Sababu muhimu zinazoifanya hii kuwa Nyumba ya gharama nafuu zaidi ya vyumba vitatu

1. Yakitoka kwenye gully trap yanaenda wapi?
2.Tatizo kubwa la sewage system kuwa karibu sana na nyumba ni kuwa likipata matatizo hiyo haitakalika kutokana na harufu, uchafu kuzagaa na mimea kukua. Aidha uchafu huo utaathiri sana maji yaliyomo kwenye udongo. Hamna namna ya kulinda nyumba dhidi ya athari hizi mbali ya kuyaweka mbali na eneo la makazi.
Manispaa wanahitaji michoro ya septic tank, soak pit, inspection chambers na inayoonyesha umbali wa septic na soak pit kutoka kwenye makazi. Setback haina uhusiano na population density. Setback ni umbilical unaotakiwa kutoka mipaka ya eneo. Labda ulikuwa una maanisha FAR na plot coverage?
3. Hakuna nyumba isiyohitaji sehemu ya kuhifadhia vitu. Kukosekana kwake ndio kunasababisha vitu kuwekwa sehemu kusikotakiwa. K.m. ndoo zinajaa bafuni, chakula kinatunzwa master.
4. Bado jiko ni dogo mno.
5. Kama eneo ni dogo ungemshauri mhusika ajenge ka ghorofa au nyumba ndogo zaidi . Hii design haifai kwa eneo hilo.

Amandla....
 
1. Ya jikoni yataenda kwenye Mashimo hayohayo but ya dining yatakua na shimo separate coz kuna slope kali ni ngumu kuyafikisha kwenye septic.
2. Setbacks ndio kitu kikubwa wanaangalia mzee, mfano kuna maeneo seckbacks znatakiwa kuwa 1.5m kwa pembeni, 2m nyuma na 5m mbele. Na hizo zinaongezeka kadri eneo linavyokuwa planned kuwa na low density, na hadi hizo “plot coverage” zina standards zake na ndiomaana ni lazima uoneshe “Schedule of Area”.
3. Nimesema hahitaji “store ndani”
4. Standard ya jiko ni ngapi na au hapo unafikiri ni ngapi
5. ……………….. ushauri🙏🏾
 
Mbona mkuu huja sema Kwa Hiyo ramani itagharimu milioni ngapi Hadi Hiyo nyumba imalizike kabisa na familia kuhamia, maana sio wote ma engineers
Soma vizuri point ya kwanza na umepewa “BuiltUp area” ni hesabu ya kuzidisha tu (sidhani mpaka uwe engineer ndio ujue kuzidisha).
Hiyo itakusaidia hata ramani mnazoziona kwenye mitandao (hata za nje), ni kanuni hiyohiyo na standard ya ujenzi wa Tz ndio hiyo nimeweka hapo.
 
🙏🏾Boss. Umeongea point sana🙏🏾
 
Kweli mkuu🙏🏾.
 
Kwa nini nianze kuzidisha Wakati unaweza kumaliza Kila kitu, kama unaweka vitu weka Kila kitu a mpaka z na sio unaweka nusu na robo kisha sisi tumalize maana Kila mtu na upeo na angle of perspective. Nimependa Hiyo nyumba na aina hio ya mchorozela, sasa useme ni Gharama kias gani ili nijipange na ni change karata Zangu vizuri
 
1. Naona bado kuna matatizo. Maji ya jikoni utayapeleka kwenye septic tank au soak pit? Ikiwa kwenye septic tank, mzunguko utakuwa mkubwa mno. Kwa nini usiyapeleke kwenye shimo utakalojenga kwa ajili ya maji ya kutoka dining room.
2. Setbacks hazitofautishi eneo kama ni high density, medium density au low density. Kinacho tofautisha ni plot coverage ( kiasi gani cha eneo kinacho ruhusiwa kufunikwa na jengo) na Floor Area Ratio ambayo inakueleza kiasi gani unaruhusiwa kujenga katika eneo kwa ujumla ( unajumlisha eneo la kila ghorofa halafu unaigawa hiyo jumla na eneo la kiwanja). Schedule of areas inakuwezesha kupiga hesabu ya FAR. Hamna standard ya plot coverage au FAR kwa sababu kila manispaa inajipangia kutokana na ukubwa wa majengo inayotaka katika kila eneo.
3. Ndio maana nikakwambia kuwa kutokuwa na stoo ya ndani kwa mazingira yetu ni upungufu wa Romani yako.
4. Hamna standard size ya jiko ingawa inapendekezwa upana usipungue mita 2.4 na urefu mita 3. Kwa vile haujaweka scale katika mchoro ni vigumu kukisia ukubwa wa jiko lako. Nimesema nilichosema kutokana na vifaa ulivyoweka ndani. Aidha, mlango wako kufungukia ndani unakula nafasi. Hata hivyo kuna vifriji vidogo vinaweza kutosha chini ya kaunta za jikoni.
5. Ushauri? Ondoa dining room, ongeza ukubwa wa living ili itoshe meza ya kulia. Ongeza pia ukubwa wa jiko au veranda ya jiko ili wengine waweze kulia huko.

