hiyo.Adhana ya dakika mbili ina tatizo gani? Adhabu yake ipo na siyo muda mrefu
Dakika mbili wapi. Umesahau baada adhana kuna ile mikwara ya nusu saa. Cjui shuka lako litakuwa sanda yako cjui nini bure kabisa.
 
Hivi kupayuka payuka ovyo kwenye maspika.
Allah mkubwaaaaa
Allah mkubwaaaaa
Allah mkubwaaaaa
Allah mkubwaaaaa
Allah mkubwaaaaa.......
Ndio kuamshana huko ?

Kwanini mnalitaja jina la Allah
Asubuhi mchana na jioni bila sababu ya msingi.
Na

Mnapotaka kulipua Bomu ili kuangamiza halaiki ya watu.

Mnapo jilipua

Mnapotaka kuwachinja Binadamu waliomkejeri Allah au Muhammadi au Qurani.
(eg. mnavyomsaka Salman Rushdie ili mumuchinje kwa jina la Allah baada ya kushindwa kumjibu madai yake kuwa Qurani ni kitabu cha Shetani Ibris Rusifa na Malaika zake Majini )

Mnapo toa adhabu za kukata mikono wezi, kuchinja wazinzi, mashoga na mnao wafumania na wake zenu.

Mnapo andamana kudai matakwa ya Dini ?
NK. ?
Hivi muko timamu kweli ?
 
Waislam wa Rwanda wamuombe Mungu afanye maamuzi yasiyonashaka kwa yeyote aliyetoa mada,aliyepirtsha, na aliyetoa amri.Insh Allah.
 
Mada kama hii ya "Adhana" ilimfukuzisha kazi Dada mmoja maarufu tu huko Twitter baada ya kukaa kwenye kipindi cha Televisheni alichokua akiendesha aka support hoja ya 'Mgeni Mualikwa' baada ya Mgeni kusema kwamba 'Adhana' ni Noise pollution!.

Kipindi kikaisha saa 07:50, sijui wale jamaa wa Bakwata walitokea wapi..wakatwanga simu moja kwa 'Mmiliki' ...ndani ya Dakika chache walimiminika wale jamaa kwenye viunga vya studio wakitaka ufafanuzi wa hoja zilizoungwa mkono na 'Presenter'.

Flashback hiyo! Zamani kidogo imetokea..na Huyo Dada alirudi kwenye runinga baada kama ya 7 yrs hivi! 😂 😂 😂 Mada korofi sana hizi!
Hii inatisha, unaweza kuacha kuchangia.

1930 kwenye spika. Kwanini tusikubali 2022 kwenye Twita?

Tatizo ni kuwa sheria inasema kwenye "maeneo karibu na makazi" lakini humu tunaeza pindisha na kusema "amepiga marufuku adhana alfajiri" yenye kuleta nadharia ya kuwa Nchini kote Alfajiri!

Nani mchochezi?
Nafikiri mleta mada naye ndiye mkorofi na wala sio Sheria.
 
Kwa hili Rwanda nawapongeza sana, zile kelele za alfajiri zinakera sana.

Hii ni Taharifa ya BBC...

Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo.

Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.

Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu.
===

Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo

Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.

"Uamuzi huo ulikiuka haki zetu za kutekeleza imani yetu," anasema Zaina Mukamabano mwenye umri wa miaka 55 ambaye anaishi katika mji mkuu, Kigali.

Anasema ni mara ya kwanza katika maisha yake kuwa hakuna wito wa maombi, au "adhan", asubuhi wakati wa Ramadhani.

Zoezi la kupachika vipaza sauti kwenye minara kwenye misikiti lilianza huko Asia katika miaka ya 1930 na kuenea kote ulimwenguni. Wito tano hutolewa kwa siku, kuwaita waumini kwa sala zao tano za kila siku.

Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu.

