Sisi nyumba yetu ilibomolewa, nakumbuka nipo darasa la nne, ninakaanga samaki wakaja na maaskari na likijiko 🤣🤣 lakini walipata shida sana kututoa uwanja uligeuka wa vita kama DRC vile.
Ilivyouzwa ikanunuliwa na mbunge fulani iliuzwa bila kushirikisha ukoo mzima kama mjuavyo nyumba za kariakoo ni za urithi, ni mtu mmoja mwenye tamaa aliyeuza (baba yao mdogo wakina mama) maana babu yetu na babu wengine walikwishafariki.
Mbunge akaiuza kwa mwarabu wameuziana weeeeee lakini ajabu hadi leo hawajapandisha, ujenzi haujaisha ghorofa liko kama gofu(nadhani mnunuzi wa mwisho alitonywa kuwa wenye eneo siku wakiibuka ni hatari maana wenyewe kwa wenyewe walikuwa wanakatana mapanga humo ndani na hadi leo kesi iko mahakamani)
Kuna mdogo wangu huwa anasema nitaifufua kesi tutachukua ghorofa letu hawatoamini.
Yaani ni ile nikipita mtaa wa uhuru siku zote roho lazima idunde na lazima nichungulie dirishani na lazima niliyenaye nimuambie kwetu pale 😭😭😭
Enzi za Makonda tulipigwa simu na bi mkubwa mmoja tukampe company eti atusaidie tupate haki 🤣🤣🤣🤣 maskini ya Mungu mama zetu walikusanyika na foleni ile ya makonda(hawakupata msaada wowote)
Anyway hizo ndo nyumba za kariakoo zilivyo.
Na mara nyingi sababu kubwa ni kugeukana wanandugu, tamaa na dhulma baina ya wanandugu.
Hongera zao wakina pazi wameweza kupambana miaka yote, hiyo familia ina umoja na wanapendana.
Nadhani na sisi wazazi wetu wangekuwa walau wana umoja, wanapendana wangerudishiwa eneo lao.
🤣🤣🤣🤣🤣 ila si tatizo lao ni kwa sababu wana asili ya vita.