Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

NINAOMBA MODS HII THREAD WAI'PIN NA IKIWEZEKANA WAIZUNGUSHE KWENYE SOCIAL NETWORKS ZAO ILI WENYE MAMLAKA WALIONE HILI NA WALIFANYIE KAZI...
Naunga mkono hoja , imekuwa kero kubwa walimu wa bongo wanapenda maandalizi zima moto bila kujali kuna athari zipi.
 
Ni kwa sababu za tuition na remedial. Walimu nao wanakula kwa urefu wa kamba zao. Kuna shule wazazi wanatozwa fedha kila wiki kwa ajili huyo. Serikali inawadanganya Kuna Elimu ya Bure?!
Una uhakika?
 
fanya tafiti zaidi. mara nyingi yanakuaga maagizo toka ngazi za juu. Walimu wanapangiwa majukumu ya ziada , wakati mwingine huwa nje ya muda wa kazi. Hamna mwalimu asiependa kupumzika na kufanya shughuli zake za kimaendeleo.
 
KIMBIJI SHULE YA MSINGI..KIGAMBONI DSM

mwl mkuu kama upo humu naomba huo utaratibu wa kuwachanganya watoto wa darasa la Saba na la 6 pamoja wakati hata topic za darasa la tano hamkuzimaliza Bado mnawarukisha watoto wasome Mambo ya darasa la Saba hailet tija

Binafsi mnawarudisha nyuma watoto

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Sasa huyo ni nini anatafuta ..mbona ndio anazidi kuharibu...?
 
Watoto wengine wanakaa umbali mrefu mfano mtaani kwangu watoto wa drs la 7 wanataka saa 11alfajiri na kurudi saa 2 usiku huku wakiwa wamechoka kabisa.
Tulipigieni kelele hili...
 
fanya tafiti zaidi. mara nyingi yanakuaga maagizo toka ngazi za juu. Walimu wanapangiwa majukumu ya ziada , wakati mwingine huwa nje ya muda wa kazi. Hamna mwalimu asiependa kupumzika na kufanya shughuli zake za kimaendeleo.
Basi hili tulipigie kelele...
 
Hao saa 12 mbona afadhali mkuu,kuna hii mikocheni sec wanatoka saa 2usiku
 
Ninachojua mimi nikuwa mfano darasa la saba wanafanya mtihani mwezi wa 9 sasa bila kuongeza muda wa kosoma hawawezi maliza topic, ambazo kikawaida huwa zinaisha mwezi wa 11.
 
Ninachojua mimi nikuwa mfano darasa la saba wanafanya mtihani mwezi wa 9 sasa bila kuongeza muda wa kosoma hawawezi maliza topic, ambazo kikawaida huwa zinaisha mwezi wa 11.
Kwani mitihani hii si ipo miska nenda rudi na mtaala ni huo huo, sasa nini kinafanya mtaala uishe Novemba mtihani uwe Septemba!
 
Huu ujinga umetufikia hata wazazi.
Angalia mtoto wa chekechea au primary hususan hizi shule waita english medium

1. Mtoto anaondoka nyumbani saa 12 anarudi saa 12 jioni

2. Mtoto anabebeshwa mzigo wa begi mgongoni ,vitabu lundo hii kiafya sio poa
Mbona sisi tulikuwa tunaenda shule tena kwa kunawa miguu tu au unajipitisha kwenye nyasi inajiosha yenyewe.
Hakuna tution wala home work lukuki
Lakini tulifanya vzr tu

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Mbona mnalalamika nani kasema wakikaa mpaka jioni wanakua tuition?
1. Ni wao wenyewe wanajisomea
2. Wanasubiri wenzao.
3. Wanacheza.
4. Wanaenda kwa wapenzi wao( mabwana na mabibi)
5. Wanatengeneza connection
6. Umbali na usafiri.
7. Mazoea yakurudi wamechelewa.
8. Kujifunza dini
9. Kusindikizana.
10. Wanahitaji muda wo binafsi kujitafakari, kuliko kurudi home.

Of which is not bad. Msisingizie walimu
 
Hivi hawa watoto wa school bus huwa wanaamshwa saa ngapi?
Ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom