Sababu ya Siasa: Biashara Kariakoo zinakufa kisa kuwapenda na kuwakumbatia machinga

Sababu ya Siasa: Biashara Kariakoo zinakufa kisa kuwapenda na kuwakumbatia machinga

Nimemtunuku sifa hii kutokana na kutumia kwake akili (angalau)katika kujibu hoja.Lakini kuna watu humu instead of giving out their view,wanaanza kuponda na kukashfu.Watu hao hawawezi kutufikisha sehem yoyote.Ni vema zaidi kama tukichangia kwa kutoa hoja zenye msingi na kujenga.
Wakati mwingine mtu anaamua kukejeli kila kitu kwa sababu kila mfumo umeoza siku hizi na matumaini yanapotea kwa kasi Sana.
 
Wakati mwingine mtu anaamua kukejeli kila kitu kwa sababu kila mfumo umeoza siku hizi .na matumaini yanapotea kwa kasi Sana.
Nakushauri endelea kuiamini serikali yako, kuwa mzalendo, penda nchi yako.
Hakuna sababu yoyote ya kuchafua jina la nchi yako.
 
Wore wanao chafua sii wazalendo sijui kwako mwenzangu.
Kama unaipenda nchi yako, si rahisi kujipendekeza kwa mabeberu eti ya "tunyimwe msaada" huo ni uzandiki wa kiwango cha icc
 
Kama unaipenda nchi yako, si rahisi kujipendekeza kwa mabeberu eti ya"tunyimwe msaada" huo ni uzandiki wa kiwango cha icc
Lakini sii kwa kusifia haha uovu, kwenye mapungufu pasemwe huo ndio uzalendo wa kweli.
 
Lakini sii kwa kusifia haha uovu, kwenye mapungufu pasemwe huo ndio uzalendo wa kweli.
Safi, unaonekana ni mtu timamu unayeelewa unafanya nini, sio kujibishana tu na watu wazima humu bila mpangilio wa hoja. Washauri na wenzako
 
Tangu awamu ya 5 ya Rais wetu JPM iingie madarakani imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga. Pamoja na malengo mazuri ya serikali kuwasaidia wamachinga lakini pia wafanyabiashara wenye maduka nao wanatakiwa kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Kama wewe ni mfanyabiashara makini, mmachinga hawezi kukusumbua, hao na ni wafanyabiashara na wananunua mizigo toka kwa wafanyabiashara wenzao.

Mlizoea vya kunyonga sasa mnalia lia, zamani mlikua mnatoa mpaka milioni 40 kwa mwaka kulipia pango uchochoro tu, lakini kodi hamlipi.

Hakuna sheria mpya alizoleta Magufuli, zote ni za Kikwete na Mkapa, lipeni kodi
 
Wamachinga wasumbufu sana k/koo hata kupishana ni tabu tupu coz ya wao kujazana tu.
 
Official address isiyo na tija ya kazi gani?

Piga chini fremu nunua mwamvuli
Ili iweje.....
wateja wangu wa mikoani wanaijua address yangu kamili....
nikiweka mwanvuli watajua nimewehuka
kwa mzigo wa maana wanaoingiza
 
Nasisitiza... kkoo tulikua wale watu wa mwanzo kabisa kuwekeza kwenye 90's. 2015 mzazi wangu akanambia.. " kariakoo haifai tena tuondoke mazima tikaendeleze hizo shughuli zingine kwanza zinatupatia pesa nyingi kuliko hapa" nilikasirika ila nioasema sawa. Sasa najionea mwenyewe.


Nakumbuka tulikuaga na ugomvi kweli na wamachinga. Wenye maduka vs. Machinga. Yaan walikua hawatupendi kbs wanaona kama ndo tunaowachongea. Vipira vikimwagwa enzi hizo ni mawe yanarushwa acheni. Kuna kipindi kulisafishwa balaa. Ila huwezi amini na biashara ikawa mbaya[emoji23][emoji23][emoji119]
Tukaja kukubali kwamba hawa machinga ndo hununua kwetu halaf huwashilisha wateja kwenye korido sema ni wale wa pisi chache chache. Waliporudishwa tena biashara ikarudi. Kwamba tunategemeana.

Wale mara nyingi wanaiuza jeans elf 10 chini huwa mara nyingi ni wale wanataka kuquit kwenye biashara kwahiyo wanapush mzigo uishe. Kuna wale pia wanaotoa copy yaan nguo haina quality hata ila ndo imefanana na ya dukani kwako kila kitu. Uzuri wako wateja wanaojua ubora wa kitu.

