Sababu kubwa ya Nyerere kumkataa Lowassa asiwe Rais ni utajiri wake uliotokana na urefu wa kamba yake wakati huo!

Huwa najiuliza hivi biashara kubwa kubwa za Edo mpaka kuonekana ana utajiri wa wizi zilikuwa ni zipi hasa?
Mkuu, umesahau alikuwa mkurugenzi wa Arusha International Conference Centre, na Waziri kwa miaka mingi sana kabla ya kugombea uraisi 1995? Kuna watu wanapewa ukurugenzi au uwaziri miaka mitatu tu na wanabadilika kabisa katika hali yao ya kifedha. Kuna namna, sio lazima uibe hela ya serikali. Leo hii ukiambiwa tunakupa kazi utununulie magari 100 tu wizara ya kilimo tayari unaweza kuwa bilionea, au kivuko cha kigamboni.
 
Alikuwa na roho mbaya huyo babu yenu
 
Mada yako ingekuwa na mantiki kama ungelinganisha na EL kukataliwa na CC ya CCM mwaka 2015. Habari ya Samia usingeiingiza hapa.
 
Huu msiba umetubless wale wa upande mwingine ihiiiiiiii,,,, naona JF sasa imetawaliwa na thread za machawa wa msoga na monduli,,,acha tupate burudani
 
Kama hafai kuwa Raisi kwa kuhalalisha watu kufanya ufisadi kwa vile yeye mwenyewe ni fisadi, ni kwa nini unaona anaweza "hakikisha nchi inapata kiongozi aina ya jpm 2025' ????

Halafu kwa nini unataka Rais anaeondoka madarakani ndio akuchagulie Rais ajaye ? Nini maana ya kufanya uchaguzi na kubadilsha viongozi kila baada vipindi fulani kama unataka akili za yule yule aliyekuwepo ndio akuchagulie mrithi? Hivi chui akizeeka anaweza kupendekeza Twiga amrithi madaraka yake mbugani ?

Watanzania tumepikwa tukaiva U-third world wa utawala wa ki-Chifu Chifu. Tumeiva tepe tepe! Mmedanganywa miaka nenda rudi mpaka mkaamini kwamba Rais ndio anapaswa kuchagua Rais, masikini ya Mungu ..... daaaaah.... inauma vibaya sana. Julius Nyerere alianzisha hii trend alipom handpick Ally Mwinyi, right, lakini kuna mambo Baba wa Taifa alikosea jamani, na akaseme kuna ya kijinga tukiyaona tusimfatishe, aliyaita ya kijinga, au hakusema hivyo jamaniii ?????
 
Mada yako ingekuwa na mantiki kama ungelinganisha na EL kukataliwa na CC ya CCM mwaka 2015. Habari ya Samia usingeiingiza hapa.
Mada yangu nimesema inahusu watu wa sasa kuona Lowasa alionewa tangu ile 1995 kwa tuhuma za ufisadi, na kisha na Kikwete 2015. Sasa kwa sababu lengo ilikuwa kujibu hoja ya kwamba alionewa kuwa fisadi na kukataliwa uraisi 1995, ndio maana nikasema mnapaswa muelewe context ya ufisadi ya 1995 chini ya inflence ya Nyerere na context ya sasa chini ya Samia. Na nikzidi kuwaelimisha watu kwamba msimsafishe Lowasa 1995 kwa kutumia context ya sasa ya Samia. In fact, kwa namna Samia alivyo, Nyerere angemkataa Samia kuwa raisi wa Tanzania zaidi ya alivyomkataa Lowasa
 
Nyerere aliongoza watu milioni 20 na sio zaidi Samia anaongoza watu milioni 63.

Wakati wa Mwalimu chuo kikuu kilikuwa kimoja tu na mtu akimaliza masomo anaikuta kazi inamsubiri wakati huu wa Samia akili kichwani mwako, usipokuwa mtundu na mbunifu utakula jeuri yako.
 
Nyerere angekuwepo leo angekuwa ni mzee wa miaka 102 asingekuwa na nguvu ya kuhudhuria vikao vya CCM achilia mbali kuwa na akili yenye uwezo wa kuichagulia TZ yenye watu milioni 63 nani aiongoze.

Mambo ya 1995 yameshapoteza kabisa mantiki leo hii 2024.
 
Kosa la Lowassa kuwa mlutheri tu......hizo zingine zote ni ngonjera
 
Alikuwa na roho mbaya huyo babu yenu
Babu yetu alikuwa na moyo safi sana. Amini nakuambia, kwa namna Samia alivyojionyesha, Nyerere asingekubali NEC imputishe 2025. Yaani hafikii hata points za Lowasa za 1995. Utasemaje vitu kama kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake na wewe ni raisi wa nchi? Unahalalisha ufisadi kwa wachache walio na nafasi?
 
Enyi watu wa kizazi hiki kiovu mnaoona kupewa kuongoza kitengo chenye mianya ya rushwa ni kuukata! Ipo siku ya mapinduzi inakuja mbele yenu, mtalia kilio cha mbwa koko aliepigwa!
 
Umeandika ujinga mtupu. Jiulize yule Dudley alishafanya biashara wapi hadi kumiliki gazeti la Tanzania Daima na jumba Mikocheni? Hao tunaowaona malaika ndo mafisadi wa hatari. CHADEMA ikichukua nchi sio tutasikia Dudley ni shareholder wa migodi ya madini na mmiliki wa majengo city centre?
 
Enyi watu wa kizazi hiki kiovu mnaoona kupewa kuongoza kitengo chenye mianya ya rushwa ni kuukata! Ipo siku ya mapinduzi inakuja mbele yenu, mtalia kilio cha mbwa koko aliepigwa!
Mkuu hizo ni ndoto za mkosaji tu, Mbowe alikuwa mwnaharakati anatisha watu kwa makala zake za gazeti la Tanzania Daima miaka ya 2000 katikati leo hii anaitwa ikulu na analamba asali kama kawaida.
 
Kwa hiyo nyerere alikuwa anamuogopa Lowassa?
Alijuaje mtu kajitajirisha kwa wizi ampe adhabu ya kutogomea Urais badala ya kumfukuza CCM au ashawishi Serikali imuweke ndani. Kunauwezekano jamaa alikuwa a mpunga halali kitambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…