Sababu ya Marekani kupiga yowe kuwa nchi za Afrika zinaficha takwimu za Corona ni kuficha aibu kuwa wao taifa kubwa limeshindwa kupambana na Corona!

Sababu ya Marekani kupiga yowe kuwa nchi za Afrika zinaficha takwimu za Corona ni kuficha aibu kuwa wao taifa kubwa limeshindwa kupambana na Corona!

Hilo la mitaa unaenda mbali sana. Tuambie tu kwanza kwenye ukoo wako umepoteza wangapi. Utakacho ona itoshe tu kujua na kwenye koo za wenzako pia hali ni kama hiyo.
Huyu ni wakuonea huruma sana tu
 
Sisi wametuletea vifaa vibovu na tulipo waambia kuwa ni vibovu wakakataa halafu baadae wakakubali
Vifaa tuliagiza wenyewe. Tena china.
Wachina hawa tunaowaita marafiki wa kweli.
Leo hii hao hao ndio walatuletea vipimo feki.
Kwann hatumlaum mchina?
 
L
Kuna korona huko nao wanaficha takwimu sana tu

Hata kama kuna yeyote anaficha. Wewe huoni ni jambo la aibu sana kwa Tanzania kuwa ficha wananchi wake yaani kutuficha sisi?

Wanaoficha takwimu hizi hapa kwetu wanajua maisha ya watu wangapi yanapotea hali yangali weza kuokolewa?

Kama hali ingejulikana kwa usahihi mfano wapi kuliko na hali mbaya zaidi si ambao leo hawapo huko na wazima wasingekuwa wanapanga kwenda huko kesho na hivyo kubakia wazima?

Kwanini bwana 'Union of Soviet Socialist Republics' tusiungane sote pale Lumumba kuwalilia hali hawa viongozi wetu kwa heshima na taadhima tu ili waweza kutambua umuhimu wa takwimu sahihi kwetu kama haki yetu hata kama wao hawataki kutuhami?
 
Hilo la mitaa unaenda mbali sana. Tuambie tu kwanza kwenye ukoo wako umepoteza wangapi. Utakacho ona itoshe tu kujua na kwenye koo za wenzako pia hali ni kama hiyo.
Hivi ninavyoongea kuna dada anazikwa Moshi. Haipiti wiki bila kusikia msiba wa Covid-19.

Watu wengine wanajifunga macho na masikio kwa cognitive dissonance tu.
 
Watatue yakwao kwanza hawa jamaa wana kasumba mbaya sana

Kiufupi USA Kwa sasa si rafiki wa kweli kwa Africa
Wala USA haijawahi kuwa Rafiki wakweli wa Africa,

Marekani hawanaga rafiki wa kudumu bali wao wana maslahi ya kudumu!

Hakuna Mjomba wa Africa huko nje!
 
Ukipewa data zitakusaidia nini

Mfano kama epicenter ni Dar wengine wasio na sababu muhimu yakufanya kuja Dar watabakia waliko salama.

Vivyo hivyo walioko Dar watachukua tahadhari zaidi kutosambaza kwingine kuliko na nafuu.

Huo umuhimu hauna maana yoyote kwako mkuu?
 
We ni mpuuzi sana hao wameandikwa wapi kuwa wamekufa kwa korona. Jinga sana wewe

Mkuu kwani wameandikwa wapi kuwa hawakufa kwa Corona?

Au ni zile changamoto za kupumua ndiyo ungependa azitumie badala ya neno Corona mkuu?
 
Data zinasaidia kujua ukubwa wa tatizo.

Hatuabya kwanza ya kutatua tatizo ni kukubali kuna tatizo.

Sasa ukikataa kutafuta data ni kama umekataa kuna tatizo.

Utataua vipi tatizo ambalo hukubali kwamba lipo?
Mkuu sijui ni tatizo la Taifa au kizazi kilichopo. Kuna ombwe la kufikiri na kutafuta ufahamu.
Takwimu za medical si sawa na takwimu za miti au malimao.

Takwimu za medical zipo katika Bio statistic na hutafsiriwa katika epidemiology.
Maeneo hayo mawili yanafanya kazi kwa pamoja kila moja liki suppliment jingine.

Huwezi kujua uwepo wa tatizo kama huna takwimu. Huwezi kujua trend ya ugonjwa kama huna takwimu.
Huwezi kujua 'factor' za tatizo kama huna takwimu.Huwezi kulikabili tatizo kama huna takwimu.

Mimi sioni kwanini tatizo la dunia Tanzania ilikatae kwa aibu. Leo tunasema hatuna Corona, je, ni kweli hatuna?
At the end of the day waathirika ni sisi na watakaolia au kubaki na tatizo ni sisi.