"Hatuna furaha ... wakati wa Ramadhani ni adhana ambayo inatuambia kuwa ni wakati wa kuanza kufunga, na sio Waislamu wote nchini Rwanda wana saa za kengele," anasema mkazi mwingine, Nuhu Bihibindi.

Bi Mukamabano anasema serikali ingeweza kuiambia misikiti kupunguza tu sauti, "kama wanavyowaambia mabaa kupunguza sauti ya muziki wao".

“Adhana ni utamaduni wetu, ni imani yetu, kuipiga marufuku ni kuwakera Waislamu, kutokuwa nayo wakati wa Ramadhani kunatia uchungu zaidi,” anasema.

Mkazi mwingine wa Kigali, Issa Karim Mugabo, anasema yeye na wengine sasa wanafikiria kupeleka serikali mahakamani.

Lakini Sheikh Souleiman Mbarushimana, mshauri wa mufti wa Rwanda, na mwanazuoni wa Kiislamu, anasema viongozi wa Kiislamu tayari wamelijadili suala hilo na serikali na kukubaliana juu ya uamuzi huo.

"Waislamu wanasema haki yao ya imani ilikiukwa ... lakini mamlaka imetuambia (Adhana)] imepigwa marufuku kwa manufaa ya wote," Bw Mbarushimana anasema.

"Tulisema kwamba lazima tukubaliane na kuendelea, kwa sababu imani yetu pia inatutaka kuheshimu uamuzi wa mamlaka."

Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
Mungu alibariki taifa teule la Rwanda, kwa kweli huu upuuzi wa kuamsha watu usiku eti waache kulala waende kusali ni ujinga uliopitiliza. Seriously, utawalazimishaje watu waache kulala waende kusali, hivi kweli Mungu anayataka haya? Watanzania tusiwe wajinga kihivi, Mungu katupa alili tuzitumie si tu kuendeshwa kwa matakwa ya watu ili wapate wali wa bure pampja na tende kwa ajili ya kulazimisha watu waamke. Huu ni ujinga uliopitiliza. Homgera Rais Kagame kwa kusimamia haki.
 
Na bahati mbaya kweli kweli nimejenga kakibanda kangu sehemu na sina furaha kabisaa kwa kelele

Nyuma yangu kuna msikiti halafu sijui kwanini huwa hawaweki hata spika za kisasa zenye mlio usio umiza sana kwa makelele
Vispika vile wakianza Adhana hiyo alfajiri utadhani wameviweka dirishani kwangu nikele balaa

Kulia kwangu kuna kanisa la walojole aisee
Yaani hawa viumbe jumapili wanapiga “masebene ya Yesu” ni hatari, maspika yanadunda upo nyumbani kwako lakini utadhani upo kwenye tamasha la papa mpao

Kwakweli kuna haja ya kuwadhibiti hawa watu kwakweli wanakera sana
 
Adhana iliyotungwa na Umar , inahusika vipi na Allah kutoa thawabu ?
Adhana ni wito uliofaradhishwa na Mwenyezi Mungu katika Qur'an (Soma Qur'an 62:9) ndio maana maswahaba wakatumia Qiyyaas kutafuta namna ya kuitana na Mtume s.a.w naye akaridhia.Mtume s.a.w hafanyi kwa matamanio yake bali kwa uongozi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Waislamu kufuata alichoridhia Mtume ni wajibu na kutokufanya hivyo ni uasi.
 
Dakika mbili wapi. Umesahau baada adhana kuna ile mikwara ya nusu saa. Cjui shuka lako litakuwa sanda yako cjui nini bure kabisa.
Wanaofanya hiyo mikwara hata sisi hatuwakubali.Hao pia tunawapiga vita sisi wenyewe.Lakini kwenye adhana ikibidi tutapigana na nyinyi.
 
