Sababu nne za kuweka mali kwenye jina la Mama badala ya mpenzi

Sababu nne za kuweka mali kwenye jina la Mama badala ya mpenzi

Kuna watu waliwahi kujenga nyumba kwenye kiwanja cha baba zao; watoto wote wanajua nyumba ilijengwa na ndugu yao, picha linaanza sasa, Mzee kafariki; wale wale uliokua unadhani ni ndugu zako wanadai nyumba ni ya familia, sasa may be na wewe ndio kipato kimekata, umerudi kwenye nyumba yako..., utajua hujui.
Anyway, unajua kinacho endelea kwa mtoto wa Dr. Mwele Malecela? Bro, hi ni Tanzania, usije uka copy huko na ku paste huku. Naona ume attach na picha ya Hakimi, usisahau pia kupitia historia ya yule mchezaji wa Togo, sijui ni Emmanuel Ebue? Kamsome some nae, ana kitu cha kujifunza kwake
Kipi bora mkuu! Pesa yako ipigwe na ndugu zako au mwanamke ambaye atakwenda kula na mwanaume mwingine!?? Kipi bora Mercedes-Benz yako aendeshe ndugu yako au aendeshe Mwanaume mpya wa ex wako!??
 
Mama yako anaweza je yule mama aliemchoma moto mwanae na petrol je anaweza.
Wamama wote sio sawa

Lakin pia kibongo bongo kwetu je inawezekana mama anawatoto wa 5 tajiri ni mmoja je ataweza tunza mali zako na aache ndugu zako wakiteketea kwenye shimo
La ufukala,

Lakin km ww ni mfuatiliaji mzuri wa wasanii wa kimarekan utaona ata wao pia wanachangamoto
Na wazazi wao britany spear ata beyonce alimuweka mzazi yake manager na mwisho wa sku baba akataka mzurumu mali mwanae

Cha muhimu ni kuomba tu mungu akujalie mke mwema na familia yenye maadili bas
Binadamu hawaaminiki ata mama yako anaweza kukuzunguka
Mimi mali zangu watarithi mke wangu,watoto na shemeji zangu,
Nb:samahani sana msije kusema nimerogwa
 
Kwa dunia ya sasa hakuna nafuu wala afadhali unaweza muamini huyo Mzazi wako na mwisho wa siku akakuzingua vile vile.
Mzazi kukuzingua ni mara chache sana tofauti na wanawake ambao daily wanasababisha majanga kwa wanaume sababu ya mali.
 
Sasa mnaoa ya kazi gani Mkuu?

Si mkae single tu.
Kuoa tunaoa ila Tumeambiwa tuishi nao kwa akili kwa experience yangu ndogo jamaa zangu kadhaa ndoa zao ziliharibika kwa sababu ya migogoro iliyoanzia kwenye mali, mwisho wa siku wanaachana na wanaume kuanza upya.
 
Katika jamii yetu, ni kawaida kwa wanaume kuwekeza katika mali na kuhifadhi fedha zao. Hata hivyo, wengi hujikuta katika mawimbi ya maamuzi magumu kuhusu ni nani anapaswa kuwa mshiriki katika mali hizo. Kwa baadhi ya watu, chaguo lao ni kuweka mali zao na fedha zao kwenye jina la mama zao badala ya mpenzi wao.
Hapa kuna sababu tano ambazo zimenitia moyo kutamani kufanya hivyo:

1. Ulinzi wa Mali katika Nyakati za Mgogoro

Moja ya sababu kuu za kuweka mali kwenye jina la mama ni kulinda mali hizo wakati wa mgogoro, hasa wakati wa talaka au kutengana. Kwa kuwa mama sio mshiriki katika uhusiano wa kimapenzi, mali hiyo itakuwa nje ya mzozo wowote wa kisheria unaoweza kutokea. Hii inasaidia kuhakikisha kuwa mali yako inabaki salama na inalindwa.

2. Uhakika wa Urithi wa mali na fedha zako.

Kuweka mali kwenye jina la mama kunaweza kurahisisha mchakato wa kurithi. Kwa kawaida, sheria nyingi hupa wazazi haki ya kurithi mali za watoto wao. Kwa hivyo, kwa kuweka mali kwenye jina la mama, unahakikisha kuwa itakuwa sehemu ya urithi wake na inapita kwa familia yako.

Ni mara mia ukikata moto mali zote ziwe chini ya bi mkubwa kuliko kwenda kwa bi mdada ambaye kiasili atakwenda kwa mtu mwingine punde tu baada ya wewe kuondoka. Unaweza kuacha nusu ya mali ziende kwa mwanamke endapo kama mmepata baraka ya watoto.