Nimesoma hoja ya ''takwimu' zinasaidia nini kila siku hapa jamvini. Nilichobaini ni kuwa ima wanaosema hivyo hawajui wanasema nini, au wanajua lakini wanapotosha tu .

Tanzania ni masikini kwasababu ya kizazi kama hiki kisichojua takwimu na bado tunategemea kuingia uchumi wa kati na mentality ya watu hao ambao wengine ni 'senior' katika vyombo mbali mbali tunavyotegemea!
 
Mfano ni hapa TAKWIMU ziko wapi. Kenya nimewapenda, uelewa na usomi uko juu san, wanatoa bila kificho. Sisi mzee baba hataki kusikia Takwimu, watu majumban wanakufa hajali. Wazungu hawana unafiki wanatoa Takwimu ili watu wajue ukubwa wa tatizo
 
Unatia huruma kweli! Hivi suala la kutokutoa taarifa limelalamikiwa Afrika nzima au sisi tuu?

Na unajua kuwa masuala ya Pandemic utoaji taarifa sio sharti la hiari bali lazima kwa dunia nzima ili kulinda na kuchukua hatua kwa wengine?

Madhara tuwezayo kupata kwa hili la kutotoa taarifa za kweli ni kutengwa na huo muziki unakuja kwa kuendekeza akili za kijinga.

Magonjwa yanadhibitiwa kwa kufuata kanuni sio maombi ya siku tatu msimchoshe Mungu kwa uzembe wenu.
Kuna kauli za sijui wivu, yaani US anayekupa ARV na vyandalua bure akuonee wivu masikini kama wewe?

Mbona mnakuwa masikini jeuri hivi?
Jifunzeni kuwa na adabu. Na fuateni masharti ya tiba acheni kudanganywa na Vibwetere wa kizazi hiki.
Bora uwaambie ukweli.... Coz tuna viongozi wengine ni kama wamekuwa machizi... Hutoi taarifaa halafu Kesho unaomba msaada....
 
Naunga mkono hoja,
Kwavile vile nchi za jirani zetu maambukizi na vifo vinaendelea, lakini Tanzania hakuna vifo na hakuna maambukizi, kama huu ndio
Ukweli wenyewe na sio kuficha takwimu, then Marekani anayetutangaza vibaya ndiye muongo, tusimnyamazie kama nilivyo shauri hapa.

COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani?!. Kwanini waseme uongo huu waachwe?.
P
Jamani... Kuna mambo hayahitaji siasa kabisa.... Hasa khs afya za watu.. Mda utasema ukweli cku moja...
 
Mkuu sijui ni tatizo la Taifa au kizazi kilichopo. Kuna ombwe la kufikiri na kutafuta ufahamu.
Takwimu za medical si sawa na takwimu za miti au malimao.

Takwimu za medical zipo katika Bio statistic na hutafsiriwa katika epidemiology.
Maeneo hayo mawili yanafanya kazi kwa pamoja kila moja liki suppliment jingine.

Huwezi kujua uwepo wa tatizo kama huna takwimu. Huwezi kujua trend ya ugonjwa kama huna takwimu.
Huwezi kujua 'factor' za tatizo kama huna takwimu.Huwezi kulikabili tatizo kama huna takwimu.

Mimi sioni kwanini tatizo la dunia Tanzania ilikatae kwa aibu. Leo tunasema hatuna Corona, je, ni kweli hatuna?
At the end of the day waathirika ni sisi na watakaolia au kubaki na tatizo ni sisi.

Nimesoma hoja ya ''takwimu' zinasaidia nini kila siku hapa jamvini. Nilichobaini ni kuwa ima wanaosema hivyo hawajui wanasema nini, au wanajua lakini wanapotosha tu .

Tanzania ni masikini kwasababu ya kizazi kama hiki kisichojua takwimu na bado tunategemea kuingia uchumi wa kati na mentality ya watu hao ambao wengine ni 'senior' katika vyombo mbali mbali tunavyotegemea!

Mkuu umenena sawa sawa kabisa.

Lengo ni upotoshaji wa wazi. Tatizo la kisayansi limefanywa kuwa siasa. Corona au takwimu zinageuka vipi kuwa CCM au CHADEMA? Kwa nini siyo ACT, UDP, NCCR au wengine?

Kama mazezeta tu tunalazimishwa kuamini kuwa hii ni vita vya kiuchumi na eti kuwa tume vishinda kwa na utaratibu huu:

Corona: Siri ya mafanikio yetu katika hii vita
 
Back
Top Bottom