Uchaguzi 2020 Sababu kuntu 5 za kwanini Rais Magufuli atashinda tena Uchaguzi huu

Bibie unabonga nini wewe..?nitajie hivyo viwanda? Au kwa kuwa unachezea kirungu Cha mmeo hapo Basi unahisi ni kiwanda...

Endeleeni kudanganywa na huyo muhutu!
Viwanda tulivyonavyo sasa ni 61110 ongezeko la viwanda 8477 toka miaka mitano nyuma, tatizo lenu si tu hamna elimu ila hamjaelimika ndomana matusi ndio silaha kwenu
 
Kwa hiyo saccos watashinda
Saccos yenyewe ni ki group cha wapigaji tu. Hawana huruma na watanzania kabisa, yani hata kusikiliza Sera zao unachangishwa hovyo kabisa. October ndio mwisho wa hio saccos, maana hawata ambulia kitu ili iwe funzo.
 
Viwanda tulivyonavyo sasa ni 61110 ongezeko la viwanda 8477 toka miaka mitano nyuma, tatizo lenu si tu hamna elimu ila hamjaelimika ndomana matusi ndio silaha kwenu
Hebu kuwa muungwana basi...kiwanda unachokijua ni cha hao 'madanga' wako wa kwenye kampeni.
Be humble bibie!
 
Kwa hiyo saccos watashinda
Saccos wapigaji tu. Hawana huruma na watanzania kabisa, yani hata kusikiliza Sera zao unachangishwa hovyo kabisa. Safari hii watanzania tutawashikisha adabu, ili iwe funzo.
 
Hebu kuwa muungwana basi...kiwanda unachokijua ni cha hao 'madanga' wako wa kwenye kampeni.
Be humble bibie!
Kiwanda cha kusindika maziwa cha Milkcom Ltd kilichopo Kigamboni chenye uwekezaji wa Bilion44, kiwanda cha MeatKing pia...attack hoja sio mtu wapinzani wa tanzania hamtokuja shika dola kamwe sababu hamna misingi mizuri
 
Wapinzani wote wamejaa porojo tupu, kwa mtanzania makini hawezi chagua pumba.Kwa aina ya kazi za JPM, wana saccos wajipange upya 2040.
 
Na Bwanku M Bwanku

Dirisha la kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani limefunguliwa na tayali vyama mbalimbali vya siasa vimeanza kazi ya kupita maeneo mbalimbali ya wananchi kunadi sera na mipango yao ili wachaguliwe Oktoba 28.

Kuelekea uchaguzi huu yako mambo ya kuyamulika kwa vyama vya siasa na wagombea wao na nafasi yao kwenye uchaguzi huu. Kwenye mijadala kuelekea uchaguzi huu, leo nakuletea sababu 5 zilizodadavuliwa kwa undani za kueleza kwanini mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli atashinda kwa kishindo na kutetea tena kiti chake cha Urais uchaguzi mkuu huu.

Moja; Kitendo cha vyama vya upinzani kususia uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hili ni moja ya kosa kubwa sana ambalo vyama vya upinzani vilifanya, kosa ambalo litaendelea kuwatafuna sana kwa miaka mitano mpaka 2024 huku kosa hilo likimpa nafasi Rais Magufuli kutetea kiti chake kwa awamu ya pili kwa kishindo sana.

Kususia kwa uchaguzi kwa vyama vya upinzani kunawanyima nafasi vyama vyote vya upinzani kukosa wawakilishi wao hasa wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji ambao wangewasaidia sana kuwaombea kura vyama hivyo kwenye ngazi za chini kabisa za wananchi kule vijijini. Leo vyama vya upinzani kwa makosa yao ya kujitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wanaenda kwenye uchaguzi huu wakiwa kama yatima wasio hata na baba na mama wanaoweza kuwapokea watapoenda mitaani kuomba kura.

Fikilia leo Lissu, Membe au Lipumba akienda kijijini nani ataandaa hata sehemu ya kufanyia mkutano na kuwatafutia kura? Hii inampa nafasi Rais Magufuli kumaliza kazi mapema sana mana tayali ana wawakilishi wengi sana ngazi za chini wanaoweza kufanya kazi hizo kwa ufasaha sana.

Mbili; mtaji mkubwa wa wanachama wa Chama cha mapinduzi; CCM ni moja ya vyama vyenye mtaji mkubwa sana wa wanachama ukilinganisha na vyama vya upinzani. Kwa mujibu wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM- Taifa Humphrey Polepole chama hiko kina zaidi ya wanachama million 14 waliojiandikisha na waliopo kwenye database ya Chama nchi nzima. Hapo unazungumzia idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftali la wapiga kura kuwa million 29 tu.

Kimahesabu ukitoa wale ambao hawatapiga kura na ambao kwa namna CCM inavyopiga kampeni ni dhahili Rais Magufuli atashinda mapema sana. Mtaji huu unampa Rais Magufuli kutafuta kura nje ya CCM akiwa tayali ana mtaji mkubwa wa wanachama ndani ya Chama ambao hawafikiwi hata robo na wanachama wa vyama vya upinzani.

Tatu; kuvunjika kwa UKAWA. Ukawa kama umoja wa vyama vya upinzani ulioungana mwaka 2015 na kumsimamisha mgombea mmoja tu wa Urais kwa kiasi kikubwa sana ulisaidia sana vyama vya upinzani kuihangaisha CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana kura zote za upinzani zilienda kwa mgombea mmoja tu wa upinzani ambae alikuwa ni Lowassa. Hapo unazungumza vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR na NLD ambavyo viliungana.

Kuvunjika kwa umoja huo wa upinzani unaufanya upinzani karibu kila chama kusimamisha mgombea wake hali inayowafanya wapinzani kugawanyika sana kwa makundi ya kugawana kura zaidi ya makundi 10. Kwa mazingira haya upinzani utagawana sana kura na hivyo kumfanya mgombea pekee wa CCM kukusanya kura kama mchele mbele ya kuku.

Nne; kufanyiwa kazi kwa ajenda mama za upinzani na zilizowaumiza sana Watanzania. Moja ya ajenda zilizowapa nguvu kubwa sana na kuufanya upinzani kunawili sana mwaka 2010 mpaka 2015 ilikuwa ni ajenda ya ufisadi. Mpaka mwaka 2015 hoja hiyo ilikuwa ndio mama na kwa kiwango kikubwa ndio iliwatambulisha sana wapinzani. Hata ukija kwa Watanzania kwa kiwango kikubwa sana walikuwa wameielewa hoja ya upinzani kwani wananchi walichoka sana kusikia stori za ufisadi Serikalini na kwenye ofisi za imma zilizowafanya Watanzania kuendelea kudidimia kwenye umaskini.

Hoja hii kwa kiwango kikubwa sana imefanyiwa kazi na Rais Magufuli kwa kuanzisha mahakama ya mafisadi ambayo ilikuwa ikipigiwa kelele sana na wapinzani. Zaidi Rais Magufuli ameshughulika na ufisadi kiwango kinachoonekana na wananchi ikiwemo tumbuatumbua na kukamatwa kwa wahujumu uchumi. Hii imewapa imani sana wananchi na kuona hawana haja tena ya kuipigia kura upinzani wakati tayali mgombea Urais wa CCM kwenye awamu yake ya kwanza tu ameifanyia kazi kwa kiwango kikubwa sana ajenda hiyo iliyowaumiza Watanzania na kuwapa nafasi wapinzani.

Tano; ubabaishaji wa wagombea wengi wa upinzani. Mpaka sasa sera nyingi za wagombea wa vyama vya upinzani ni vichekesho tupu kwa Watanzania wa leo wanaotaka maendeleo baada ya kuchoshwa na kuyasubili kwa muda mrefu sana. Wakati Rais Magufuli akinadi Hapa Kazi Tu na kueleza namna atakavyoendeleza mapinduzi makubwa ya uchumi kwa awamu yake ya pili, upinzani wamejikita kwenye hoja zilizojaa utani, vichekesho na ubinafsi mkubwa.

Leo Chadema wanakwambia Ni yeye tu huku mgombea wao Lissu akitumia muda mwingi kuelezea tukio lake la kupigwa risasi kuliko atakavyotatua shida za wananchi. Mara ACT wakinadi Kazi na Bata, sera iliyojaa mzaha ndani yake huku wengine wakinadi sera ya kugawa ubwabwa kwenye kampeni zao.

Huu ni utani na ubabaishaji wa wazi wazi unaompa nafasi kubwa ya ushindi Rais Magufuli ambae yeye kwenye mikutano yake amekuwa akijikita kueleza namna atavyoongeza na kuboresha huduma za afya, uchumi na miundombinu wezeshi ya barabara na maendeleo

0657475347
Ni JPM pekee, kiongozi mzalendo na mwenye nia ya dhati ya kufanya kazi na watanzania wote.
 
Baada tu ya Uvccm kufunguliwa kutoka kifungoni na Katibu wao Mkuu Bashiru Ali, hatimaye tunaanza kuona cheche zao.
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hoja ya msingi ambayo iko mezani ni JPM kushinda tena. Tunasisitiza Magufuli anashinda, ataendelea kuitumikia nchi kwa uamanifu mkubwa.
 
