Sababu Tano kwa nini Mkristo upambane kushinda umasikini wa kipato?

Ina maana wainjilisti, wachungaji, mashemasi, mapadre na maaskofu wana laana maana kila siku wako madhabahuni kuhimiza sadaka kutoka kwa waumini matajiri na masikini kwa kisingizio cha kumpa Mungu wakati wao wanaongea na Mungu usiku na mchana hawapi isipokuwa wakristo
 
Mungu ameweka mfumo wa wao kuendesha maisha yao kupitia zaka na sadaka.

Tatizo wengi wanahofu na Mungu kiasi kutumia ujanjaujanja kushawishi watu kitoa pesa. Pia wengine kugeuka machawa wa matajiri makanisani.

Mimi naamini ukitoq zaka na sadaka kwa mtumishi au kanisa mnufaikaji ni wewe sio mpokeaji. Mshahara wa Mchungaji hauna takwimu. Pesa anazopokea ni 0.001% ya mshahara wote anaolipwa na Mungu. 99.009 inayobaki anatoa Mungu mwenyewe kwa njia zilweza kupimika kifedha na kitakwimu. Mchungaji kupokea sadaka haimaanishi hawezi kufanya kazi nyingine za kipato. Wakati wa Nehemiah waumini wakiacha kuleta sadaka watumishi wakaacha utumishi wakaingia kwenye ukulima na maisha yalienda hadi Nehemia alipokuja kurekebisha mambo.

Ukiona mchungaji anababishwa na Pesa, hajatumwa na Mungu wala hamjui.
 
Masikini hawaendi mbinguni,maana masikini wengi wana roho mbays
Mbinguni wanaingia maskini wa Roho. Watu wanyenyekevu wanaojua wenyewe bila Mungu na msaada wake hawawezi chochote.
Maskini wa Pesa au Tajiri wa Pesa bila unyenyekevu na kujisalimisha kwa mamlaka kuu ya uungu sehemu yao no katika lile ziwa liwakalo moto na kibiriti, Kinyume chake pia no sahihi.
 
Mimi sadaka yangu napeleka kwa wajane, yatima, wazee wasiojiweza na wagonjwa, wachungaji and the likes waje tuungane tukawape wenye uhitaji siyo kujilimbikizia mali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…