Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

Shida..
 
Serikali ipige marufuku utaratibu wa kumfanyisha mitihani mwanafunzi siku za jumamosi kufanya mitihani 6 kwa masaa matatu halafu wanasahihisha wanafunzi wenyewe.Upimaji wa namna hii hauna tija
 
Baada ya harakati zangu za kuwa busy na shule kuanzia nikiwa little kid mpaka kumaliza chuo , sijalizika na nilichokipata ukilinganisha na muda nilioutumia shule, ndo maana sikuhizi nawaona miyeyusho watu wanaotaka watoto wasome muda wote
 
Hakika tupaaze sauti aisee kinachoharibu watoto siku hizi ni hizo ratiba za masomo zisizo rasmi pamoja na baadhi yawamiliki wa shule za binafsi wanaolazimisha walimu wabaki na watoto muda wote.
Kuna shule moja kule mwanza ratiba ya masomo ilikuwa inaanza saa 10 alfajir. Sijui wameacha??
 
Hakuna matokeo mazuri kutoka a na ukweli kuwa hao watoto wanakalishwa tu, hakuna mwalimu atakayefundisha tangu 12 asubuhi mpaka 12 jioni! Kwa malipo gani?
 
Duh. Ngoja waje wataalamu.

Ila mimi nimechoka kufanya homeworks za wanangu aisee.. yani ada nitoe na homeworks nije nifanye mimi. Hawa walimu hawaaa!!???
Unafanyaje wewe? Pengine umeamua. Kama unatoa ada, iweje umfundishe au umfanyie mwanao kazi zake. Mrudishe akiwa amekosea au hakufanya, update mrejesho kafanywa nini huko shule, ili ukawaulize, nani anayepaswa kumfundisha?
 
Hao walimu walisomea ujinga na wao wanasomesha ujinga.

Mtoto ambae hajafika miaka 14 hapaswi kusomeshwa zaidi ya masaa 2 tu kwa siku, kwa vipindi vya dakika 20 mpaka 30 tu. Tena wanasomeshwa kwa mchezo mchezo.

Mtoto ana haki ya kucheza na kupumzika zaidi ya haki ya kusomeshwa kwa lazima. Mtoe kabisa mwanao shule inayomg'an'ania mtoto kuanzia alfajiri mpaka jioni, utakuta wanafanyishwa mambo ya kijinga jinga tu.
 
Kuna shule nimeikuta huku mbeya,,,,inaitwa MPUGUSO SECONDARY SCHOOL wilayani RUNGWE, sio ya bweni....! wanafunzi wanaenda shule saa kumi na mbili asubuhi wanatoka saa tatu kasoro usiku, imagine saa tatu kasoro usiku!!!!! Sasa shule ni ya kata na kuna mabinti wanaanza safari ya kurudi makwao ambapo ni zaidi ya 3km to 4km.

Siku niliposhuhudia hili nilisisimka sana....haya huyu mwanafunzi ukiacha maswahibu yote anayokutana nayo njiani usiku huo wa saa tatu kasoro, ambapo ni vibaka, walevi, wale wa kumgasi na kumtongoza njiani na uchovu wa zaidi ya masaa 13 ya kukaa kwenye madawati..........! Anapumzika sa ngapi huyu mwanafunzi? Ana refresh mind saa ngap? Anatuliza akili na kujisomea saa ngapi? Anafanya kazi zake za nyumban sa ngap?

WIZARA YA ELIMU IANGALIE HILI SWALA TENA KWA UKARIBU.....kama ni sababu ya ugumu wa vichwa vya wanafunzi basi alie washauri kwamba kuwatoa usiku kutasaidia kulainisha vichwa vya wanafunzi, hakuishia hapo......akaenda mbali mpaka kuwashika na makalio.

stupidy.
 
Uzi umekaa vizuri, haya mambo yanandelea na kufanyika, jambo linalokera ni vile walimu wanatafuta sympathy ya wazazi kupitisha jambo lao so wazazi wanakuwa kinga yao ikitokea kuhoji.

Utasikia"
TULIKUBALIANA KWENYE VIKAO NA WAZAZI" au hayo ni "maamuzi ya wazazi!"
 
Zile kazi za kufanya nyumbani inakua ni kama kazi za wazazi walimu wana relux tuu harafu wanatoa maswali ya kutosha...mwalimu mwingine wa kifaransa nilimfata shuleni anampa mtoto maswali eti kafanye na baba yaani wanajua wote tumesoma wanavyofundisha....shule za siku hizi tunasoma wazazi.
 
Ufaulu na alama za juu kwa watoto was shule NI Credit kwa mwalimu kwakuwa yupo kazini na hvyo ndio vithibitisho kuwa ana piga kazi
Kikubwa ni kulinda maslahi yao binafsi.

#SalaryAndPositionAdiction🤔
 
Haingii akilini mtoto wa darasa la 4 kuanza masomo saa 12 mpaka saa12 jioni au mpaka saa 3 usiku na mbaya zaidi jumamosi pia wanaenda.
Shule za private zinakaririsha watoto muda huo ili tu wafaulu mitihani ya taifa na shule kuonekana inafaulisha hivyo kujitangaza kibiashara.

Shule za serikali wanafanya hivyo wakiamini watapandisha ufaulu na hivyo kutosumbuliwa na wanasiasà.

Kwa kuanza NECTA wabadili namna ya kutangaza matokeo ya mitihani. Kama mtoto amefikisha alama za ufaulu kama ni 30 aandikiwe P (pass) sawa sawa na yule aliepata 80 nae awekewe P. Hii itaondoa utofauti mkubwa wa ufaulu kati ya shule na shule hivyo shule asilimia kubwa kuonekana zinaufaulu sawa.
Iwe kama GS kwa advance.

Hivyo shule ijitangaze kwa vigezo vya miundombinu na huduma zingine na sio matokeo ya mitihani ya watoto wetu waliokaririshwa.
 
Sisi wakati tunasoma darasa la kwanza tunaingia saa mbili tunatoka saa tano. Darasa la pili kuanzia saa sita hadi saa kumi. Na tulikuwa vizuri sana
 
Serikali ipige marufuku utaratibu wa kumfanyisha mitihani mwanafunzi siku za jumamosi kufanya mitihani 6 kwa masaa matatu halafu wanasahihisha wanafunzi wenyewe.Upimaji wa namna hii hauna tija
Huu mtindo uko tokea mwanzoni mwaka 2000 ina maana kwa sasa uko na zaidi ya miaka 20.
Mnafanyana mitihani hasa mnashindanishwa kishule, halafu wanachaguliwa top layer wachache kusaidiana na walimu kusahihisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…