Sababu ipi ilikufanya kujiunga JamiiForums? Mimi ni kikao cha Mwitongo, nikiwa na Makongoro na Mkapa December 2014!

Sababu ipi ilikufanya kujiunga JamiiForums? Mimi ni kikao cha Mwitongo, nikiwa na Makongoro na Mkapa December 2014!

Mimi nilikuwa naogopa kujiunga JF.

Nilikuwa najua JF ni jukwaa la kisiasa, sababu Kaka yangu ambae alikuwa member hapa
Na alikuwa upinzani kindakindaki.

Kwahiyo nikawa nahisi ukijiunga JF moja kwa moja wewe ni mkosoaji wa serikali. ( hadi hivi karibuni kuna watu walikuwa wanaamini hivyo).

Baadae link ndio ikanileta hapa, nika kaa kama dk 10 naona mbona watu wanashusha madini hivyo.
Ndio kufungua acc na kujiunga rasmi.
 
Binafs mwaka 2010 ulikuwa mgumu kwangu baada ya kuacha kaz serikal nakuanza biashàra baadaye mambo yakaniendea kombo nikarud kwa mjomba maeneo fulan hapa dsm yeye n POLISI wa NGAZI za juu kidogo wakat huo ila sasa n DCP

BAS akaja rafikiye kutoka Arusha kahamia hapa mjn na makaz hana so uncle akambeba nikawa nalala nae chumba kimoja sasa alipangiwa kitengo cha intelejensia makao makuu wakamwambia ajiunge JAMII forums huko ndiko wanaowatafuta wapo wengi akaja akaniuliza namna ya kujiunga nokampigia rafik yangu akanielekeza nikamwelekeza

Toka hapo nikawa nam nataka kujua hyo jf ndyo nn kwann polis wanaitaka sana so mwaka 2010 nikajiunga baadaye nikapoteza smu na akaunt ikafia hapo nikaamua kufungua nyingine tofaut na hii

Kwa hyo tuwe macho POLISI wanapiga doria humu Toka way back
 
Mimi nilikuwa naogopa kujiunga JF.

Nilikuwa najua JF ni jukwaa la kisiasa, sababu Kaka yangu ambae alikuwa member hapa
Na alikuwa upinzani kindakindaki.

Kwahiyo nikawa nahisi ukijiunga JF moja kwa moja wewe ni mkosoaji wa serikali. ( hadi hivi karibuni kuna watu walikuwa wanaamini hivyo).

Baadae link ndio ikanileta hapa, nika kaa kama dk 10 naona mbona watu wanashusha madini hivyo.
Ndio kufungua acc na kujiunga rasmi.
bora wewe mimi nilijuaga ni mods wenyewe wanachat anonymously sikujua kama kuna members wanajiunga kuchangia bali kusoma tu nyuzi loh!😅
 
Mimi nilikuwa naogopa kujiunga JF.

Nilikuwa najua JF ni jukwaa la kisiasa, sababu Kaka yangu ambae alikuwa member hapa
Na alikuwa upinzani kindakindaki.

Kwahiyo nikawa nahisi ukijiunga JF moja kwa moja wewe ni mkosoaji wa serikali. ( hadi hivi karibuni kuna watu walikuwa wanaamini hivyo).

Baadae link ndio ikanileta hapa, nika kaa kama dk 10 naona mbona watu wanashusha madini hivyo.
Ndio kufungua acc na kujiunga rasmi.
Hili lilifanya wengi tuchelewe kujiunga

Tulihisi jf ni chungu cha kukaagia senene

Ila Baada ya muda ikapata Uaminifu ambao upo karibu kwisha
 
Tarehe 11/12/2014

Pale Mwitongo walikuwapo watu kwa kikao cha Siri hasa Mzee Mkapa ndo alishnikiza kikao kufanyika, nakumbuka tulikuwa watu saba!

Kulikuwa na Threat ndani ya CCM yaan Lowassa, na sasa Wakaanza kujadili how to bow him down !

Mkapa alisema CCM imekuwa kwenye mikono ya walanguzi kwa miaka 10 sasa ! Lazima turudie kuheshimika lazima tuzuie ujinga unaoendelea watu wameshaweka chama mfukoni

Wakasema sasa Mwenyekiti wake Jakaya ndo wa kulitatua Hilo, jibu lilitoka kwa mzee mmoja anaheshimika sana kwamba mfumo ushamuelemea Jakaya na aliulea hivo inatakiwa intervention ya nguvu ! La sivyo CHADEMA ile ya Slaa inabeba nchi!

