Sababu kubwa ya Nyerere kumkataa Lowassa asiwe Rais ni utajiri wake uliotokana na urefu wa kamba yake wakati huo!

Sababu kubwa ya Nyerere kumkataa Lowassa asiwe Rais ni utajiri wake uliotokana na urefu wa kamba yake wakati huo!

Mkuu nadhani wewe na watu wengi hamfamu nini mama Samia alimaanisha aliposema "kula kwa urefu wa kamba"

Kamba hapa ina maanisha uhali wa kisheria yaani usivuke na kula zaidi ya sheria ilivyokupa yaani ukakata kamba na kula zaidi ya vyako kisheria (ufisadi)

Kamba, yaani sheria inakuwekea eneo lako la kula kihalali na usivuke nje.

Kiswahili si kigumu ila ukikisoma juujuu utapata maana potofu.
Hao wanapotosha kwa makusudi maana iliyokusudiwa kwa nia zao chafu za kisiasa ni wapiga domo na kila awamu huwa hawakosekani.
 
Hali siku hizi ni tofauti sana, hasa chini ya uongozi wa raisi Samia. Kimsingi Samia amehalalisha wanasiasa na viongozi wa serikali kutumia nafasi zao kujitajirisha, na wanapojitajirisha hauwaulizwi maswali yeyote!
Huyu Bibi hana sifa yoyote ya kuwa kiongozi, ni usanii mtupu ndio maana kiki nyingi tu zinafanywa na chawa ili aweze ku trend.
 
Ilikuwa ni Wivu tu wa mwalimu baada ya kuambiwa Lowassa ana kibanda pale SA

Edward hakuwa na Utajiri wowote ila hakuwa na mawazo ya Kimaskini
Na hata hii, eti alikodi ndege ikazunguka nchi nzima, ni uongo, na wawaongopee ambao hawakuwepo, au walikuwa hawajitambui wakati huo. Kwanza Dar tu, watu walijaa na KUSUKUMANA kutaka kumdhamini!
 
Ni kweli, tena kwenda Morogoro kutafuta wadhamini alipanda Abood Bus
 
Back
Top Bottom