Kiukweli nimeshiriki na kushuhudia chaguzi nyingi tangu mwaka 1995 kimsingi kwa siasa za upande wa kushoto zimepoteza mwelekeo,,ninaposema zimepoteza mwelekeo ninamaanisha ,,, humu ndani ni home of great think tunahitaji kufikiri sawa sawa .

Sababu ya Kwanza , Raisi aliyepo madarakani kwa sasa ni mtu ambaye ameleta maendeleo katika nyanja tofauti vitu,,na uchumi halali wa watu ,, maisha yamekua Bora zaidi kwa sababu kila mtu anafurahiya matunda ya nchi hii katika uvuvi,uchukuzi,afya na nk.

Nichotaka kusema hotuba za Raisi kwa sasa zinaenda katika namba na sio porojo.

Itaendelea
 
Kiwanda cha kusindika maziwa cha Milkcom Ltd kilichopo Kigamboni chenye uwekezaji wa Bilion44, kiwanda cha MeatKing pia...attack hoja sio mtu wapinzani wa tanzania hamtokuja shika dola kamwe sababu hamna misingi mizuri
Aisee . .hapo ndo umetetea hoja yako..haki ya mama Polepole inabidi awapunguzie dau. !!
 
Na Bwanku M Bwanku

Dirisha la kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani limefunguliwa na tayali vyama mbalimbali vya siasa vimeanza kazi ya kupita maeneo mbalimbali ya wananchi kunadi sera na mipango yao ili wachaguliwe Oktoba 28

Kuelekea uchaguzi huu yako mambo ya kuyamulika kwa vyama vya siasa na wagombea wao na nafasi yao kwenye uchaguzi huu. Kwenye mijadala kuelekea uchaguzi huu, leo nakuletea sababu 5 zilizodadavuliwa kwa undani za kueleza kwanini mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli atashinda kwa kishindo na kutetea tena kiti chake cha Urais Uchaguzi Mkuu huu

Moja; Kitendo cha Vyama vya Upinzani kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hili ni moja ya kosa kubwa sana ambalo vyama vya upinzani vilifanya, kosa ambalo litaendelea kuwatafuna sana kwa miaka mitano mpaka 2024 huku kosa hilo likimpa nafasi Rais Magufuli kutetea kiti chake kwa awamu ya pili kwa kishindo sana.

Kususia kwa uchaguzi kwa vyama vya upinzani kunawanyima nafasi vyama vyote vya upinzani kukosa wawakilishi wao hasa wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji ambao wangewasaidia sana kuwaombea kura vyama hivyo kwenye ngazi za chini kabisa za wananchi kule vijijini. Leo vyama vya upinzani kwa makosa yao ya kujitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wanaenda kwenye uchaguzi huu wakiwa kama yatima wasio hata na baba na mama wanaoweza kuwapokea watapoenda mitaani kuomba kura.

Fikilia leo Lissu, Membe au Lipumba akienda kijijini nani ataandaa hata sehemu ya kufanyia mkutano na kuwatafutia kura? Hii inampa nafasi Rais Magufuli kumaliza kazi mapema sana mana tayali ana wawakilishi wengi sana ngazi za chini wanaoweza kufanya kazi hizo kwa ufasaha sana.

Mbili; mtaji mkubwa wa wanachama wa Chama cha mapinduzi; CCM ni moja ya vyama vyenye mtaji mkubwa sana wa wanachama ukilinganisha na vyama vya upinzani. Kwa mujibu wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM- Taifa Humphrey Polepole chama hiko kina zaidi ya wanachama million 14 waliojiandikisha na waliopo kwenye database ya Chama nchi nzima. Hapo unazungumzia idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftali la wapiga kura kuwa million 29 tu.

Kimahesabu ukitoa wale ambao hawatapiga kura na ambao kwa namna CCM inavyopiga kampeni ni dhahili Rais Magufuli atashinda mapema sana. Mtaji huu unampa Rais Magufuli kutafuta kura nje ya CCM akiwa tayali ana mtaji mkubwa wa wanachama ndani ya Chama ambao hawafikiwi hata robo na wanachama wa vyama vya upinzani.

Tatu; kuvunjika kwa UKAWA. Ukawa kama umoja wa vyama vya upinzani ulioungana mwaka 2015 na kumsimamisha mgombea mmoja tu wa Urais kwa kiasi kikubwa sana ulisaidia sana vyama vya upinzani kuihangaisha CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana kura zote za upinzani zilienda kwa mgombea mmoja tu wa upinzani ambae alikuwa ni Lowassa. Hapo unazungumza vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR na NLD ambavyo viliungana.