Nilijifunza mambo mengi Ila Muhimu matano
1. CCM bila Pesa na Ulaghai hutoboi
2. Ukiwa msafi sana unaweza usidumu ikulu
3. Kumbe kuna wazee si wa kushare nao Siri wanakuuza asubuhi na mapema
4. Mkapa aliogopa sana CCM kutoka Madarakani, yaan ilikuwa kama Familia kwake
5. Uchaguzi Tanzania uwa si HURU wala haki ila Wachache wanaojifungia CHAMWINO ndo wanaamua Nani awe Rais

Sera nzito ilikuwa

CHAMA KITOKE KWA WAFANYABIASHARA KIWE KWA WANACHAMA NA WANANCHI
Hapa sasa wakaanza kupendekeza watu ambao wanaweza pitishwa
Wapo hapa kwenye Uzi niliuandika kiutani kumbe nafikisha Ujumbe

Nakumbuka nilijiunga Rasmi Hapa May 21 2015 kwa kazi maalumu,


Sasa yanayoendelea nchini nasubiria CCM kuanguka na hakuna mtu kariba ya Mkapa tena

Kwa sasa Yale yalofanywa na Lowassa naona anayafanya hata Mwigulu, bahati nzuri wote waneshika kiti cha Uwaziri mkuu

Naona kaanza kuhonga watu wamsafishe kwamba ndo mwenyewe 2030 wameanza mapema sana ! Mabilion yanatambaa huko

Britanicca
Nilifungua acc ya kwanza 2004 lakini kweli nilikuwa na desktop ya familia na mimi nikaamishwa kazi nikapelekwa Rukwa. Niliporudi nikawa nimepoteza kumbukumbu ya accaont, 2008 nikajiunga tena lakini yakanikuta familia ikapata shida ya siasa maana mzee alikuwa kiongozi wa chama dola lakini bi mkubwa alikuwa mlezi wa CHADEMA kwenye kata yetu..
Tukaitwa na kutakiwa tusijihusishe kabisa na siasa za kukosoa chama dola na hivyo mama yangu akakatazwa kujihusisha na siasa mpaka leo hataki.
Mimi nikaachana na Jamii forum kwa kuwa nilikuwa natumika kuandika taarifa furani kwa manufaa ya mtu.
2015 nikajiunga lakini nikajiapiza hii ni kwa ajili ya manufaa yangu sio mtu tena kama nilivyopelekwa Rukwa na kwingine.
Mpaka sasa nipo
 
Jamiiforums ya 2010 mpaka 2015 ilikuwa ya moto sana kuna mda unatamani zile moment zirudi sahivi kumejaa watoto na watukaji imekuà hopeless haivutii hata

Uchawa umeiharibu sana jamiiforum na aina za siasa alizozileta magufuli mpaka leo zimeathiri nyanja nyingi sana za habari
Jf flani tishio

Watu walikuwa wanavujisha siri humu kuanzia siasani hadi kwa celebrities. Ila leo hii jf inategemea social media kupata cha kujadili.

Hakuna taarifa exclusive ama unique advantage

Kiuhalisia kuna ile ladha imepotea ila bado tupo kwa sababu ndio tunaipenda na sometimes kuna mijadala solid
 
Niliingia ofisini miye peke yangu nilikuwa mdogo mdogo. Ninakaa kwenye kiti changu nikafungua Michuzi blog. Jamaa yangu wa pembeni akaniambia Soma Jf ww achana na blog hiyo.
Akanipa ABC za kujiunga.
Nikaanza kuingia km guest member ila 2012 nikajiunga rasmi.
 
Nilifungua acc ya kwanza 2004 lakini kweli nilikuwa na desktop ya familia na mimi nikaamishwa kazi nikapelekwa Rukwa. Niliporudi nikawa nimepoteza kumbukumbu ya accaont, 2008 nikajiunga tena lakini yakanikuta familia ikapata shida ya siasa maana mzee alikuwa kiongozi wa chama dola lakini bi mkubwa alikuwa mlezi wa CHADEMA kwenye kata yetu..
Tukaitwa na kutakiwa tusijihusishe kabisa na siasa za kukosoa chama dola na hivyo mama yangu akakatazwa kujihusisha na siasa mpaka leo hataki.
Mimi nikaachana na Jamii forum kwa kuwa nilikuwa natumika kuandika taarifa furani kwa manufaa ya mtu.
2015 nikajiunga lakini nikajiapiza hii ni kwa ajili ya manufaa yangu sio mtu tena kama nilivyopelekwa Rukwa na kwingine.
Mpaka sasa nipo
HYo nadhan n jambo forum kabla haijawa jf 2008
 
Kwa mara ya kwanza 2009 nikalijua hili jukwaa bahati mbaya 2018 nikapoteza simu nikasahau na nywila account nikaiacha hivyo baadae nikawa sipiti humu kabisaa nikahamia X nilipoona na huko upuuzi mwingi nikarudi humu mazima .Appolinary Mahilane popote ulipo wewe ndio ulisababisha niijue Jf tukiwa ujasi UDOM CVE pale tunakula makande🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom