S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

Aombe mapitio ili mahakama iamuru waliokuwa wamiliki wa awali ambao wamerudishiwa umiliki wao wamlipe gharama za jengo au aruhusiwe kulivunja jengo lake ili wao wabaki na kiwanja chao.
Awajengee nyumba ya mil 400 aliyo ibomoa na kujenga hilo ghorofa. Njia halali na raisi ni kukaa nao mezani apewe hisa awe mmoja wa wamiliki. Sema hapo kuna kugeulana mbeleni vifo vya ghafla kuibiana nyaraka hila za kibiashara kurubuni wana hisa kuuza hisa zao n.k vinaweza kutamalaki😎😎😎
 
Mahakama hizohizo zìnakosea. Km siyo Mahakama ya Rufani, bado chochote kinaweza tokea
 
Jamaa atoe jengo lake na amwachie kiwanja ndugu pazi na kesi iishie hapo
Ni kweli, wao wamemwaga ugali, yeye amwage mboga ili wite wakose, ingawa hapo panawaka moto, hawezi kutia mguu tena!
 
Haki huchelewa tu. Huyo awe mpole awapigie magoti awape cash na hisa 50% maisha yaendelee.
 
Tatu alikula mchongo na mpangaji wake kazuba (pengine labda hakuridhika na mgao alioupata) baada ya nyumba kuuzwa mara ya kwanza kwa mwekezaji ambae hakutajwa.

Wakasuka dili la kimkakati na wakamtafuta mteja wao ambae sasa ni S.H. Amon, ngoma ikaenda mahakamani na kabla ya mapingamizi ga nduguze Tatu kusikilizwa Mahakama Kuu ikatoa hujumu ikim-favor Tatu na wadau wake!

Mnada ukafanyika nyumba ikauzwa tena kwa mara nyingine kwa Tsh. 105 million, alieshinda ni S.H. Amon.

je hio 105 alipewa nani? Wanafamilia wote?

Kama pesa walipewa wanafamilia wote na kazuba nae akafaidi kupitia malalamiko yake, naweza kusema bwana Sauli aliingizwa mjini na watoto wa kariakoo!
 
Amoni tulia tu uwe mpole, unanunua vipi nyumba bila kushirikisha wanafamilia wote. Amoni we nenda kaidai fidia mahakama ikulipe kwa kukuingiza mkenge kwa kukosea kutoa hukumu. Pili ushavuna sana, waachie wenyewe. Wao ndio wa kwanza kuja mjini wakati wewe unashindia mbalaga Mbeya
 
Sijui na sisi tuliouziwa mashamba ya ukoo itakuwaje?
 
Michezo ya kupora watu viwanja vyao ilikuwepo Sana nyuma kabla ya lukuvi angalau na jiwe watu waliogopa. Zamani kiwanja chako unakuta mtu kajenga nyumba kibabe ukienda mahakamani hakimu anaangalia pesa tu na siyo haki
 
Kuna jengo limeungua moto mara kadhaa na wanunuzi kadhaa wamefariki punde baada ya kulinunua, lipo mtaa wa uhindini Dodoma linapakana na Studio za TBC Dodoma, unaweza kujaribu bahati yako mkuu. Nenda ukathubutu
 

Mkuu kwanza kabla Bank hawajakupa mkopo ni lazima uwe na hati ya kiwanja na process zingine kibao..

Na wanapofanya mnada kuna process nyingi wanapitia ili kuthibitisha kuwa wewe umeshindwa mkataba mliokubaliana...

Wanasheria pia wanahusika sana katika hio michakato yote... sio Jambo rahisi sana kutokea... labda kama lilihusisha Rushwa kukwepa some Procedure
 
Wakuu habari. Hiyo hoja ya wanahisa 6/7 kutokushirikishwa katika uuzwaji imenipa darasa kubwa sana, hili inabidi iwe angalizo kwetu sote.
Ukinunua nyumba ya familia ni lazima ridhaa ya wote kimaandishi iwepo.
Hata ukinunua nyumba au kiwanja cha wanandoa labda ukimshirikisha mmoja tu bila mwingine kisheria imekula kwako umetapeliwa ni lzm wanandoa wote watie wino,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…