Sababu ipi ilikufanya kujiunga JamiiForums? Mimi ni kikao cha Mwitongo, nikiwa na Makongoro na Mkapa December 2014!

Sababu ipi ilikufanya kujiunga JamiiForums? Mimi ni kikao cha Mwitongo, nikiwa na Makongoro na Mkapa December 2014!

Tarehe 11/12/2014

Pale Mwitongo walikuwapo watu kwa kikao cha Siri hasa Mzee Mkapa ndo alishnikiza kikao kufanyika, nakumbuka tulikuwa watu saba!

Kulikuwa na Threat ndani ya CCM yaan Lowassa, na sasa Wakaanza kujadili how to bow him down !

Mkapa alisema CCM imekuwa kwenye mikono ya walanguzi kwa miaka 10 sasa ! Lazima turudie kuheshimika lazima tuzuie ujinga unaoendelea watu wameshaweka chama mfukoni

Wakasema sasa Mwenyekiti wake Jakaya ndo wa kulitatua Hilo, jibu lilitoka kwa mzee mmoja anaheshimika sana kwamba mfumo ushamuelemea Jakaya na aliulea hivo inatakiwa intervention ya nguvu ! La sivyo CHADEMA ile ya Slaa inabeba nchi!

Nilijifunza mambo mengi Ila Muhimu matano
1. CCM bila Pesa na Ulaghai hutoboi
2. Ukiwa msafi sana unaweza usidumu ikulu
3. Kumbe kuna wazee si wa kushare nao Siri wanakuuza asubuhi na mapema
4. Mkapa aliogopa sana CCM kutoka Madarakani, yaan ilikuwa kama Familia kwake
5. Uchaguzi Tanzania uwa si HURU wala haki ila Wachache wanaojifungia CHAMWINO ndo wanaamua Nani awe Rais

Sera nzito ilikuwa

CHAMA KITOKE KWA WAFANYABIASHARA KIWE KWA WANACHAMA NA WANANCHI
Hapa sasa wakaanza kupendekeza watu ambao wanaweza pitishwa
Wapo hapa kwenye Uzi niliuandika kiutani kumbe nafikisha Ujumbe

Nakumbuka nilijiunga Rasmi Hapa May 21 2015 kwa kazi maalumu,


Sasa yanayoendelea nchini nasubiria CCM kuanguka na hakuna mtu kariba ya Mkapa tena

Kwa sasa Yale yalofanywa na Lowassa naona anayafanya hata Mwigulu, bahati nzuri wote waneshika kiti cha Uwaziri mkuu

Naona kaanza kuhonga watu wamsafishe kwamba ndo mwenyewe 2030 wameanza mapema sana ! Mabilion yanatambaa huko

Britanicca
ok🐒
 
Nilikuwa mwaka wa kwanza, profesa wangu mmoja muhindi alikuwa anapenda kuniita chimbo ananifundisha kuhusu mambo ya imani yao, Chakra, jicho la tatu na mengine kibao.

Siku moja nikaingia google na kisimu changu ki Huwawei, nikagoogle Jicho la la tatu, link ikanileta JF, uzi wa Pasco kama sikosei alikuwa anazungumzia hayo mambo, i was soooo invested. Nikafungua ID…

12 years and counting….
 
Niliingizwa na kijana mahiri sasa ni marehemu jina SHY (Yona Maro) alijiondoa duniani baada ya kujua mke wake ambaye alimuamini sana na huyo mke kwenda Ulaya kusoma aliporudi akahamishiwa mkoa wa Nyanda za Juu Kusini huko akawa anamsaliti mume wake marehemu SHY kwa kutembea na boss wake.

SHY pamoja na umahiri wake kwenye mambo yake lakini alikuwa na udhaifu mmoja mkubwa alikuwa na hasira za papo kwa papo.

RIP SHY
 
Mi nilikuja rasmi kumsagia kunguni Lowassa na kumpitisha Kato cc Pascal Mayalla ambaye baadae alitutesa

Britanicca
Mmojammoja mtatoa siri zenu zote. Kumbe kuna "kazi maalumu nyingi tu humu"?!

Mimi binafsi nilijoliunga rasmi humu mwaka 2010 nikiwa chuo hasa kilichonivutia ni jukwaa la uchumi na lile la historia.

Ghafla nikaanza kuvutiwa na jukwaa la siasa miaka michache mbele baada ya kuona vitu vingi vinavyojadiliwa bungeni vinakuwa vimeanzia huku

Mpaka leo hii ni akaunti kama ya tano sababu ya kusahau password
 
2013 nilikuwa nafwatilia bila kujiunga members kama Nyani Ngabu Mzee Mwanakijiji Chahali Mwanadiwani Pascal Mayalla enzi hizo Pasco wa Jf Hija Madava and etc makala zao zilikuwa moto haswa zilinivuta kujiunga ila Jf ya Sasa haina mvuto kiiiivuo
Ni kweli kabisa haiwezi kuwa na mvuto sababu ya kuwa na chawa kama akina Lucas Mwashambwa,

Tlaatlaah hawa hawatumii ubongo kufikiri bali masaburi, ningekuwa mimi ni admin ningewafurusha hawa ndio walitufanya tuanze kutumia VPN, na kwa upumbafu wao nao wakawa bado wamo tu ilihali ujinga wao ndio uliotufikisha hapa.​

 
2013 nilikuwa nafwatilia bila kujiunga members kama Nyani Ngabu Mzee Mwanakijiji Chahali Mwanadiwani Pascal Mayalla enzi hizo Pasco wa Jf Hija Madava and etc makala zao zilikuwa moto haswa zilinivuta kujiunga ila Jf ya Sasa haina mvuto kiiiivuo
Kipindi hicho anajiita. pasco na ukijaribu kusema we ni mayalla anakuwa mbogo haha

Britanicca
 
JF balaa kipindi hicho
Jamiiforums ya 2010 mpaka 2015 ilikuwa ya moto sana kuna mda unatamani zile moment zirudi sahivi kumejaa watoto na watukaji imekuà hopeless haivutii hata

Uchawa umeiharibu sana jamiiforum na aina za siasa alizozileta magufuli mpaka leo zimeathiri nyanja nyingi sana za habari
 
Jamiiforums ya 2010 mpaka 2015 ilikuwa ya moto sana kuna mda unatamani zile moment zirudi sahivi kumejaa watoto na watunaji hopeless haivutii hata

Uchawa umeiharibu sana jamiiforum na aina za siasa alizozileta magufuli mpaka leo zimeathiri nyanja nyingi sana za habari
Kulikuwa na watu wenye akili sana mpaka ukitaka kuandika kitu unafikiria mara mbili mbili
 
Nilikuwa mwaka wa kwanza, profesa wangu mmoja muhindi alikuwa anapenda kuniita chimbo ananifundisha kuhusu mambo ya imani yao, Chakra, jicho la tatu na mengine kibao.

Siku moja nikaingia google na kisimu changu ki Huwawei, nikagoogle Jicho la la tatu, link ikanileta JF, uzi wa Pasco kama sikosei alikuwa anazungumzia hayo mambo, i was soooo invested. Nikafungua ID…

12 years and counting….
Maxence Melo mpe platinum binti kiziwi
 
Back
Top Bottom