Adhana ni wito uliofaradhishwa na Mwenyezi Mungu katika Qur'an (Soma Qur'an 62:9) ndio maana maswahaba wakatumia Qiyyaas kutafuta namna ya kuitana na Mtume s.a.w naye akaridhia.Mtume s.a.w hafanyi kwa matamanio yake bali kwa uongozi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Waislamu kufuata alichoridhia Mtume ni wajibu na kutokufanya hivyo ni uasi.
Mtunzi wa adhana ni Umar , Allah ka copy kutoka kwake, sio adhana tu Umar ana verse kazitunga kwenye Koran
 
Mimi ni Uislam namuunga mkono Kagame kwa hili la zuio..

Uislam ni dini ya hekima,dini iliyojaa busara,lakini kuna baadhi ya Waislam wanazidisha mambo na kuifanya hii dini iwee dini ya kelele

Sala ni moja ya nguzo za kiislam,ni njia moja ya kuwa karibu na Mungu,sasa kuna misikiti mingine utasikia Imam anasalisha na yale yote anayosalisha unayasikia kwenye vipaza sauti

Sheikh anasoma sura na mambo mingine, yanasikika nje kwa kutumia vipaza sauti...bila ya kujali jamii iliyomzunguka,wagonjwa,wazee,watoto wadogo nk

Huu utamaduni wa kutumia vipaza sauti kwenye misikiti umeanzia mashariki ya mbali na sisi huku tukaiga..

Bora Tanzania nayo iige mfano wa Rwanda,turudi kama zamani,Adhana zote ziwe za sauti ya muadhini bila ya kutumia Vipaza sauti
Ndio uislamu ni dini ya hekma, lakini hukmu zake huwa haziendeshwi kwa rai namna hiyo.

Ulichosema ambacho wanafanya baadhi ya waadhini/mashekhe sio sahihi, maana wanazidisha, pia walivyofanya Rwanda nacho sio sahihi maana wamekataza kabisa.

Kinachatakiwa ni kati na kati

Kama kuna palipo zaidi, basi papunguzwe, lakini sio kukataza kabisa, kufanya hivyo lengo litakuwa halifikiwi.
 
Hivi wakati was mtume maspika yalikuwepo? Kama hayakuwepo waislam walitumia Nini tuanzie hapo kuhoji uhalali wa adhana ya maspika

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wakati wa mtume hata mabusati hayakuwepo, kwa hiyo unataka kusemaje? tuswali kwenye michanga.

Hata cement haikuwepo wakati huo, vipi tujenge misikiti ya makuti?

Uislamu haupo hivyo.
 
Adhana ilibuniwa na mtu anaitwa Umar wala sio Muhammad, waislamu walikuwa hawana jinsi ya kuitana kwenda kwenye salat , wakajadili waige wakristo kutumia kengele au waige wayahudi kutumia tarumbeta , Umar ndie akaja na idea ya adhana Muhammad akadakia hapo hapo kumuamrisha mtumwa anaitwa Bilal Aite watu , kumbuka ilikuwa anaanza asubuhi kombora ndio maana wakamuweka mtumwa

Hadith
"When the Muslims arrived in AI-Madinah, they used to assemble for the Salat, and guess the time for it there was no one who called for it (the prayer). One day they discussed that and some of them said that they should use a bell like the bell the Christians use. Others said they should use a trumpet like the horn the Jews use. But Umar [bin Al-Khattab] said: 'Wouldn't it better if we had a man call for the prayer?'" He said: "So Muhammad said: 'O Bilal! Stand up and call for the Salat.'" Jami` at-Tirmidhi 190
Kasome vizuri adhana haijabuniwa.

Kwa maelezo ya hadhithi inaonyesha kabisa kuwa, kulikuwa na haja ya kupatikana namna ya kuwaita watu katika swala, ndio maana zilitolewa rai tofauti.

Sasa unaposema mtu fulani alibuni, sijui unakusaidia nini? adhana yenyewe au uwepo wa adhana?

Na kama ni adhana yenyewe (maneno yake) basi kasome vizuri maana haikubuniwa, ili kuja kwa maneno yake kama ilivyo kasome ilikujaje.
 
Back
Top Bottom