Kuna sababu nyingi za kuipigia kura ya hapana katiba inayopendekezwa.
Kati ya sababu hizo ni
ubatili wa mchakato wenyewe ambao ulihodhiwa na ccm, kutokuwa na
sifa za msingi za katiba, kutokuwa na
muafaka wa kitaifa zaidi ya kulinda maslahi ya ccm na baadhi ya wabunge hasa wasio na elimu na uwezo,
kuacha mambo ya msingi yaliyopendekezwa na wananchi nk.
Haijaweka mfumo wa kutenganisha mamlaka
(separation of powers) na hivyo inatoa fursa kwa matumizi mabaya ya madaraka (abuse of powers).
Lakini pia katika kuipitia katiba yenyewe inayopendekezwa nimeona mapungufu mengi, hasa katika
muundo wa serikali ambao una mikanganyiko mingi ibara za 1(1), 75, 76, 77 na 163.
Inaruhusu
viongozi wa umma kuwa na fedha nje ya nchi ( ie issue km ya vijisenti vya chenge haitokuwa kashfa tena) ibara 29(2)(b).
Katiba hii pia bado
inapingana katika maeneo mengi na Katiba ya Zanzibar ya mwaka (1984) toleo la 2010.
Tume huru ya uchaguzi ni jina tu, lakini sio huru -
viongozi wake wote wanateuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa ccm - Ibara 217(2) na 222(1).
Nadhani ilikuwa vema kwa Bunge Maalumu
kuzingatia maoni ya Tume ya Jaji Warioba.
N.B
Separation of powers is a political system in which
Legislative,
Executive, and
Judicial are kept distinct in order to prevent
abuse of power and promote a system of
checks and balances.
View attachment 248635