Amandla...
 
Hawalalamiki una uhakika? Na hayo maisha ya kulala chumba kimoja baba mama na watoto sio something ppl love its just that hawana uwezo.
Toa a better example that one is just inane.
 
Hawalalamiki una uhakika? Na hayo maisha ya kulala chumba kimoja baba mama na watoto sio something ppl love its just that hawana uwezo.
Toa a better example that one is just inane.
Try to think out of the box! Mtu hujikuna pale anapofikia. Huyu jamaa ameleta design ya nyumba ya bei nafuu kwa watu wasio na uwezo mkubwa. Yaani watu ambao wako tayari ku-sacrify hizo issue za ''kugegedena'' au hazina umuhimu kwao kwa cost, just kama watu wa uswahilini wanavyofanya. Kama una noti za kutosha utajenga nyumba ya aina hiyo? Bila shaka ni hapana!
 
Naungana na wewe Kwa upande wa privacy. Lakini ramani inaweza kubaki kama ilivyo, dining ikasogea ilipo sitting room, dirisha likaenda upande wa emergency door Mambo yakawa sawia tu. Nimeipenda ramani yake Ila sina hakika na idadi ya bati.
 
With the same low cost and some minor adjustments mbona hiyo nyumba inawezekana.
 
Hii design ni hovyo ijaangalia swala la privacy hasa kwenye mahaba, unapo design nyumba ya familia kuangalia mahaba ni muhimu Sana.
 
Daahh😁😁. Tatizo wabongo tunapenda sana vitu “rahisi” hatupendi vitu “Halisi”.
Kama bado unaona ngumu kwa maelezo niliyokupa mzee basi iache hiyo haikufai hata kidogo.
Ila kama unataka kujua+kujifunza basi rudi tena kwenye point namba moja
 
Hii design ni hovyo ijaangalia swala la privacy hasa kwenye mahaba, unapo design nyumba ya familia kuangalia mahaba ni muhimu Sana.
😁😁😁 sawa eng. Wa mahaba.
Yani katika vyote umeona ishu ya mahaba tu, daaahh😂😂
 
With the same low cost and some minor adjustments mbona hiyo nyumba inawezekana.
Hebu jaribu ufanye then upost hapa mkuu. Na umesema wewe unataka ya vyumba viwili, na hautaki master ishee ukuta na chumba kingine wala isi shee ukuta na sebule kwaajili ya privacy. Post hapa, kwa vyumba viwili labda uweke unecessary korido just kutenganisha kuta😁😁.
 
Naungana na wewe Kwa upande wa privacy. Lakini ramani inaweza kubaki kama ilivyo, dining ikasogea ilipo sitting room, dirisha likaenda upande wa emergency door Mambo yakawa sawia tu. Nimeipenda ramani yake Ila sina hakika na idadi ya bati.
Boss sijaelewa vizuri kuhusu dirisha kwenda kwenye emergency door lakini dining iki exchange na sittong tayari itakua mbali na jiko, na sebule (wageni wanaka muda mwingi) itakua hapo ambapo milango ya vyumba ipo exposed, yani ndio utakua umeua privacy kabisa.
Kuhusu hesabu ya material ni uhakika by 95+%, na hapo nime add 10% ya wastage kwenye bati
 
Hawalalamiki una uhakika? Na hayo maisha ya kulala chumba kimoja baba mama na watoto sio something ppl love its just that hawana uwezo.
Toa a better example that one is just inane.
Unahisi niliposema “nyumba ya gharama nafuu” niliwalenga wenye pesa.
Nimejaribu kukutumia ramani yenye privacy yakutosha kabisa na umekubali lakini ukasema wewe unataka ya vyumba viwili😂🤣🤣, inamaa pesa no tatizo. Unarudi kwenye nilichojaribu kufanya mimi. Sasa wewe tafuta mtu au kaa tulia then uchore ramani ya vyumba viwili ya gharama bafuu ambayo master haishei ukuta na chumba kingine wala haishei na sebule, af uje uniite “naniii🐕” nipo hapa kwenye huu uzi nakusubiri😁
 
🙏🏾🙏🏾Boss lengo la huu uzi ilikua ni kuja na ramani ya vyumba vitatu (ambayo wengi hupenda kujenga) ya gharama nafuu. Lakini naona wengi wanatoka kwenye lengo la uzi. Kama ni ramani nnazo nyingi saana.
🙏🏾Mkuu
 
Sasa hiyo ramani yake sii dakika sifuri tuu unaipata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…