Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,577
Reaction score
4,637
Salamu kwenu ndugu.

Ningeomba uzi huu MODS wanisaidie kuusambaza kwa wenye mamlaka.

Sasa hivi kuna kamtindo kameshamiri kwa shule za msingi za serikali kuwachukua wanafunzi na kukaa nao kuanzia saa 12 Alfajr hadi saa 12 jioni... Kwa kisingizio cha kusoma na masomo kuzidi kasi.

Hivi hasa ni nani kawadanganya walimu hawa kuwa MTOTO atafaulu kwa kuwa na muda mrefu wa kusoma?

Hata hizo shule zinazoongoza kwa ufaulu kama ST. FRANCIS ukiangalia kikubwa wanachokisisitiza ni NIDHAMU, Kuanzia kwa walimu mpaka kwa wanafunzi...

Wanazingatia sana ratiba na TEACHING MANUAL(Kama sijakosea) YAANI kila kitu kina wakati wake...sio kwamba wanasoma muda woteee...

Yaani ukiangalia ratiba zao, kuna muda wa kusoma, muda wa kucheza, muda wa kusali na muda wa kupumzika na kulala. NA WANAFANIKIWA.

ILA hizi shule zetu sasa za SERIKALI...wanafanya hivi miaka nenda miaka rudi lakini bado hatujaona hasa nini wamepakipata kwamba walikuwa wanakitafuta.

Yaani kuanzia Saa 12 ASUBUHI hadi saa 12 Jioni KILA SIKU, JUMATATU MPAKA JUMAMOSI Vilevile Kasoro JUMAPILI TU(na KWANINI IWE JUMAPILI TU? Tuseme UDINI ama)...

MUHULA MZIMA WA MIEZI 12...Yaani na LIKIZO VILEVILE wanawaita watoto wasiende likizo nyumbani(na hii tunawashukuru MAWAZIRI UMMY na NDALICHAKO waliliingilia kati suala hili kwa likizo hii).

SWALI LANGU NI;

Je Walimu hawa wanatafuta nini? LENGO LAO NI NINI?

Kama lengo ni kufaulisha, WANATAKA WAFAULISHEJE KWA MTINDO HUU...Mbona matokeo ni yale yale?

Mfano kuna shule iko jirani hapa...MWAKA JANA WAMEFANYA UTARATIBU HUO...Lakini wametoa WANAFUNZI WOTE WAMEENDA SHULE YA KATA ILIYO KARIBU...Hakuna hata mmoja alienda KIPAJI MAALUM...

Ina maana hawafanyi tathmini juu ya mbinu wanazotumia?

Mimi kwa Upande wangu nimeona yafuatayo;-

1. Hii ni dalili ya KUTOKUWAJIBIKA IPASAVYO na UVIVU kwa walimu wetu hawa, Kama hukuweza kufundisha na kumaliza at a given time frame WEWE NI MZEMBE, Hata ukipewa muda mwingi iweje you wont succeed.

2. Ukiwauliza kwanini hivi, watakwambia HIVI NDIVYO TULIVYOKUBALIANA NA WAZAZI KWENYE MKUTANO WA WAZAZI(Huku kwenye mkutano ndipo wanakotumia kupitisha vimichango vyao kwa kisingizio tumekubaliana).

Siri ni hivi...WAZAZI wa zama hizi ni wavivu na hawataki kulibeba jukumu lao la malezi...kwahiyo kukaa na mtoto siku nzima kwao ni AFUENI ya malezi, kwahiyo wazazi na walimu wana malengo tofauti kwa maslahi yao binafsi.

MATOKEO YAKE NI NINI?

1. Mtoto kukosa elimu ya muhimu ya uendeshaji wa maisha yake akiwa mtaani mbali na shule. Watoto wanashinda siku nzima kusoma JIOGRAFIA, HISTORIA YA KINA LIVINGSTONE, HISABATI ZA KKS NA KDS, SAYANSI YA KUMSOMA PANZI...Wanapomaliza masomo na kurudi mtaani, SERIKALI inakuachia mzigo wako mwenyewe TOTO LIMEKUWA JINGA, hata namna ya kuchomeka BULB Ili iwake ATAMWITA FUNDI amfanyie...huku AKILILIA AJIRA YA SERIKALI ili aweze kuifanyia kazi(kuapply) elimu yake ya SAYANSI YA KUMSOMA PANZI na sehemu zake katika maisha yake, wapi aapply HESABU ZA KKS na KDS kwenye maisha...hakuna.

