Sababu kubwa ya Nyerere kumkataa Lowassa asiwe Rais ni utajiri wake uliotokana na urefu wa kamba yake wakati huo!

Ilikuwa ni Wivu tu wa mwalimu baada ya kuambiwa Lowassa ana kibanda pale SA

Edward hakuwa na Utajiri wowote ila hakuwa na mawazo ya Kimaskini
Be realistic chief.

Wewe hapo, leo unaweza kukodi ndege kutembeza form ya kugombea nafasi ya kiasiasa hata mikoa mitano tu?

Nataka kuamini JKN kwa taarifa toka jikoni hazikuwa zinadanganya. EL 1995 alitoa wapi fedha za kumfanya kuzunguka nchi nzima?

Kama ni mawazo ya utajiri ni jambo jema, ila kwa nafasi zake za utumishi wa umma, alitoa wapi fedha za kukodi ndege, "kununua media na wajumbe" ili aonekane "anakubalika"?

Wazungu wanasema, show me your friend, I can tell, who you're. Mmoja wa marafiki wa EL ndiyo yule mburushi ambae kupitia kampuni zake tumepigwa sana; je, unadhani angeingia jumbe jeupe akiwa na uwahiba na watu kama mburushi ambae Kagoda, EPA, Richmond&Dowans alikuwa nyuma ya pazia, unadhani nini kingebaki?
 
Sawa. Mada inaeleweka sana. Tatizo ni kutumia jina la Samia kama vile mazingira yalibadilika wakati wake au ufisadi ulifikia climax wakati wake. Kilele cha “ufisadi” na fitna zake ni awamu ya nne. Na Lowassa alitelekezwa enzi hiyo na mafisadi wenzake (ref. list of shame).

Kuepuka mpambano usio na tija na machawa wa Samia, muache huyo mama na kamba zake. That was just a gaffe from a simple-minded mswahili lady.
 
Kwani Huyo mburushi sasa hayuko kwenye mifumo ya serikali?

Shujaa Magufuli: Rostam Aziz 2025 gombea ubunge jimbo la Morogoro Mjini

Rais Mwinyi alishatoa ruksa so kuwa Maskini ilikuwa ni chaguo lako 😂

Nyerere aliacha nchi Maskini Kabisa tena mno
 
Walikuwa wawili wale Saleh wa Bakwata na Idd wa Kwacha

Saleh alikuwa kipenzi cha Nyerere na ndiye aliasisi Bakwata taifa

Nawakumbuka bwashee 😄
Sasa ule utajiri wa Mzee Idd Masasi ulikuwa ni wa kawaida kweli kwa miaka ile ?

Nadhani pale mjini ukiwatoa kina Piri Mohamed na Abri nadhani hakuna aliyekuwa na pesa kama Idd.
Watanzania ukiwaambia kwamba kuna watu walikuwa na utajiri mwingi muda mrefu huwa hawakubali.​
 
Mkuu nadhani wewe na watu wengi hamfamu nini mama Samia alimaanisha aliposema "kula kwa urefu wa kamba"

Kamba hapa ina maanisha uhali wa kisheria yaani usivuke na kula zaidi ya sheria ilivyokupa yaani ukakata kamba na kula zaidi ya vyako kisheria (ufisadi)

Kamba, yaani sheria inakuwekea eneo lako la kula kihalali na usivuke nje.

Kiswahili si kigumu ila ukikisoma juujuu utapata maana potofu.
 
Labda vijana wa leo. Nyerere angetaifisha nini kama matajiri wasingekuwepo?

Halafu pamoja na kelele zote za “kijamaa” za nationalization without compensation, double standards ilitumika japo kwa wachache. Nasikia watu kama Mzee John Rupia walikuwa untouchable.
 
Sasa kama kamba ni uhalali wa kisheria, kwa nini aseme msile sana hadi kumaliza na kuvimbiwa? Yaani unataka kusema anataka alitaka kuwa limit watu benefits zao za kisheria?
 
Naam, sasa John Rupia na Iddi Masasi ndiyo watu ambao Mzee Nyerere aliwafuata wakati anataka kuanzisha Azimio la Arusha, kiukweli ni watu ambao walikuwa na utajiri wa kutisha. Hata hivyo wajanja wengi walioingia ndani ya mfumo, wengi walikuwa hawana utajiri wa MONEY IN CASH, bali POSSESSIONS kama ardhi. Waajiriwa wengi wa serikali hasa ndani ya mfumo walinunua sana ardhi sehemu nyingi za Tanzania, na uzuri ilikuwa haijapimwa.

Fedha ilipoanza kuingia kipindi cha Mwinyi na Mkapa, watu waliokuwa na ardhi muda mrefu walitajirika mno. Kuna Mzee alikuwepo kule Tukuyu, alikuwa anafanya kazi Migodini Afrika Kusini kipindi cha Makabulu, alikuwa ana ukwasi wa kutisha kwenye mashamba na mifugo. Miaka ya 60's na 70's watoto wake walisoma Agha Khan Schools, halafu kuna watu wanaamini kwamba watu walikuwa masikini. Wajanja wengi ambao walifanikiwa kutoka nje ya Tanzania kipindi hicho walifunguka akili na kuanza kufanya mambo ya msingi.

Umasikini mkubwa ambao watanzania tunao ni, Lack of Correct Information and Opacity. Serikali ndiyo ina Control The Narrative, ikisema huyu ni fisadi, basi kama makasuku watanzania wanaanza kuamini kwamba huyu ni Fisadi. It's like we're living in a 1984, Orwellian State.​
 
Kwani Nyerere alitaifisha nini cha Wahindi ambacho Rupia nae alikuwa nacho lakinini hakikutaifishwa?
 
Kabisa Kabisa bwashee

Idd Masasi alitisha Sana Iringa na huyu kaka yake Saleh alitisha hapa Mzizima watu hawajui tu kuna matajiri kitambo Sana
 
je, unadhani angeingia jumbe jeupe akiwa na uwahiba na watu kama mburushi ambae Kagoda, EPA, Richmond&Dowans alikuwa nyuma ya pazia, unadhani nini kingebaki?
He is very strategic. Sasa hivi ziara za rais nje ya nchi hakosekani.

Za uhakika zinasema matatizo ya umeme tunayopitia kwa sasa ni mkakati wa kumkabidhi shirika kabla ya 2025.
 
Utajiri sio kitu kibaya.

Tulikuwa na akina Ndesamburo ambao ni wanasiasa matajiri na biashara zao zinafahamika na hawakuwa na harufu ya kukwiba.

Huyo uliemtaja, hata kama ana biashara nyingi, ila mikono yake ni michafu.
Kuna sehemu nyingi sana kahusika kwenye kukwiba ma-bn ya hela. Kumbuka saga EPA ambapo katika 133bn alihusika sana tu.
 
Unakijua kisa cha Mkulima wa mahindi mkinga Sekeni Sanga na Ndesa lakini?! 🐼

Ndesa alikuwa taxi driver tu 😂😂
 
Uyu Bi kilemba ni worse President ever ..nashangaa uko kutaka kugombea tena 2025
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…