Kiujumla kkoo ni biashara kichaa. Kwanza sipendi kabisa kwenda maana ni kero. Usumbufu. Yaan sijui hata kifanyike nini
 
Kwani hujui kwamba wamachinga ndio viwanda vya Magufuli
 
Walishawapa na Vitambulisho , kwa elfu ishirini sasa jamaa wameitumia hiyo fursa.

Mbaya zaidi bidhaa zinapangwa mpaka kwenye njia za waenda kwa miguu.

Ni kero mtindo mmoja,hapa mamlaka zimechemka sana.
 
Tangu awamu ya 5 ya Rais wetu JPM iingie madarakani imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga. Pamoja na malengo mazuri ya serikali kuwasaidia wamachinga lakini pia wafanyabiashara wenye maduka nao wanatakiwa kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Kwa sasa wamachinga wameachiwa huru kufanya lolote watakalo kiasi kwamba wanafanya bishara zao mpaka milangoni mwa Maduka makubwa, mfano mbele ya duka moja machinga wanakaanga chips, moshi wa mafuta huishia kwenye Maduka.

Sidhani kama wafanyabishara kutoka nchi za nje kama CONGO, ZAMBIA, BURUNDI, ZIMBABWE, BURUNDI NA NK wanapendezwa na hali hii, kwa sababu hata kufunga mizigo mkubwa haiwezekani, kushusha mzigo mkubwa mchana haiwezekani.

Machinga hawalipi kodi za pango la bishara, hawalipi leseni za biashara. Swali, hivi serikali inapoteza pesa kiasi gani kutokana na madhara ya wamachinga?

Tunaomba Serikali ilianglie suala kwa jicho la kipekee ikiwa ni pamoja na kuwawekea wamachinga utaratibu mzuri wa kufanya biashara. Serikali imekuwa inakusanya mapato mengi kutoka Kariakoo lakini kwa sasa hali ni mbaya sana kiasi kwamba biashara nyingi zinafungwa.

Je, wafanyabiashara tunaolipa kodi, tukiacha kulipa leseni ya biashara na kodi ya mapato TRA tutakuwa tumefanya makosa?

Ushauri wangu kwa Serikali: Iwatafutie maeneo ya kufanyia biashara, si kwa Kariakoo tu hata maeneo mengine. Maeneo mengi ya watembea kwa miguu machinga wamechiwa kujenga mpaka vibanda vya kudumu kwa kuezekwa na bati. Mfano ni pale standi ya mabasi ya Makonde njia za watembea kwa miguu zimefungwa kwa kujengwa mabanda.

Kwanini wasielekezwe walau waache njia zilizojengwa kwa gharama kubwa? Kariakoo siyo Dubai ya Bongo tena bali imekuwa ni gulio.
Kwakwelii juuu ya hili mkuuu umenena vema, machinga wamepewa kipaumbele zaidi na huku hawalipi kodi au kodi zao ni ndogoo. Sio hapo dar tu karibia miji yote. Utakuta machinga anamwaga mzigo wa takribani milioni mbili na zaidi mbele ya duka la mtu, huku huyo mwenye duka anabidhaa ile ile, sasa lini mteja ataingia dukani na huku bidhaaa hiyohiyo imemwagwa mbele ya duka?? Tunaiomba serikali baada ya kufanya miradi mikubwa ya maendeleo, sasa ianze kujenga masoko ya machinga ilikunuru wafanyabiashara wenye madukaa makubwaa. Kama hawa mama ntilie wamezidi, yaani popote wao nikukoka moto na kupika
 
Kama wewe ni mfanyabiashara makini, mmachinga hawezi kukusumbua, hao na ni wafanyabiashara na wananunua mizigo toka kwa wafanyabiashara wenzao.

Mlizoea vya kunyonga sasa mnalia lia, zamani mlikua mnatoa mpaka milioni 40 kwa mwaka kulipia pango uchochoro tu, lakini kodi hamlipi.

Hakuna sheria mpya alizoleta Magufuli, zote ni za Kikwete na Mkapa, lipeni kodi
Mtaa wa kijani huwa zinapatikana ruzuku kuboresha maisha
 
Nini lengo lako kuu hasa??🤔🤔
lengo lango ni kuwa uwe unasoma post yote na kuielewa kabla ya kutoa mapovu, maana unapotoa mapofu kabla ya kusoma unajidhalilisha wewe na wanaccm wenzako
 
Ndio namna ya kuishi nao tu ili siku wakikuta maduka yote yamefungwa bidhaa zipo nje watakuwa na la kujifunza
Yes, na ukiuzia nje hakuna EFD receipts. Ngoja nitafute vijana km 5 hivi niwe nawapa mzigo asubuhi jioni mahesabu. vita na giant inatakiwa akili.
 
Back
Top Bottom