Na sasa hivi sijui kama hata lile somo la STADI ZA KAZI likifundishwa...maana sioni hata watoto wakichonga mifagio ya chelewa kupeleka shuleni...labda ingesaidia...

BILA SHAKA hakuna asiyekubali kuwa kumekithiri yale maneno ya MJIAJIRI kutoka kwa viongozi...hii inathibitisha elimu hii INAYOTOLEWA TOTALLY FAILED

2. NAAMINI TUTAKUBALIANA WOTE KUWA...HAKUNA MAHALA PANAPOHARIBU MAADILI NA TABIA YA MTOTO KAMA SHULENI...

Shuleni hasa za serikali, WANAJAZANA WATOTO WA AINA TOFAUTI WALIOTOKA KWENYE FAMILIA TOFAUTI WENYE MALEZI TOFAUTI NA TABIA TOFAUTI...

Na kwa vile walimu wale wa serikali hawapo pale kurekebisha tabia za mtoto wa mtu...zaidi ya kuhakikisha AMEFUNDISHA ZAKE HESABU ZAKE KUTAFUTA "X"...Huyo mtoto wa mtu hamuhusu na tabia zake mbaya ..

Mwisho wa siku WATOTO wenye tabia mbaya watawaathiri watoto wenye malezi mazuri ..mwisho wa siku wote wanaharibika...

Tujiulize hizi MIMBA ZA SHULENI zimefuata nini huko? Kama shuleni ni sehemu salama tena...?

NI NINI NACHOOMBA KWA WENYE MAMLAKA.

1. Mamlaka ziratibu utoaji wa elimu kwa manufaa mema ya mtoto wa kitanzania ..badala ya kustick kwenye elimu ambayo tayari ina KILA DALILI ZA KUFAIL. Badilisheni sylabus...muda wa kusoma KKS na KDS na ALGEBRA, kusoma PANZI tuutumie kufundisha watoto mazingira halisi ya kuishi maisha yao.

2. GAWENI MUDA WENU HATA MPAKA SAA 6 AU SAA 8 INATOSHA...ILI MTOTO ARUDI MTAANI JAMII IMFUNDISHE "ELIMU MTAA".

3. Haya maadili ambayo kila kukicha viongozi mnalalamikia viongozi wa dini wayatengeneze...unadhani uharibifu wake...unaanzia wapi? Unaanzia kwenu shuleni...mtoto mnakaa nae akiwa mdogo kutwa nzima...akiharibika mnamrudisha mtaani...huyo kiongozi wa dini atatengeneza nini sasa? SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI.

4. Kwa mustakabali wa kimaadili, Wekeni sera ya KULAZIMISHA KILA MZAZI KUHAKIKISHA Mtoto wake anapata elimu ya dini yake kwanza akiwa mdogo kama elimu ya awali. Na anapoanza elimu ya msingi KUHAKIKISHA ule muda baada ya saa 8 kila mtoto aruhusiwe arudi nyumbani na kuhudhuria mafunzo ya dini yake kwa lazima...hii italinda maadili ya jamii.

SERIKALI MSIKAE NA WATOTO KUTWA NZIMA, TUACHIENI NA SISI JAMII TUITENGENEZE JAMII TUITAKAYO. KWA MWALIMU BORA NA ELIMU BORA...MASAA 8 KWA SIKU YANATOSHA KUFUNDISHA NA ELIMU IKAWA NA MANUFAA...KULIKO KUSHINDA NAO SIKU NZIMA.

INATOSHA KWA LEO.
 
Ni kwa sababu za tuition na remedial. Walimu nao wanakula kwa urefu wa kamba zao. Kuna shule wazazi wanatozwa fedha kila wiki kwa ajili huyo. Serikali inawadanganya Kuna Elimu ya Bure?!
 
Umeeleza vizuri sana tatizo ni waalimu kunufaika na fedha wanazowatoza watoto kwa kinachoitwa tuisheni kwa hiyo sio kweli eti Wana shida ya kufaulisha Bali kujiongezea kipato. Hawajali watoto kukaa na njaa siku zote mradi wao wanaingiza hela na wananunua chakula. Mh Waziri wa Elimu na wa Tamisemi chukueni hatua watoto wetu wanadumazwa na njaa za kutwa nzima kwa tamaa ya waalimu wenu waliokosa ubunifu wa njia mbadala za kujiingizia kipato na kugeuza wanafunzi wao vitega uchumi vyao
 
Bora SAA 12 jioni, nenda sekondari ya KABINDI(RUNAZI) iliyoko BIHARAMULO wanafunzi wanasoma vipindi vya kawaida mchana alafu wanarudi jioni hadi SAA tatu usiku.
Wakiachiwa wanazagaa mitaani hadi SAA NNE usiku.
Yaani ni hatari hata kwa watoto wa kike na wale wanaotoka mbali hasa kipindi hiki cha mvua.
 
