Wakati mwingine mtu anaamua kukejeli kila kitu kwa sababu kila mfumo umeoza siku hizi na matumaini yanapotea kwa kasi Sana.Nimemtunuku sifa hii kutokana na kutumia kwake akili (angalau)katika kujibu hoja.Lakini kuna watu humu instead of giving out their view,wanaanza kuponda na kukashfu.Watu hao hawawezi kutufikisha sehem yoyote.Ni vema zaidi kama tukichangia kwa kutoa hoja zenye msingi na kujenga.
Nakushauri endelea kuiamini serikali yako, kuwa mzalendo, penda nchi yako.Wakati mwingine mtu anaamua kukejeli kila kitu kwa sababu kila mfumo umeoza siku hizi .na matumaini yanapotea kwa kasi Sana.
Wore wanao chafua sii wazalendo sijui kwako mwenzangu.Nakushauri endelea kuiamini serikali yako,kuwa mzalendo,penda nchi yako.
Hakuna sababu yoyote ya kuchafua jina la nchi yako.
Kama unaipenda nchi yako, si rahisi kujipendekeza kwa mabeberu eti ya "tunyimwe msaada" huo ni uzandiki wa kiwango cha iccWore wanao chafua sii wazalendo sijui kwako mwenzangu.
Hahah mniombeeeeeeeeee nibadilike.Ndio wee nasema rongoo
Lakini sii kwa kusifia haha uovu, kwenye mapungufu pasemwe huo ndio uzalendo wa kweli.Kama unaipenda nchi yako, si rahisi kujipendekeza kwa mabeberu eti ya"tunyimwe msaada" huo ni uzandiki wa kiwango cha icc
Safi, unaonekana ni mtu timamu unayeelewa unafanya nini, sio kujibishana tu na watu wazima humu bila mpangilio wa hoja. Washauri na wenzakoLakini sii kwa kusifia haha uovu, kwenye mapungufu pasemwe huo ndio uzalendo wa kweli.
Hao ni wapiga kura tegemeo wa CCM wasibughudhiweWakifukuzwa, zitapanda nyuzi hapa kama mvua.." Machinga wanyanyaswa kama mbwa kariakoo"
Yani hamueleweki nini shida yenu.
Any way
Kama wewe ni mfanyabiashara makini, mmachinga hawezi kukusumbua, hao na ni wafanyabiashara na wananunua mizigo toka kwa wafanyabiashara wenzao.Tangu awamu ya 5 ya Rais wetu JPM iingie madarakani imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga. Pamoja na malengo mazuri ya serikali kuwasaidia wamachinga lakini pia wafanyabiashara wenye maduka nao wanatakiwa kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Are you stupid or what.....
unajuae maana ya official address!!?
Ili iweje.....Official address isiyo na tija ya kazi gani?
Piga chini fremu nunua mwamvuli
Ili iweje.....
wateja wangu wa mikoani wanaijua address yangu kamili....
nikiweka mwanvuli watajua nimewehuka
kwa mzigo wa maana wanaoingiza
Kwakwelii juuu ya hili mkuuu umenena vema, machinga wamepewa kipaumbele zaidi na huku hawalipi kodi au kodi zao ni ndogoo. Sio hapo dar tu karibia miji yote. Utakuta machinga anamwaga mzigo wa takribani milioni mbili na zaidi mbele ya duka la mtu, huku huyo mwenye duka anabidhaa ile ile, sasa lini mteja ataingia dukani na huku bidhaaa hiyohiyo imemwagwa mbele ya duka?? Tunaiomba serikali baada ya kufanya miradi mikubwa ya maendeleo, sasa ianze kujenga masoko ya machinga ilikunuru wafanyabiashara wenye madukaa makubwaa. Kama hawa mama ntilie wamezidi, yaani popote wao nikukoka moto na kupikaTangu awamu ya 5 ya Rais wetu JPM iingie madarakani imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga. Pamoja na malengo mazuri ya serikali kuwasaidia wamachinga lakini pia wafanyabiashara wenye maduka nao wanatakiwa kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Kwa sasa wamachinga wameachiwa huru kufanya lolote watakalo kiasi kwamba wanafanya bishara zao mpaka milangoni mwa Maduka makubwa, mfano mbele ya duka moja machinga wanakaanga chips, moshi wa mafuta huishia kwenye Maduka.
Sidhani kama wafanyabishara kutoka nchi za nje kama CONGO, ZAMBIA, BURUNDI, ZIMBABWE, BURUNDI NA NK wanapendezwa na hali hii, kwa sababu hata kufunga mizigo mkubwa haiwezekani, kushusha mzigo mkubwa mchana haiwezekani.
Machinga hawalipi kodi za pango la bishara, hawalipi leseni za biashara. Swali, hivi serikali inapoteza pesa kiasi gani kutokana na madhara ya wamachinga?
Tunaomba Serikali ilianglie suala kwa jicho la kipekee ikiwa ni pamoja na kuwawekea wamachinga utaratibu mzuri wa kufanya biashara. Serikali imekuwa inakusanya mapato mengi kutoka Kariakoo lakini kwa sasa hali ni mbaya sana kiasi kwamba biashara nyingi zinafungwa.
Je, wafanyabiashara tunaolipa kodi, tukiacha kulipa leseni ya biashara na kodi ya mapato TRA tutakuwa tumefanya makosa?
Ushauri wangu kwa Serikali: Iwatafutie maeneo ya kufanyia biashara, si kwa Kariakoo tu hata maeneo mengine. Maeneo mengi ya watembea kwa miguu machinga wamechiwa kujenga mpaka vibanda vya kudumu kwa kuezekwa na bati. Mfano ni pale standi ya mabasi ya Makonde njia za watembea kwa miguu zimefungwa kwa kujengwa mabanda.
Kwanini wasielekezwe walau waache njia zilizojengwa kwa gharama kubwa? Kariakoo siyo Dubai ya Bongo tena bali imekuwa ni gulio.
Mtaa wa kijani huwa zinapatikana ruzuku kuboresha maishaKama wewe ni mfanyabiashara makini, mmachinga hawezi kukusumbua, hao na ni wafanyabiashara na wananunua mizigo toka kwa wafanyabiashara wenzao.
Mlizoea vya kunyonga sasa mnalia lia, zamani mlikua mnatoa mpaka milioni 40 kwa mwaka kulipia pango uchochoro tu, lakini kodi hamlipi.
Hakuna sheria mpya alizoleta Magufuli, zote ni za Kikwete na Mkapa, lipeni kodi
lengo lango ni kuwa uwe unasoma post yote na kuielewa kabla ya kutoa mapovu, maana unapotoa mapofu kabla ya kusoma unajidhalilisha wewe na wanaccm wenzakoNini lengo lako kuu hasa??🤔🤔
Yes, na ukiuzia nje hakuna EFD receipts. Ngoja nitafute vijana km 5 hivi niwe nawapa mzigo asubuhi jioni mahesabu. vita na giant inatakiwa akili.Ndio namna ya kuishi nao tu ili siku wakikuta maduka yote yamefungwa bidhaa zipo nje watakuwa na la kujifunza