Black Thought
Senior Member
- Feb 25, 2015
- 161
- 408
- Thread starter
- #41
🙏🏾 Shkrani kwa maoni, ninachokukubali unakuja na maoni yenye logic.1. Naona bado kuna matatizo. Maji ya jikoni utayapeleka kwenye septic tank au soak pit? Ikiwa kwenye septic tank, mzunguko utakuwa mkubwa mno. Kwa nini usiyapeleke kwenye shimo utakalojenga kwa ajili ya maji ya kutoka dining room.
2. Setbacks hazitofautishi eneo kama ni high density, medium density au low density. Kinacho tofautisha ni plot coverage ( kiasi gani cha eneo kinacho ruhusiwa kufunikwa na jengo) na Floor Area Ratio ambayo inakueleza kiasi gani unaruhusiwa kujenga katika eneo kwa ujumla ( unajumlisha eneo la kila ghorofa halafu unaigawa hiyo jumla na eneo la kiwanja). Schedule of areas inakuwezesha kupiga hesabu ya FAR. Hamna standard ya plot coverage au FAR kwa sababu kila manispaa inajipangia kutokana na ukubwa wa majengo inayotaka katika kila eneo.
3. Ndio maana nikakwambia kuwa kutokuwa na stoo ya ndani kwa mazingira yetu ni upungufu wa Romani yako.
4. Hamna standard size ya jiko ingawa inapendekezwa upana usipungue mita 2.4 na urefu mita 3. Kwa vile haujaweka scale katika mchoro ni vigumu kukisia ukubwa wa jiko lako. Nimesema nilichosema kutokana na vifaa ulivyoweka ndani. Aidha, mlango wako kufungukia ndani unakula nafasi. Hata hivyo kuna vifriji vidogo vinaweza kutosha chini ya kaunta za jikoni.
5. Ushauri? Ondoa dining room, ongeza ukubwa wa living ili itoshe meza ya kulia. Ongeza pia ukubwa wa jiko au veranda ya jiko ili wengine waweze kulia huko.
Amandla...
1. Umetoa wazo zuri, ila kwa kawaida moja kati ya kazi muhimu za Septic ni kufanya “skimming” ya maji taka, na maji ya jikoni huwa yakua na skam layer ya mafuta ambayo isipoondolewa inaenda kupunguza ufanisi wa shimo kunyonya maji (mafuta yanatanda kwenye kuta za shimo). So ikilazimu yes yanaweza kuwekwa direct kwenye shimo linalonyonya.
2. Hapa nakubaliana nawewe kwa kiasi kikubwa but still ninachofahamu setbacks huwa zinaangaliwa pia na nimeweka picha hapo uangalie
3. Vitu vingi vinawekwa kwenye makabati ya kikoni siku hizi, mikaa na vingine vinawekwa nje huko, si wote wanataka stoo ya ndani kuna watu nisha wachorea nyumba kubwa na bado hawakutaka store ya ndani
4.ok sawa
5. Hapo kwenye kuondoa dining nafikiri tutaongea yaleyale ni mtazamo wa mtu pia. Ushauri mzuri tho🙏🏾