Bora SAA 12 jioni, nenda sekondari ya KABINDI(RUNAZI) iliyoko BIHARAMULO wanafunzi wanasoma vipindi vya kawaida mchana alafu wanarudi jioni hadi SAA tatu usiku.
Wakiachiwa wanazagaa mitaani hadi SAA NNE usiku.
Yaani ni hatari hata kwa watoto wa kike na wale wanaotoka mbali hasa kipindi hiki cha mvua.
Sasa hapo mimba zinakosekanaje? Hawa ndio wanatuharibia jamii ijayo...
 
Umeeleza vizuri sana tatizo ni waalimu kunufaika na fedha wanazowatoza watoto kwa kinachoitwa tuisheni kwa hiyo sio kweli eti Wana shida ya kufaulisha Bali kujiongezea kipato. Hawajali watoto kukaa na njaa siku zote mradi wao wanaingiza hela na wananunua chakula. Mh Waziri wa Elimu na wa Tamisemi chukueni hatua watoto wetu wanadumazwa na njaa za kutwa nzima kwa tamaa ya waalimu wenu waliokosa ubunifu wa njia mbadala za kujiingizia kipato na kugeuza wanafunzi wao vitega uchumi vyao
Hii ni tabu...
 
Sasa hapo mimba zinakosekanaje? Hawa ndio wanatuharibia jamii ijayo...
Hapana mimba zitakuepo hata wakirudi saa saba.

Muhimu ni kuwa hakuna elimu ya kusoma masaa 12 huko shule.

Mtoto anatakiwa ajifunze mambo mbalimbali,kulala,kucheza na wenzie n.k

Mtoto wa siku hizi anasoma masaa mengi shuleni kuliko mwajiri anavyokaa masaa mengi kazini

Kwa kifupi watoto nao wamegeuka waajiriwa siku hizi

maana wazqzi wao wanawahi kurudi kazini lakini wo bado
 
Ungekuwa mwalimu pengine hata ww ungekuwa hivyo.

Sababu kubwa ni;

1. Kulinda kibarua cha mwalimu(shule binafsi hapa); Elimu ni biashara, ukifelisha, mkurugenzi hana huruma na ww, so lazima utumie kila njia kuhakikisha watoto wanafaulu ili ubaki kibaruani na kulinda biashara ya bosi wako.

2. Watoto hawalingani uwezo, hivyo wengine wanabaki ili wapate mda wa kutosha kujisomea na kueleweshwa zaidi wakiwa wachache.

3. Urefu wa kamba, hapa kuna hela za twisheni, hivyo walimu ndipo tunapopatia marupurupu.

4. Umbali wa mtoto kutoka nyumbani hadi shuleni; hii inafanya mtoto achukuliwe na gari saa kumi na moja alfajiri na kurudi ni saa kumi na mbili jioni.

Na haya yanafanyika kulinga kwamba kila mzazi anataka mwanaye apate ufaulu mkubwa kitu ambacho walimu kuna mda tunawakaririsha watoto ili mzazi aridhike pale mwanae anapofaulu. Na wazazi wengi wanaridhia kabisa hizo ratiba.

Mwisho; Teknolojia yenyewe imeharibu maadili; mtoto akitoka shule anawaza kwenda kuangalia TV, wengine kucheza PS, sasa si bora wakae shuleni tu, kama mtaani kwenyewe hamna wanalojifunza sababu mtaala huu wa sasa umejaribu kuingiza mambo mengi ya kwenye jamii kwenye masomo yao wanayosoma huko shuleni.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
KIMBIJI SHULE YA MSINGI..KIGAMBONI DSM

mwl mkuu kama upo humu naomba huo utaratibu wa kuwachanganya watoto wa darasa la Saba na la 6 pamoja wakati hata topic za darasa la tano hamkuzimaliza Bado mnawarukisha watoto wasome Mambo ya darasa la Saba hailet tija

Binafsi mnawarudisha nyuma watoto

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom