S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

... benki hawawezi kuendesha mnada bila idhini ya mahakama nadhani. Lazima shauri lipelekewe mahakamani kwamba umeshindwa kulipa mkopo wao kwa mujibu wa mkataba (umekiuka mkataba) then mahakama itatoa hukumu ya nyumba yako kuuzwa. So, mnunuzi atakuwa ameinunua kwa utaratibu sahihi kuja kumgeuka itakuwa ngumu sana.
Asante sana. Nadhani uko sahihi.
 
Nje ya mada, kwa wenye uelewa: Hivi entity kama benki ikiendesha mnada wa nyumba ya mtu aliyeshindwa kulipa deni na mahakama baadae ikasema mnada ulifanyika ndivyo sivyo, hivyo nyumba inatakiwa irudi kwa wenyewe, mimi mnunuzi nitapoteza? Gharama zangu nani atalipa na hasa kama nimeshaendeleza?
Hata kama utalipwa hela utayopewa ni sawa na hasara,miaka 20 ni mingi inflation lazima ile kwako.
 
Umekosea kuripoti, hajarudishiwa nyumba ni amerudishiwa kiwanja, hivyo SH Amin, yuko free kuyachukua majengo yake, hivyo jamaa kubaki na kiwanja chake kirudishwe ile nyumba aliyoinunua.
P


In the final result and for the reasons as aforesaid, we allow the appeal with costs to the extent as afore stated. We quash and set aside the judgment and decree of the trial court and declare the appellants as the rightful owners of the suit property and all developments thereon to the extent of their 6/7 shares reflected in exhibit P2.DATED at DAR ES SALAAM this 13th day of A pril, 2022.M. A. KWARIKO.JUSTICE OF APPEALI. J. MAIGEThe judgment delivered on 13th day of April, 2022 in the presence of Ms. Subira Omary, learned counsel for the appellants and Ms. Sia Ngowi, learned counsel for the 1st and 2nd respondents, 3rd and 4th present unrepresented and Mr. Gallus Lupogo, learned State Attorney for the third party, is hereby certified as true copy of the original.JUSTICE OF APPEALA. M. MWAMPASHI JUSTICE OF APPEALA. L. KALEGEYA ^ DEPUTY REGISTRAR ^ COURT OF

Source READ THE FULL JUDGEMENT : Hamisi Bushiri Pazi & Others vs Saul Henry Amon & Others (Civil Appeal 166 of 2019) [2022] TZCA 186 (13 April 2022); | Tanzlii
 
Lessons Learned:
Whenever you are buying a property through an auction kwa sababu ya deni la benki au mgogoro wowote wa madeni, lazima uwe EXTREMELY CAREFUL

Most of the time hawa court brokers wanakosea sana kwenye utaratibu wa kufanya minada hii. Kwanza, wanajua wanunuzi wanaopenda property za design hii, na pia wana tendency ya kuwaonea sana wamiliki halali wa property.

Sheria inamruhusu dalali kuuza property mpaka kwa asilimia 25% ya thamani ya jengo. Manake nini? Jengo la billioni moja linaweza kuuzwa kwa hadi shilingi mil 250 na hii ni Sawa kabisa. So kama deni lako tuseme mil 500, property yako yenye thamani ya bil 1 inauzwa kwa hasara ya zaidi ya asilimia 50 na bado unakuwa na deni limebakia juu yake. This is very unfair on the face of it. Na watu wengi wameumia kwa staili hii.
 
Haki huwa inapotea
Mungu ni mwema sana.
Hivi ndivyo haki inavyokua haipotea, ingawa inaweza tu ikacheleweshwa.
Miaka kuanzia ya 2014 kurudi nyumba, wafanya biashara/wanasiasa walionekana kua wenye mguvu kuliko hata serikali, na hii ndio matokeo ya sheria zilizo pindishwa na wenye fedha/mamlaka enzi hizo
 
Aombe mapitio ili mahakama iamuru waliokuwa wamiliki wa awali ambao wamerudishiwa umiliki wao wamlipe gharama za jengo au aruhusiwe kulivunja jengo lake ili wao wabaki na kiwanja chao.
Yeye alikosea akanunua nyumba makusudi akijua kuna shauri mahakamani. Pia Ile aliyoivunja na Mali zao zilizokuwa ndani Kwa miaka ishirini fidia yake ni ipi?
 
Kuna jamaa alitaka kuniuzia Hilo jengo alisema 6.5b mie namwambia achukue 4 akakataa. Tukaishia Hapo. Afadhali ukosefu wa hela wangu uliniokoa na ambavyo sipendi kesi
Nilipanga kusoma bila kuchangia huu uzi mpaka nilivyoshtuka mtu mwenye B's akichangia Jf

Kumbe tuna watu wazito sana humu[emoji848][emoji848]
 
Binafsi huwa sio muumini wa kununua mali za mnada, hazina baraka aisee kuna nyumba ilinunuliwa kwa bei chee baada ya bank kupiga mbada matokeo hiyo nyumba mpaka leo haikai mtu aliyenunua ameshindwa kukaa wanaopanga wanaondoka bila kumaliza kodi
Nadhani hii ni imani tu. Watu wanaoshindwa kulipa madeni wamekuwa wanavumisha hivyo ili nyumba zao zikose wanunuzi. Mnunuaji huna kosa lolote kama taratibu zimefuatwa. BTW siku za nyuma nilikuwa naulizia members hapa kama kuna mtu yeyote anayejua nyumba yenye mauzauza yoyote kama majini nk naomba awasiliane na mimi ili nikalala kwenye hiyo nyumba lakini sikupata mrejesho. Nadhani hukuona hilo ombi.
 
Binafsi huwa sio muumini wa kununua mali za mnada, hazina baraka aisee kuna nyumba ilinunuliwa kwa bei chee baada ya bank kupiga mbada matokeo hiyo nyumba mpaka leo haikai mtu aliyenunua ameshindwa kukaa wanaopanga wanaondoka bila kumaliza kodi
Hebu tuonyeshane hizi nyumba.

Humu stori za kuna nyumba ya mnada haikaliki ni nyingi sana.

Tuonyeshane ili tukapange
 
Aombe mapitio ili mahakama iamuru waliokuwa wamiliki wa awali ambao wamerudishiwa umiliki wao wamlipe gharama za jengo au aruhusiwe kulivunja jengo lake ili wao wabaki na kiwanja chao.
Hiyo haipo kisheria, yaani mahakama ya rufani imeshaamua, hakuna mapitio tena maana hadi kutoa hiyo hukumu mahakama ilishapitia.
 
Back
Top Bottom