Sababu nne za kuweka mali kwenye jina la Mama badala ya mpenzi

Sababu nne za kuweka mali kwenye jina la Mama badala ya mpenzi

Kwahiyo ni heri apige mali manzi kuliko mshua wa kambo!?

Mali ni zako.
Mali zinamaana kama ataitumia mwanao tena kwa AKILI.

Mkeo akirithi possibility ya watoto uliozaa naye kufaidika ni kubwa Sana.
Lakini wengine wote akiwemo mamaako, babaako, ndugu zako hawawezi kufaidisha watoto wako.

Kama Mkeo hamna watoto angalau hoja hii inaweza Kupata nguvu.

Kama wewe ni mgumba na umezaliwa pekee yako kwa Mamaako Basi andika Mamaako kwenye hizo Mali.

Watoto hawana haki ya kudai Mali zozote kwa Bibi yao(Mama yako) lakini wanahaki ya kudai Mali kwa mama Yao(Mkeo) ikiwa wewe Baba yao uliacha Mali
 
Ni ubinafsi uliokothiri wa aidha mume au mke. Hiyo ndiyo sababu kuu
 
ukweli haupingiki wanaume tupo kwenye vita na wanawake kupitia ndoa, hawa wanaojifanya kama hawajui yanayoendelea ulimwenguni kwa sasa wanashangaza.
dunia na sheria zote duniani zipo kumkandamiza mwanaume.
inabidi uwe na mbinu za kutosha kupambana wakati unapozidiwa utoke.
wanawake watulivu ni wazamani sio hawa wa sasa tunaokumbana nao.
TAKE CARE NDOA NI VITA HATA AKUONYESHE ANAKUPENDA VIPI.
 
Bora hivyo kuliko achukue mwanamke niliyekutana naye ukubwani

Aliyekuzalia watoto.
Huyo Mamaako anaubavu wa kukuzalia hao watoto ili upate kizazi hapa duniani?

Kama wewe ni mgumba upo sahihi kumpa Mama Mali zako zote lakini kama unakizazi na mmezaliwa wengi huo uamuzi haujawahi kuitwa uamuzi wa HEKIMA.

Uamuzi huo ni kwa kina John Cena na wanaume wote ambao hawajapata watoto.
 
Aliyekuzalia watoto.
Huyo Mamaako anaubavu wa kukuzalia hao watoto ili upate kizazi hapa duniani?

Kama wewe ni mgumba upo sahihi kumpa Mama Mali zako zote lakini kama unakizazi na mmezaliwa wengi huo uamuzi haujawahi kuitwa uamuzi wa HEKIMA.

Uamuzi huo ni kwa kina John Cena na wanaume wote ambao hawajapata watoto.
Mwanamke ni rafiki yangu wa ukubwani....na sio ndugu yangu
 
Tangu Lini ndugu wakarithi Mali?

Wanaorithi Mali ni Watoto.
Kama watoto ni wadogo Mkeo ndio atakuwa msimamizi wa Mali hizo.

Ndugu na Mama yako hawawezi na hawana haki ya kurithi Mali zako
Mimi mali zangu nitawaandika mama yangu ili ndugu zangu waje kurithi.....watoto wangu watarithi kwenye mgao huo
 
Je mkipata divorce halafu mke akapewa watoto inakuwaje!?
Siku yaja ambapo utataka umeze hizi theory zako ila utakuwa umechelewa sana😄😄😄😄

Huyo huyo mke wako unashupaza naye shingo yeye akiwa na mali wewe utakuwa mtu wa mwisho huko kwenye list ya warithi.

Wake up my friend!!!!Najua upo kwenye pick ya ujana na ndoa ila graph ikianza kushuka utayaelewa haya yote kwa mapana🙏

Maisha ya mwanaume ni mafupi sana kama mbio za vijiti,make sure ww ni HUSEIN BOLT and not otherwise maana itakuwa hasara sana katika historia yako ya maisha.
 
Wengi humu wanakomenti kama matahira au wavulana ila ni mara mia ndugu zako wale hiyo mali kuliko mali hiyo ukaona inaliwa na mwanaume mwenzako ambaye anakuwa ndo kakurithi tunda lako,,,hakuna dharau kubwa kama hii😂😂😂.


Nyie wavulana mnaetengeneza kasumba oohhh mara vipi kama maza akifa eleweni tu kuwa hao wanawake zenu bado hamjawajua vizur na siku mkiwajua mtakuwa mmechelewa sana na hamna la kufanya.

Kama humuamini mamako andika watoto na ustate hiyo mali ni WAKFU😁😁😁😁yaani haiuzwi mpaka wewe ufufuke uje ubatilishe hiyo sheria.Unaweza ukaandika watoto lakini mwananke akaja akasimama kama msimamizi wa mali na kama mali zipo anaweza akaanza kucheza rafu na kuanza kutumbua mali.Dawa hapo ni kustate hiyo mali ni WAKFU🥱🥱🥱hapa utakuwa umemaliza maana hata hao watoto hawataweza kuiuza hiyo mali mpaka ufufuke uje utie wino😂😂😂

Huwezi kabisa andikisha ukifa mali zithaminishwe ziuzwe ziwekezwe kwenye hisa/ Bond za serikali then zifunguliwe account hela ziwe zinaingizwa kwa watoto kwa mfumo huo wa divident, hela hizo zitawasaidia kwenye elimu na mambo mengine.

Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake, make use of this son on your favour,,,,,women are selfish creatures use them to your advantage🙏 kama unatumali(vimali),,,,wacha wenye mali waende na hisa/ Bond na WAKFU.

###Stay toxic, be rational 👍always know the game is brutal and not on your favour.Never be soft!!!use ur brain to think not your pen*s!!!!
Jichanganye, utakuja na uzi hapa wa malalamiko hapa. Ndugu wa Kiafrika tunawajua sana, unaweza ukatokea ugomvi huo hadi mwenye mali ukarestishwa in peace. Mimi siwezi kufanya huo ujinga, kama sio kuandikisha watoto basi bora niache liwalo na liwe. Bora kugawana wawili kuliko kundi la watu.
 
Unaandika mali zako jina la mama yako. Unawahi kufa, mama yako anafariki siku chache baadae.
Ndugu zako wanakuja kugawana mali za mama yao, watoto wako wanabakia kuwa machokoraa.
Akili ya kuambiwa changanya za zako, usioe gold digger. Oa mwanamke ambaye unajua mtapambana pamoja, na mtazeeka pamoja.
 
Katika jamii yetu, ni kawaida kwa wanaume kuwekeza katika mali na kuhifadhi fedha zao. Hata hivyo, wengi hujikuta katika mawimbi ya maamuzi magumu kuhusu ni nani anapaswa kuwa mshiriki katika mali hizo. Kwa baadhi ya watu, chaguo lao ni kuweka mali zao na fedha zao kwenye jina la mama zao badala ya mpenzi wao.
Hapa kuna sababu tano ambazo zimenitia moyo kutamani kufanya hivyo:

1. Ulinzi wa Mali katika Nyakati za Mgogoro

Moja ya sababu kuu za kuweka mali kwenye jina la mama ni kulinda mali hizo wakati wa mgogoro, hasa wakati wa talaka au kutengana. Kwa kuwa mama sio mshiriki katika uhusiano wa kimapenzi, mali hiyo itakuwa nje ya mzozo wowote wa kisheria unaoweza kutokea. Hii inasaidia kuhakikisha kuwa mali yako inabaki salama na inalindwa.

2. Uhakika wa Urithi wa mali na fedha zako.

Kuweka mali kwenye jina la mama kunaweza kurahisisha mchakato wa kurithi. Kwa kawaida, sheria nyingi hupa wazazi haki ya kurithi mali za watoto wao. Kwa hivyo, kwa kuweka mali kwenye jina la mama, unahakikisha kuwa itakuwa sehemu ya urithi wake na inapita kwa familia yako.

Ni mara mia ukikata moto mali zote ziwe chini ya bi mkubwa kuliko kwenda kwa bi mdada ambaye kiasili atakwenda kwa mtu mwingine punde tu baada ya wewe kuondoka. Unaweza kuacha nusu ya mali ziende kwa mwanamke endapo kama mmepata baraka ya watoto.

3. Uaminifu na Utulivu wa Kifedha
Mama mara nyingi huwa mtu wa kuaminika na mwenye utulivu wa kifedha. Kwa kuweka mali na fedha zako kwenye akaunti yake, unaweza kuwa na uhakika kuwa fedha zako ziko salama na zitatumika kwa busara.

Mama wako anaweza kukusaidia kusimamia fedha zako, pamoja na miradi yako huku akiwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa zinatumika kwa mahitaji muhimu na kuwekeza kwa busara na wakati mwingine bila kuweka shurti wala mikwara ya kugoma.

4. Kuimarisha mahusiano na Mzazi wako.
Kuweka mali kwenye jina la mama ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano wako na mama yako. Unaonyesha uaminifu wako kwake na uthamini wako kwa mchango wake katika maisha yako. Pia, unahakikisha kuwa ana usalama wa kifedha na anaweza kutegemea msaada wako wakati wowote, ukizingatia ni mama ni mtu ambaye atakuwa nawe kwa uzima na ugonjwa.

Kwa kumalizia, kuweka mali kwenye jina la mama ni chaguo la kibinafsi ambalo linapaswa kufanywa kwa uangalifu. Kwa kuzingatia sababu hizi tano, unaweza kufanya uamuzi sahihi ambao utafaidika wewe na familia yako kwa muda mrefu.

Kwenye purukushani ambazo Ashraf Hakimi pamoja na Ben Zobrist wamezipitia basi wanaume tuna mengi ya kujifunza, muda wowote kinaweza kukuramba mapema sana.
Mali zako andika jina lako mwenyewe, ukiandika jina lako hata ikitokea mwenza mmeachana mtagawa 50/50 utabakiwa na kitu.

Hasara za kuandika majina ya mama, ndugu, ikitokea mama ameenda utapata mgao kidgo kutokana na Mali zilizopo au usipate kbsaa.

Au ukiandika wanao , watoto wa sasa wengi Hawana huruma watakutimua kwenye Mali zako mwenyewe hutobaki hata na mia.

Na kwanini uhangaike kuandika watu wengine wakati uliyehenyeka ni wewe.
 
Back
Top Bottom