S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

Mkuu kwanza kabla Bank hawajakupa mkopo ni lazima uwe na hati ya kiwanja na process zingine kibao..

Na wanapofanya mnada kuna process nyingi wanapitia ili kuthibitisha kuwa wewe umeshindwa mkataba mliokubaliana...

Wanasheria pia wanahusika sana katika hio michakato yote... sio Jambo rahisi sana kutokea... labda kama lilihusisha Rushwa kukwepa some Procedure
Asante sana
 
Milioni 105 angeweza kupata kiwanja njia ya Tegeta na kujenga kwa nafasi, mji unapanuka. Pole zake.
umesoma habari hiyo vizuri mkuu milioon 105 ya mwaka 2001 kariakoo haiwezi kuwa sawa na ya milion 105 ya sasa hapo hapo kariakoo hata huko tegeta ulikosema hapawezi kuwa sawa kibiashara na kariakoo
 
Akate rufaa wapi wakati mahakama ya Rufaa ndio kubwa. Ni sawa na ugonjwa umeshindikana Muhimbili unambeba mgonjwa kumpeleka hospitali ya Mwananyamala
Bado mara 2 hapo hapo rufaa.....marejeo.ikishindikana anaomba full benchi majaji5....maana sasa wanakaa 3
 
Sauli ana option mbili baada ya rufaa kufungwa.
1.Awaite wahusika wabargain awape pesa watakayo. Au pesa na nyumba hata tatu tatu ya kuishi na ya kupanga
2.Aondoe jengo lake awaachie uwanja wao.
 
Hawezi kukubali kirahisi kuachia huo mjengo atakata rufaa tu
 
Binafsi huwa sio muumini wa kununua mali za mnada, hazina baraka aisee kuna nyumba ilinunuliwa kwa bei chee baada ya bank kupiga mbada matokeo hiyo nyumba mpaka leo haikai mtu aliyenunua ameshindwa kukaa wanaopanga wanaondoka bila kumaliza kodi
Mnada ni dhuluma sababu mmiliki ajakunjua nafsi.Hata magari sio poa uchelewi kula mzinga
 
Nje ya mada, kwa wenye uelewa: Hivi entity kama benki ikiendesha mnada wa nyumba ya mtu aliyeshindwa kulipa deni na mahakama baadae ikasema mnada ulifanyika ndivyo sivyo, hivyo nyumba inatakiwa irudi kwa wenyewe, mimi mnunuzi nitapoteza? Gharama zangu nani atalipa na hasa kama nimeshaendeleza?
Sheria zetu zina mapungufu sana
 
Sisi nyumba yetu ilibomolewa, nakumbuka nipo darasa la nne, ninakaanga samaki wakaja na maaskari na likijiko 🤣🤣 lakini walipata shida sana kututoa uwanja uligeuka wa vita kama DRC vile.
Ilivyouzwa ikanunuliwa na mbunge fulani iliuzwa bila kushirikisha ukoo mzima kama mjuavyo nyumba za kariakoo ni za urithi, ni mtu mmoja mwenye tamaa aliyeuza (baba yao mdogo wakina mama) maana babu yetu na babu wengine walikwishafariki.
Mbunge akaiuza kwa mwarabu wameuziana weeeeee lakini ajabu hadi leo hawajapandisha, ujenzi haujaisha ghorofa liko kama gofu(nadhani mnunuzi wa mwisho alitonywa kuwa wenye eneo siku wakiibuka ni hatari maana wenyewe kwa wenyewe walikuwa wanakatana mapanga humo ndani na hadi leo kesi iko mahakamani)
Kuna mdogo wangu huwa anasema nitaifufua kesi tutachukua ghorofa letu hawatoamini.
Yaani ni ile nikipita mtaa wa uhuru siku zote roho lazima idunde na lazima nichungulie dirishani na lazima niliyenaye nimuambie kwetu pale 😭😭😭

Enzi za Makonda tulipigwa simu na bi mkubwa mmoja tukampe company eti atusaidie tupate haki 🤣🤣🤣🤣 maskini ya Mungu mama zetu walikusanyika na foleni ile ya makonda(hawakupata msaada wowote)
Anyway hizo ndo nyumba za kariakoo zilivyo.
Na mara nyingi sababu kubwa ni kugeukana wanandugu, tamaa na dhulma baina ya wanandugu.

Hongera zao wakina pazi wameweza kupambana miaka yote, hiyo familia ina umoja na wanapendana.

Nadhani na sisi wazazi wetu wangekuwa walau wana umoja, wanapendana wangerudishiwa eneo lao.
🤣🤣🤣🤣🤣 ila si tatizo lao ni kwa sababu wana asili ya vita.
 
Back
Top Bottom