3. Uaminifu na Utulivu wa Kifedha
Mama mara nyingi huwa mtu wa kuaminika na mwenye utulivu wa kifedha. Kwa kuweka mali na fedha zako kwenye akaunti yake, unaweza kuwa na uhakika kuwa fedha zako ziko salama na zitatumika kwa busara.

Mama wako anaweza kukusaidia kusimamia fedha zako, pamoja na miradi yako huku akiwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa zinatumika kwa mahitaji muhimu na kuwekeza kwa busara na wakati mwingine bila kuweka shurti wala mikwara ya kugoma.

4. Kuimarisha mahusiano na Mzazi wako.
Kuweka mali kwenye jina la mama ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano wako na mama yako. Unaonyesha uaminifu wako kwake na uthamini wako kwa mchango wake katika maisha yako. Pia, unahakikisha kuwa ana usalama wa kifedha na anaweza kutegemea msaada wako wakati wowote, ukizingatia ni mama ni mtu ambaye atakuwa nawe kwa uzima na ugonjwa.

Kwa kumalizia, kuweka mali kwenye jina la mama ni chaguo la kibinafsi ambalo linapaswa kufanywa kwa uangalifu. Kwa kuzingatia sababu hizi tano, unaweza kufanya uamuzi sahihi ambao utafaidika wewe na familia yako kwa muda mrefu.

Kwenye purukushani ambazo Ashraf Hakimi pamoja na Ben Zobrist wamezipitia basi wanaume tuna mengi ya kujifunza, muda wowote kinaweza kukuramba mapema sana.
Da!!!,wanawake wamekuwa pasua kichwa sana jamaa!!!,,,,yaani wamekuwa majambazi,,,,,yaani mimi nawaogopa sana,tangu mwenzangu abebe kila ki2 cha ndani,kuanzia fenicha,mafriji,vitanda,magodoro,vitanda,jiko la gesi na m2ngi wake,yaani kila ki2,yhen 2ulikuwa na duka la samaki jumla na rejareja pale banana akahamishia hilo duka sehemu anayoijua yeye na yeye kwenda kupanga sehemu anayoijua mwenyewe{sikutaka kupajua na wala sina mpango wa kupajua],,,,kiukweli nimekufa ganzi kabisa!!! yaani ata nikipanda usafiri wa umma kama daladala akaja mdada kukaa karibu yangu,,,,nasjihisi kama atanichomolea pesa mfukoni,,,then naanza kutoka jasho la hofu huku mwili ukinitetemeka!!!!,,,,,,,,,,kimsingi "IDON'T LOVE THEM AT ALL"...da!!! kudadadadadadadeq!!
 
Pole yako Mkuu! Kikubwa sasa hivi ni kusaini prenup pekee 😔 tunatafuta mwanasheria anakula elfu 50 mnatia saini kabsa
 
Kuoa tunaoa ila Tumeambiwa tuishi nao kwa akili kwa experience yangu ndogo jamaa zangu kadhaa ndoa zao ziliharibika kwa sababu ya migogoro iliyoanzia kwenye mali, mwisho wa siku wanaachana na wanaume kuanza upya.
Sheria za ndoa huwa inampa advantage mwanamke wa kwanza kabsa
 
Pole yako Mkuu! Kikubwa sasa hivi ni kusaini prenup pekee 😔 tunatafuta mwanasheria anakula elfu 50 mnatia saini kabsa
asante sana!!! ila kwa sasa sina mpango wa kuishi tena na mwanamke wa aina yoyote,,,yaliyonitokea ni JINAMIZI zito sana!!!!,,,,,,,,,,,,nilikuwa najiuliza kwa nini YESU KRISTO hakuoa,,,,nikagundua inawezekana alipoona yaliyomkuta ADAM kwa EVA,na yaliyomkuta SAMSON kwa DELILA,akaona bora aishi KISELA tu!!!!,,nae mtume MUHAMMAD S.W.S...akaona dawa yao ni moja tu!!!,,,kuwaoa wengi ili waoneane WIVU,,na kweli kabisa wanaume waliooa wanawake wengi,,hauwezi kusikia wanapata misukosuko,kwani mwanaume akiona zuwena anazengua anaenda kwa halima,akiona asha anazengua anahamia kwa jasmini...mtume MUHAMMAD aliona mbali sana!!!!{amani iwe juu yake]
 
Back
Top Bottom