Kuvunjika kwa umoja huo wa upinzani unaufanya upinzani karibu kila chama kusimamisha mgombea wake hali inayowafanya wapinzani kugawanyika sana kwa makundi ya kugawana kura zaidi ya makundi 10. Kwa mazingira haya upinzani utagawana sana kura na hivyo kumfanya mgombea pekee wa CCM kukusanya kura kama mchele mbele ya kuku.

Nne; kufanyiwa kazi kwa ajenda mama za upinzani na zilizowaumiza sana Watanzania. Moja ya ajenda zilizowapa nguvu kubwa sana na kuufanya upinzani kunawili sana mwaka 2010 mpaka 2015 ilikuwa ni ajenda ya ufisadi. Mpaka mwaka 2015 hoja hiyo ilikuwa ndio mama na kwa kiwango kikubwa ndio iliwatambulisha sana wapinzani. Hata ukija kwa Watanzania kwa kiwango kikubwa sana walikuwa wameielewa hoja ya upinzani kwani wananchi walichoka sana kusikia stori za ufisadi Serikalini na kwenye ofisi za imma zilizowafanya Watanzania kuendelea kudidimia kwenye umaskini.

Hoja hii kwa kiwango kikubwa sana imefanyiwa kazi na Rais Magufuli kwa kuanzisha mahakama ya mafisadi ambayo ilikuwa ikipigiwa kelele sana na wapinzani. Zaidi Rais Magufuli ameshughulika na ufisadi kiwango kinachoonekana na wananchi ikiwemo tumbuatumbua na kukamatwa kwa wahujumu uchumi. Hii imewapa imani sana wananchi na kuona hawana haja tena ya kuipigia kura upinzani wakati tayali mgombea Urais wa CCM kwenye awamu yake ya kwanza tu ameifanyia kazi kwa kiwango kikubwa sana ajenda hiyo iliyowaumiza Watanzania na kuwapa nafasi wapinzani.

Tano; ubabaishaji wa wagombea wengi wa upinzani. Mpaka sasa sera nyingi za wagombea wa vyama vya upinzani ni vichekesho tupu kwa Watanzania wa leo wanaotaka maendeleo baada ya kuchoshwa na kuyasubili kwa muda mrefu sana. Wakati Rais Magufuli akinadi Hapa Kazi Tu na kueleza namna atakavyoendeleza mapinduzi makubwa ya uchumi kwa awamu yake ya pili, upinzani wamejikita kwenye hoja zilizojaa utani, vichekesho na ubinafsi mkubwa.

Leo Chadema wanakwambia Ni yeye tu huku mgombea wao Lissu akitumia muda mwingi kuelezea tukio lake la kupigwa risasi kuliko atakavyotatua shida za wananchi. Mara ACT wakinadi Kazi na Bata, sera iliyojaa mzaha ndani yake huku wengine wakinadi sera ya kugawa ubwabwa kwenye kampeni zao.

Huu ni utani na ubabaishaji wa wazi wazi unaompa nafasi kubwa ya ushindi Rais Magufuli ambae yeye kwenye mikutano yake amekuwa akijikita kueleza namna atavyoongeza na kuboresha huduma za afya, uchumi na miundombinu wezeshi ya barabara na maendeleo

0657475347
Ni JPM tena. Tunashinda kwa kishindo.
 
Ahsante.. Sakata la Corona tu ni ushindi tosha
Dah mwenyekiti wa saccos alijiweka kimbelembele kutoa modalities za kushinda Corona, akaangukia pua kwa hoja zake za kijinga kabisa. Leo hii tungekuwa kama Kenya kwa lockdown zisizo idadi. Thank God for JPM, hakika watanzania tunajivunia hasa.
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hoja ya msingi ambayo iko mezani ni JPM kushinda tena. Tunasisitiza Magufuli anashinda, ataendelea kuitumikia nchi kwa uamanifu mkubwa.

Hata akishinda, atakusaidia wewe na familia yako. Kwangu mimi hana faida yoyote ile kwenye ustawi wa maisha yangu.
 
Kwa taarifa yako huyo Magufuli wako ni mpinzani kuanzia hapo November 2020.
Jamani ni leo tu TL amekiri jinsi ilivyo vigumu kwa upinzani kushinda (amesema NEC ya raisi, polisi wa raisi, usalama wa taifa wa raisi na mfumo wote wa nchi uko upande wa raisi) wewe ni nani useme JPM atakuwa mpinzani novemba? Huku ni kujitoa ufahamu kwa hali ya juu sana.
 
Subiri utaona
 
Back
Top Bottom